On Mbowe: Man, Family Life and Politics

Status
Not open for further replies.
Already getting EMOTIONAL...ohh dear!

you seem to be missing the points I made in my second post

GT
Kwenye posts zako sijaona jipya hata moja, prove this. wakati wa sakata la Chacha (RIP) ilikuwa na kipimo changu binasfi ya chadema kuhimili siasa za Tanzania. The way walivyokuwa wanasoma maamuzi ya chama nikawapa tano then nikawa nasubiri niangalie hali ya hewa. Ghafla mhe akatutoka na kashfa nyingi zikatoka nikaona upepo wa chadema umetulia. This has convinced me kushabikia chadema. another Tarime by election naona mambo yanaenda vzr na sasa wanachukua mtaji wa kisiasa kwa kupeleka mbele Operation sangara. Nikiwa kama mtanzania wa kawaida tu simjui hata kama Mbowe anatoka familia ya kitajiri anamiliki T/daima, hoteli na club nimeridhika kabisa kuwa Tanzania tuna CUF na CHADEMA.

Kutokana na uelewa wangu ambao haujanitoa sana nje ya nchi kuona mambo ili nijifunze, kicopy then nilocalize hatua za kuamua kumjadili Mbowe ni majungu na ufisadi wa kiswahili ambayo nilifikiri yule mtoto ambae ameathirika na shule za kata pale katani kwangu angeniuliza. But watu kama ni waelewa kama nilivyokuwa nafikiri wewe ungeniambia SWOT analysis ya CHADEMA. Pale kwenye weakness ikaichambua kihalisia na kinadharia then kama dhambia zinaenda kwa Mbowe i will give you big support.

GT, kumbuka hata mtoto wako akifeli usimchape, try to think why na if possible and you are good in Math put down a conceptual modal, what in in and out and expected output na angalia minority input then you will have a very beautfull and strong conclusion. Jaribu kurudi nyuma kuangalia labda akirudi badala ya kujisome unampikilisha au anaangalia sana american football au whatever from there pamoja na encouragement you will see changes. Unajenga uhasama bure tu wakati sisi tuna elekea kwingine.
 
Would you counter argue my second post?

GT kama Jasusi alivyo kutosa nami nakuacha njia panda maana huwa wakati mwingi mwingine unachemka bila ya sababu zozote .Wewe maisha yako yote kwa wazungu unaongelea huko huko you never come down here uone hali halisi ndipo useme .Unapoteza maana kweney forum mkuu japokuwa bado una haki ya kusema uyatakayo .
 
Hope GTna wengine hawataleta tena habari za majungu JF; people are thinking BIG not to MAJUNGU level; tumeshatoka huko; so come up with another strategy maana i know hayo majungu ya kisiasa wakati tukitafuta namna ya kujenga jamii iliyo imara baada ya kuumizwa kwa miaka 50 almost sasa; If we talk of JK we talk of failure; we forget JK was in failure even before he was elected; POLIY/POLICY/KATIBA za vyama/Katiba ya nchi/without revolutionizing this part the country will be poor FOREVER and zaidi tutakuwa tukizidi kupigwa porojo na akina kaka CHILIGATI-nhi inaendelea vema; No how; no way; no CCM 2010
 
Hope GTna wengine hawataleta tena habari za majungu JF; people are thinking BIG not to MAJUNGU level; tumeshatoka huko; so come up with another strategy maana i know hayo majungu ya kisiasa wakati tukitafuta namna ya kujenga jamii iliyo imara baada ya kuumizwa kwa miaka 50 almost sasa; If we talk of JK we talk of failure; we forget JK was in failure even before he was elected; POLIY/POLICY/KATIBA za vyama/Katiba ya nchi/without revolutionizing this part the country will be poor FOREVER and zaidi tutakuwa tukizidi kupigwa porojo na akina kaka CHILIGATI-nhi inaendelea vema; No how; no way; no CCM 2010

Nakupa tano na chukua sasa zingine baadaye .Wapiga porojo na majungu wote hawaji Tanzania miaka yote wako huko huko ughaibuni tuuuuuuuu tumewachoka Yes .
 
Hope GTna wengine hawataleta tena habari za majungu JF; people are thinking BIG not to MAJUNGU level; tumeshatoka huko; so come up with another strategy maana i know hayo majungu ya kisiasa wakati tukitafuta namna ya kujenga jamii iliyo imara baada ya kuumizwa kwa miaka 50 almost sasa; If we talk of JK we talk of failure; we forget JK was in failure even before he was elected; POLIY/POLICY/KATIBA za vyama/Katiba ya nchi/without revolutionizing this part the country will be poor FOREVER and zaidi tutakuwa tukizidi kupigwa porojo na akina kaka CHILIGATI-nhi inaendelea vema; No how; no way; no CCM 2010

Asee kaka umesema kitu ambacho kinagusa hisia za watu moja kwa moja, mwenye akili hawezi kuendeleza malumbano na GT hapa lakini kama kuna anayeungana na GT aendelee kumsupport.
 
wakuu heshima mbele, hivi kuna mtu ameshaona kama hii ina lengo la kuwachonganisha viongozi wakuu wa CHADEMA?

Na isitoshe, nina nani anayeweza kuwa raisi wetu ajaye, ambaye yuko kamili kabisa, bila madoa?

kampeni zimeshaanza kumbe?
 
GT,
I would have loved to engage you in this topic but like Tido Mhando who is a personal friend, Freeman Mbowe is a close relative. So I will sign out. On the other hand let me just say one thing: if the helicopter was not effective how come CCM brought 2 to Tarime?

GT=Jamii Forums-Tido Muhando(Jasusi+Mbowe.)
Kaazi kweli kweli....

NB:Mathematically unatakiwa uidistribute -Tido Muhando kwenye parentheses ya Mbowe na Jasusi lakini this time haiwezekani so jibu ni NO SOLUTION...Kwasababu endapo tukifanya distribution itakuwa Jamii Forums-Tido Muhando-Jasusi-Mbowe...Kitu ambacho si kweli.
 
WHY Mbowe?ina maana katika medani za kisiasa ni mbowe pekee anayeonekana?kuna hiden agenda ambayo inaongoza na mafisadi pamoja na wale ambao wako associated na mafisadi in one way or another wakiamini kuwa kumteteresha Mh.Mbowe ni kukiteteresha CHADEMA and the may reason ni kwamba ktk uongozi wa mh.mbowe kukiongoza Chadema amekiwezesha chama kuwa na mvuto na kuonekana tishio kwa Chama cha mafisadi.vile vile chadema chini ya uongozi wa mbowe wameweza kusimamisha wagombea mamchachari ambao wanaoneka tishio kwa ccm.
 
Kwanza tuufanye URAIS wa NCHI yetu uwe ni TAASISI ndipo tunaweza kumfikiria mtu kama FM kuwa Rais. Vinginevyo ni yaleyale tunayoyasikia ndani ya CHADEMA kwa sasa.
 
JAMANI TUACHE UBISHI HII NCHI IKIONGOZWA NA CHADEMA MAMBO YATAKUWA MAZURI,Maana rais akiwa wa chadema haijarishi ninani awe mboe au siraha hata wewe wote sawa,
Ili mradi tu heshima iwepo kwa rais sio siasa za CCM mtu anaitwa ikulu na Rais anasema (NGOJA NIKAMUONENE HUYU KIJANA WANGU KAKWAMA!! RAIS UNASEMA KIJANA WAKO!!) Hizo ndio siasa za sisiemu ndio maana hawa wazee wa ccm wanapelekea Rais wetu kupigwa mawe maana tayari wamesha mshusha Ukiitwa ikuru hata kama wewe ni mzee wa ccm nenda kwa heshima kuwa unaenda kwa mkuu wako ........eti naenda kwa kijana wangu kakwama matokeo yake wanampa ushauri mbovu mwenzio aenda pigwa mawe huko.

Nadhani Rais yoyote maadamu awe na elimu ya ziada na atoke chama kingine tofauti na ccm maana ccm wazee wake hawana heshima kwa Rais wanaona kuwa wao ndio wamemuweka kumbe kawekwa na Mungu.
 
Huu nimjadala mzuri! Ni sahihi kumjadali "raisi ajaye" naomba tuanze kukiangalia kwanza chama anachokiongoza sasa maana kuna wakati tutalazimika kumuonganisha na chama hasa tutakapotaka kujadali uwezo wa mtuhuru kuongoza!

Chama cha Demokrasia na maendeleo tofauti na vyama vingine ni chama kilichokua kitaasisi na si ukuwaji wa puto(buble growth)kama vilivyo vyama vingine. Ninaposema ukuaaji wa puto nina maana gani? NCCR ilipata ukuaji wa gafla ambao ulitokana na umaaarufu wa watu binafis kwa historian a rekodi zao na si kuwaji wa chama wenye miundo ya kitasisi katika kukiendesha. Kumbuka wake ule NCCR ilikusanya watu wengi mashuhuri waliokuwa tayari wanafahamika kama kina Mrema, Marando, Lamwai,Makongoro, Abrahama Babu, Price Bagenda, Tenga na wengine wengi. Ilionekana kama “dream tema kwa wakati ule. Walichosahau ni kuwa ule ulikuwa ni umaarufu wa watu binafisi, watu waliambatanisha kwanza umaruufu watu kwanza badae chama.Ulikuwa mkusanyiko wa watu wengi wenye uelwea mkubwa na ushashi sana kwenye jamii, lakini udhaifu mkubwa chama kwa wakati ulle kiklikuwa hakina muundo uliokomaa kuweza kupokea haraka na hatimae kuendeleza ukuaji ule wa ghafla. Migogoro kwenye katika jamii ni jambo la kwaida na ipo kila siku kwa chama chochote, wengi wanadhani NCCR ilikufa kwa ajili ya mgogoro, kile kilikuwa kichochoe tu, udhaifu halisi ulikuiwa muundo na uteke wa chama kitaasisi kuweza kuwa na mamlaka zisizotiliwa shaka katika kutatua mogogoro. Matokeo yake mgogoro ule ulikipasua chama katikati, chama kilishutukizwa na ukuaji wa haraka na matokeo yake puto likapasuka!

Wakina Mrema wakahamisha ‘ukuaji’, TLP nayo ikafumka kama puto ila baada ya mda kutokana na kufubaa kisiasa kwa Mrema TLP nayo imechanika msamba kwa maana umaarufu wa chama umejiambatanisha na umaruufu wa mtu. CUF nayo ilipata faida ya kisiasa ya hali ya kihistoria Zanzibar, matokeo ya uchaguzi wa Zanizbar NA Msuguano na mnyukano uliokuwepo kule ulikisogeza chama cha CUF katika ramani za Siasa Tanzania, huu nao hakuwa ukuaji wa kitaasisi wa chama sehemu ikuwa ni umaarufu binafis wa watu Maalims Seif( ambae amawahi kuwa Waziri kiongozi na baadae kufukuzwa chama katika hali iliyotingisha nchi) pia Haji duni shabani Mloo na wengine ukichanganya na makovu ya kihostoria ya kule(jumlisha na makovu ya mapinduzi) CUF ilipata ukuaji bandia. Tofauti na vyama vingine vya upizani ukuaji wa CHADEMA ulikuwa ni ukuaji wa kitaasi, ni kweli waasisi wake kama Mzee Edwin Mtei(Muasi na mwenyekiti wa kwanza) pamoja na Bob Makani(Katibu wa kwanza na mwenyekiti wa pili) kuwa wanajulikana lakini si katika kiwango cha kina Mrema na seif kwa maana hawa ni wataalam Mzee Mtei ni Gavana wa kwanza Mzalendo TZ na badae Kuwa Waziri wa fedha na badae kuja kujiuzulu miaka ya sabini baada ya kutofaotiana kimtazamo na Mwalimu pia Makani amawahi kuwa naibu Gavana. Hawa na wengine waasisi walitulia na kuunda chama kwa unagalifu mkubwa.

Walikuwa na Maono ya mbali walitaka kujenga chama chenye nguvu walitambua wao ni waanzilishi tu kazi itakuja kukamatwa na makamanda wengine hawakutaka kukurupuka! Ndio maana mwaka 1995 CHADEMA hakisimamisha mgombea wa Uraisi bali waliunga Mkono mgombea wa Uraisi wa NCCR kwa wakati ule(Mrema) na mwaka 2000 pia hakumsimamisha mgombea wa uraisi bali walimuunga Mkono mgombea wa CUF(Lipumba) wao walikazana kujenga muundo wa chama na kukijenga kitaasi kwanza! Pia hii ni sifa nyingene muhimu ya CHADEMA, kwamba kinaamini katika siasa zilizojuu ya vyama, yaani ni watanzania kwanza kisha ndio wanachadema na si kuwa wanaccm kwanza kisha watanzania! Ukifuatilia utabaini kwamba kati mwaka 95na 2000 CHADEMA ilikuwa na wabunge wawili tu bungeni(shujaa slaaa-Karatu na Walid Kaborou- kighoma Mjini) ilipofika mwaka 2000 walifanya ongezeko la wabunge toka mili mpaka tano(Slaa-karatu, Walid Kaborou- kighoma Mjini, Freeman-Hai{Takwimu zinasema ndio alikuwa mbunge wa upinzani alingie na kura nyingi kwa mwaka ule}, Ndasemburo(Moshi Mjini) na Grace Kiwelu-Viti maaluum) baada ya hapo mwaka 2005 chama kikaongeza wabunge kufikia 11(slaa, Ndesa,Wange{takwimu zinasema ndie mbunge wa upinzani mwenye kura nyingi kuliko wote}, Saidi Arfi-Mpanda Kati, Zito Zuberi Kabwe- Kigoma Kaskazinina sita wa viti maalum) somo hapa ni kuwa chama kimefanikiwa kutanuka na kuja na ngome mpya za tarime(kanda ya ziwa) na Mpanda Kati(ukuaji wa kustajabisha na kuvutia). Lazima ukumbuke pia kupitia uchaguzi mkuu CHADEMA ina ngoma nyingne nyingi sana zimetengenezwa ambapo wagombea wake ‘walitangaza’ kuwa washindi wa pili haya ni majimbo nusu ya CHADEMA!


Leo tunazungumiza chama pekee chenye wenyeviti wa tatu wa kitaifa tangu kuanzishwa kwake, Mtei, Makani na sasa Mbowe. Kwa hiyo chama kina awamu tatu za uongozi. Unaweza tasfsiri kwamba awamu ya kwanza chini ya mtei ilikuwa na jukumu la kuanzisha na kukipa uhai(survival), awamu ya pili chini ya Makani kujenga miundo imara kitaasi na kukianda chama kwa ukuaji(Maintance) na awamu ya tatu chini ya Mbowe amabyo ina dhima ya kukikuza chama kwa haraka na kukiandaa kuakamata dola. Wachumbuzi wanasema kati ya awamu ya tatu na ya nne ya uongozi wa chama CHADEMA itakuwa chama tawala. Kwwa hiyo kama tunaovyuoona katika mtririko huu CHADEMA imekuwa na ukuaji wa kitaasi na si ukuaji wa puto kama vilivyo vyama vingine.

Awamu ya tatu imeweza kuwa na ujasiri wa kuvutia watu wengi kwa kuwa ina uhakika na miundo yake. Unapovutia watu wengi kwa haraka wanakuja watu wenye mitazamo tofauti na nia tofauti kwa mchanganyiko huo na hulka ya asili mgogoro ni jambo la kawaida swali ni je ipo miundo na taasisi zinazoeleweka kukabili migogoro itakajitokeza na ukuaji huu? Kwa maono ya mbali CHADEMA ilikuwa imekwsiha jiandaa. Majuzi ulipotokea Mgogoro wa Chacha watu walianza kupayuka kuwa ndio mwisho wa chama wakalinganisha na hatma ya NCCR na wanachosahanu ni kuwa kitaasi CHADEMA ilikuwa imekwisha vuka hatua hiyo ya ukuuaji sasa ni taasisi imara, inauwezo kukabili migogoro bila kuathiri au kutingisha uhai wa chama! Mgogoro wa chacha ulitutatuliwa kwa ustadi mkubwa na kufuata taratibu na miongozo ya chama ila kwa saababu kuna watu wenye nia mbaya waliamua kuukuza na kuonyesha kuwa eti chama hakijakomaa? Huu ni unafiki wa ajabu je ni taasisi gani ambayo hakabiliani na migogoro? Migogoro si kipimo cha ukomavu bali uweozo wa kutatua migogoro. Ndio mana hata ukiondoa chacha, Kaboru aliondoka akiwa makamu mwenyekiti pia Shaibu akilwombe akiwa naibu katibu mkuu bila kuathiri chama. CCM nayo ipitia misukosuko mingi katika uhai wake, imewahi kumfukazi unachama makamu mwenyekiti mwanzalishi wake Aboud Jumbe mwaka 84 ambae wakati huo alikuwa ni raisi wa Zanzibar, wakaja wakina Seif mwaka 88 sif akiwa Waziri kiongozi, taifa halipaswi pia kusahau mtikisiko wa Hayati Horace Kolimba amabe amewahi kuwa katibu mkuu amabe mauti yalimkuta katikati ya ‘utatatuzi’ wa mgogoro leo upo mgogoro wa Nape!

Hivyo lazima watu waelewe moigogoro ipo na itaendelea kuwepo! Cha msingi na uimara wa chama katika kuisimamia na kuipatia ufumbuzi, kwa hiyo wanaosubiri CHADEMA ife kwa ajili ya mgogoro kwa maelezo kuwa wapinzani ‘hawajakoma’ wana uhuru wa kufanya hivyo hata mpaka mwisho wa dahari. CHADEMA imweza kuibua na kukuza mashujaa wake yenyewe wapo watu kama Zito Kabwe ambao wamekuwa pamoja na ukuaji wa kitaasi, kwa wasiojua zito alijiambatanisha na CHADEMA tangu akiwa na miaka 16! Freeman mwenyewe amekuwa kisisasa sambambaba na taasisi anayoiongoza kumbuka alianza kama Mkurugenzi ya vijana! Leo wapo watu kama John Mnyika(Bingwa halisi wa harakati na mapambano ya kizazki kipya), Tundu Lissu , Halima Mdee na weng wanaoendela kuibuka kama uyoga.

CCM wanatambua hilo sasa wanatumia kila aina ya uhuni na ufisadi ilikukiondolea uhalali wa kisiasa CHADEMA! Vyama kama CUF, TLP na NCCR sasa vimeingiwa na wivu navyo vinashambulia pia CHADEMA, hawajui wenzao wamefanyia kazi kufika walipo, mvungi juzi kakurupuka kurupukua na kuelezea hisia za viongozi wengine wa vyama vya upinzani dhidi ya CHADEMA! Wenye akili wamekwisha elewa, vyama vingie viweke duara mapambano ya fikra na kimkakati sasa ni kati ya CHADEMA Na CCM. Chaguzi za 2010 na 2015(mwaka wa ahadi ya kinabii) zitakuwa ni chaguzi za kihistroia).


Changamoto iliyonayo sasa CHADEMA ni kuvutia zaidi watu wenye uelewa mkubwa pekee hawa kwa sehemu kubwa ni wachambuzi na wenye uwezo wa kutoa mawazo kukimarisha chama kimakati ni wachache sana wanaweza kuchafuka mikono na kuingia mzigonim hawa sio ‘risk takers’ hufanya mambo yao kwa unagalifu wakitaka kwanza kukamilisha mambo yao binafisi. Ni muhimu sana kuwa na watu hawa lakini kuana haja ya kuwa na mchanganyiko na kuongeza wengi zaidi hasa wale amabao wako tayari kuchafuka mikono ambao wako wachache!

. Itapendeza pia ukikumbuka CHADEMA ndio chama pekee ambao kilipata “endorsement” ya mwalimu Nyerere. Alisoma na kukubali kuwa CHADEMA ndio mbadala wa kweli wa CCM, haya ni maneneno mazito sana toka kwa mwanzalishi wa Chama cha Mapinduzi! Huko nje kuwa ‘endorsesed’ na watu wenye weledi wa mwalimu ni chapuo kubwa sana kisiasa.

Sisemi kuwa CHADEMA hakina hitilafu, zipo za hapa na pale kwa maana kinakuwa na kukabili changamoto kila siku. Utashangaa nikikwambia mimi hukosoa kwa hoja baadhi ya maamuzi ya chama kwa lengo la kujenga. Kwa maana CHADEMA ni chama cha mrengo wa kati(socio0 democrats) kwa hiyo ni muanganiko watu wenye tofauti ndogo juu ya namna ya kuongoza nchi wakati CCM ni chama chenye mguso wa ukumunisti wa kale wenye mtazamo kuwa ni mkusanyiko wa watu waliowa sawa kimtazamo na fikra katika namna ya kuongoza nchi.
 
CHADEMA ndio chama pekee ambao kilipata "endorsement" ya mwalimu Nyerere. Alisoma na kukubali kuwa CHADEMA ndio mbadala wa kweli wa CCM,....

Si kweli. Usimsingizie marehemu wa watu!
 
Huu nimjadala mzuri! Ni sahihi kumjadali "raisi ajaye" naomba tuanze kukiangalia kwanza chama anachokiongoza sasa maana kuna wakati tutalazimika kumuonganisha na chama hasa tutakapotaka kujadali uwezo wa mtuhuru kuongoza!

Chama cha Demokrasia na maendeleo tofauti na vyama vingine ni chama kilichokua kitaasisi na si ukuwaji wa puto(buble growth)kama vilivyo vyama vingine. Ninaposema ukuaaji wa puto nina maana gani? NCCR ilipata ukuaji wa gafla ambao ulitokana na umaaarufu wa watu binafis kwa historian a rekodi zao na si kuwaji wa chama wenye miundo ya kitasisi katika kukiendesha. Kumbuka wake ule NCCR ilikusanya watu wengi mashuhuri waliokuwa tayari wanafahamika kama kina Mrema, Marando, Lamwai,Makongoro, Abrahama Babu, Price Bagenda, Tenga na wengine wengi. Ilionekana kama "dream tema kwa wakati ule. Walichosahau ni kuwa ule ulikuwa ni umaarufu wa watu binafisi, watu waliambatanisha kwanza umaruufu watu kwanza badae chama.Ulikuwa mkusanyiko wa watu wengi wenye uelwea mkubwa na ushashi sana kwenye jamii, lakini udhaifu mkubwa chama kwa wakati ulle kiklikuwa hakina muundo uliokomaa kuweza kupokea haraka na hatimae kuendeleza ukuaji ule wa ghafla. Migogoro kwenye katika jamii ni jambo la kwaida na ipo kila siku kwa chama chochote, wengi wanadhani NCCR ilikufa kwa ajili ya mgogoro, kile kilikuwa kichochoe tu, udhaifu halisi ulikuiwa muundo na uteke wa chama kitaasisi kuweza kuwa na mamlaka zisizotiliwa shaka katika kutatua mogogoro. Matokeo yake mgogoro ule ulikipasua chama katikati, chama kilishutukizwa na ukuaji wa haraka na matokeo yake puto likapasuka!

Wakina Mrema wakahamisha ‘ukuaji', TLP nayo ikafumka kama puto ila baada ya mda kutokana na kufubaa kisiasa kwa Mrema TLP nayo imechanika msamba kwa maana umaarufu wa chama umejiambatanisha na umaruufu wa mtu. CUF nayo ilipata faida ya kisiasa ya hali ya kihistoria Zanzibar, matokeo ya uchaguzi wa Zanizbar NA Msuguano na mnyukano uliokuwepo kule ulikisogeza chama cha CUF katika ramani za Siasa Tanzania, huu nao hakuwa ukuaji wa kitaasisi wa chama sehemu ikuwa ni umaarufu binafis wa watu Maalims Seif( ambae amawahi kuwa Waziri kiongozi na baadae kufukuzwa chama katika hali iliyotingisha nchi) pia Haji duni shabani Mloo na wengine ukichanganya na makovu ya kihostoria ya kule(jumlisha na makovu ya mapinduzi) CUF ilipata ukuaji bandia. Tofauti na vyama vingine vya upizani ukuaji wa CHADEMA ulikuwa ni ukuaji wa kitaasi, ni kweli waasisi wake kama Mzee Edwin Mtei(Muasi na mwenyekiti wa kwanza) pamoja na Bob Makani(Katibu wa kwanza na mwenyekiti wa pili) kuwa wanajulikana lakini si katika kiwango cha kina Mrema na seif kwa maana hawa ni wataalam Mzee Mtei ni Gavana wa kwanza Mzalendo TZ na badae Kuwa Waziri wa fedha na badae kuja kujiuzulu miaka ya sabini baada ya kutofaotiana kimtazamo na Mwalimu pia Makani amawahi kuwa naibu Gavana. Hawa na wengine waasisi walitulia na kuunda chama kwa unagalifu mkubwa.

Walikuwa na Maono ya mbali walitaka kujenga chama chenye nguvu walitambua wao ni waanzilishi tu kazi itakuja kukamatwa na makamanda wengine hawakutaka kukurupuka! Ndio maana mwaka 1995 CHADEMA hakisimamisha mgombea wa Uraisi bali waliunga Mkono mgombea wa Uraisi wa NCCR kwa wakati ule(Mrema) na mwaka 2000 pia hakumsimamisha mgombea wa uraisi bali walimuunga Mkono mgombea wa CUF(Lipumba) wao walikazana kujenga muundo wa chama na kukijenga kitaasi kwanza! Pia hii ni sifa nyingene muhimu ya CHADEMA, kwamba kinaamini katika siasa zilizojuu ya vyama, yaani ni watanzania kwanza kisha ndio wanachadema na si kuwa wanaccm kwanza kisha watanzania! Ukifuatilia utabaini kwamba kati mwaka 95na 2000 CHADEMA ilikuwa na wabunge wawili tu bungeni(shujaa slaaa-Karatu na Walid Kaborou- kighoma Mjini) ilipofika mwaka 2000 walifanya ongezeko la wabunge toka mili mpaka tano(Slaa-karatu, Walid Kaborou- kighoma Mjini, Freeman-Hai{Takwimu zinasema ndio alikuwa mbunge wa upinzani alingie na kura nyingi kwa mwaka ule}, Ndasemburo(Moshi Mjini) na Grace Kiwelu-Viti maaluum) baada ya hapo mwaka 2005 chama kikaongeza wabunge kufikia 11(slaa, Ndesa,Wange{takwimu zinasema ndie mbunge wa upinzani mwenye kura nyingi kuliko wote}, Saidi Arfi-Mpanda Kati, Zito Zuberi Kabwe- Kigoma Kaskazinina sita wa viti maalum) somo hapa ni kuwa chama kimefanikiwa kutanuka na kuja na ngome mpya za tarime(kanda ya ziwa) na Mpanda Kati(ukuaji wa kustajabisha na kuvutia). Lazima ukumbuke pia kupitia uchaguzi mkuu CHADEMA ina ngoma nyingne nyingi sana zimetengenezwa ambapo wagombea wake ‘walitangaza' kuwa washindi wa pili haya ni majimbo nusu ya CHADEMA!


Leo tunazungumiza chama pekee chenye wenyeviti wa tatu wa kitaifa tangu kuanzishwa kwake, Mtei, Makani na sasa Mbowe. Kwa hiyo chama kina awamu tatu za uongozi. Unaweza tasfsiri kwamba awamu ya kwanza chini ya mtei ilikuwa na jukumu la kuanzisha na kukipa uhai(survival), awamu ya pili chini ya Makani kujenga miundo imara kitaasi na kukianda chama kwa ukuaji(Maintance) na awamu ya tatu chini ya Mbowe amabyo ina dhima ya kukikuza chama kwa haraka na kukiandaa kuakamata dola. Wachumbuzi wanasema kati ya awamu ya tatu na ya nne ya uongozi wa chama CHADEMA itakuwa chama tawala. Kwwa hiyo kama tunaovyuoona katika mtririko huu CHADEMA imekuwa na ukuaji wa kitaasi na si ukuaji wa puto kama vilivyo vyama vingine.

Awamu ya tatu imeweza kuwa na ujasiri wa kuvutia watu wengi kwa kuwa ina uhakika na miundo yake. Unapovutia watu wengi kwa haraka wanakuja watu wenye mitazamo tofauti na nia tofauti kwa mchanganyiko huo na hulka ya asili mgogoro ni jambo la kawaida swali ni je ipo miundo na taasisi zinazoeleweka kukabili migogoro itakajitokeza na ukuaji huu? Kwa maono ya mbali CHADEMA ilikuwa imekwsiha jiandaa. Majuzi ulipotokea Mgogoro wa Chacha watu walianza kupayuka kuwa ndio mwisho wa chama wakalinganisha na hatma ya NCCR na wanachosahanu ni kuwa kitaasi CHADEMA ilikuwa imekwisha vuka hatua hiyo ya ukuuaji sasa ni taasisi imara, inauwezo kukabili migogoro bila kuathiri au kutingisha uhai wa chama! Mgogoro wa chacha ulitutatuliwa kwa ustadi mkubwa na kufuata taratibu na miongozo ya chama ila kwa saababu kuna watu wenye nia mbaya waliamua kuukuza na kuonyesha kuwa eti chama hakijakomaa? Huu ni unafiki wa ajabu je ni taasisi gani ambayo hakabiliani na migogoro? Migogoro si kipimo cha ukomavu bali uweozo wa kutatua migogoro. Ndio mana hata ukiondoa chacha, Kaboru aliondoka akiwa makamu mwenyekiti pia Shaibu akilwombe akiwa naibu katibu mkuu bila kuathiri chama. CCM nayo ipitia misukosuko mingi katika uhai wake, imewahi kumfukazi unachama makamu mwenyekiti mwanzalishi wake Aboud Jumbe mwaka 84 ambae wakati huo alikuwa ni raisi wa Zanzibar, wakaja wakina Seif mwaka 88 sif akiwa Waziri kiongozi, taifa halipaswi pia kusahau mtikisiko wa Hayati Horace Kolimba amabe amewahi kuwa katibu mkuu amabe mauti yalimkuta katikati ya ‘utatatuzi' wa mgogoro leo upo mgogoro wa Nape!

Hivyo lazima watu waelewe moigogoro ipo na itaendelea kuwepo! Cha msingi na uimara wa chama katika kuisimamia na kuipatia ufumbuzi, kwa hiyo wanaosubiri CHADEMA ife kwa ajili ya mgogoro kwa maelezo kuwa wapinzani ‘hawajakoma' wana uhuru wa kufanya hivyo hata mpaka mwisho wa dahari. CHADEMA imweza kuibua na kukuza mashujaa wake yenyewe wapo watu kama Zito Kabwe ambao wamekuwa pamoja na ukuaji wa kitaasi, kwa wasiojua zito alijiambatanisha na CHADEMA tangu akiwa na miaka 16! Freeman mwenyewe amekuwa kisisasa sambambaba na taasisi anayoiongoza kumbuka alianza kama Mkurugenzi ya vijana! Leo wapo watu kama John Mnyika(Bingwa halisi wa harakati na mapambano ya kizazki kipya), Tundu Lissu , Halima Mdee na weng wanaoendela kuibuka kama uyoga.

CCM wanatambua hilo sasa wanatumia kila aina ya uhuni na ufisadi ilikukiondolea uhalali wa kisiasa CHADEMA! Vyama kama CUF, TLP na NCCR sasa vimeingiwa na wivu navyo vinashambulia pia CHADEMA, hawajui wenzao wamefanyia kazi kufika walipo, mvungi juzi kakurupuka kurupukua na kuelezea hisia za viongozi wengine wa vyama vya upinzani dhidi ya CHADEMA! Wenye akili wamekwisha elewa, vyama vingie viweke duara mapambano ya fikra na kimkakati sasa ni kati ya CHADEMA Na CCM. Chaguzi za 2010 na 2015(mwaka wa ahadi ya kinabii) zitakuwa ni chaguzi za kihistroia).


Changamoto iliyonayo sasa CHADEMA ni kuvutia zaidi watu wenye uelewa mkubwa pekee hawa kwa sehemu kubwa ni wachambuzi na wenye uwezo wa kutoa mawazo kukimarisha chama kimakati ni wachache sana wanaweza kuchafuka mikono na kuingia mzigonim hawa sio ‘risk takers' hufanya mambo yao kwa unagalifu wakitaka kwanza kukamilisha mambo yao binafisi. Ni muhimu sana kuwa na watu hawa lakini kuana haja ya kuwa na mchanganyiko na kuongeza wengi zaidi hasa wale amabao wako tayari kuchafuka mikono ambao wako wachache!

. Itapendeza pia ukikumbuka CHADEMA ndio chama pekee ambao kilipata "endorsement" ya mwalimu Nyerere. Alisoma na kukubali kuwa CHADEMA ndio mbadala wa kweli wa CCM, haya ni maneneno mazito sana toka kwa mwanzalishi wa Chama cha Mapinduzi! Huko nje kuwa ‘endorsesed' na watu wenye weledi wa mwalimu ni chapuo kubwa sana kisiasa.

Sisemi kuwa CHADEMA hakina hitilafu, zipo za hapa na pale kwa maana kinakuwa na kukabili changamoto kila siku. Utashangaa nikikwambia mimi hukosoa kwa hoja baadhi ya maamuzi ya chama kwa lengo la kujenga. Kwa maana rengo wa kati(socio0 democrats) kwa hiyo ni muanganiko watu wenye tofauti ndogo juu ya namna ya kuongoza nchi wakati CCM ni chama chenye mguso wa ukumunisti wa kale wenye mtazamo kuwa ni mkusanyiko wa watu waliowa sawa kimtazamo na fikra katika namna ya kuongoza nchi.

asante kwakutupa elimu
 
"all this after being born in the royal family, the house of Mbowe" Will some one in the know please elaborate for me? Was Aikaeli Mbowe the mangi of machame at some point?

No he most certainly was not...Abdiel Shangali my great Uncle was the chief duiring Mbowe's life. He was the paramount chief of Machame.. other chiefs at the time were Mangi Gedion of Kibon'goto.. Mangi John etc.. Freeman sio Royalty as far as i know.
 
No he most certainly was not...Abdiel Shangali my great Uncle was the chief duiring Mbowe's life. He was the paramount chief of Machame.. other chiefs at the time were Mangi Gedion of Kibon'goto.. Mangi John etc.. Freeman sio Royalty as far as i know.

Kwani Freeman ni mchaga?
 
Guys, this is real, hate him or love him.. CHADEMA imekuwa successful saana under Mbowe leadership kuliko Mwenyekiti mwingine yeyote. Awe ameenda shule au hajaenda, Mungu amempa kila mtu charisma yake, this guy has taken this party somewhere ...besides mbona Bill Gates hana hata college degree zaidi ya degree ya heshima aliyopewa mwaka huu
 
cv ya kitaaluma:
Aliapata elimu yake ya msingi
Alihitimu kidato cha sita (tusiulizane division aliyopata)
Aliendelea kusoma elimu ya juu ng'ambo ... Uingereza, kahitimu au hajahitimu...tutaelezwa 2010
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom