Ombwe la tasnia ya mawasiliano limetengenezwa wa miaka mingi na linaipa shida serikali kwa wakati huu.

Steven Joel Ntamusano

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
2,948
1,988
Tasnia mbili bado zipo nyuma na madhara ya hatua za taratibu za kusogea kwa maendeleo ya tasnia hizo yanaonekana dhahiri kabisa.

Tasnia ya polisi na tasnia ya bahari. Polisi wetu mpaka kesho wanafanya makosa mengi yanayodhihirisha kuwa namna wanavyoingia vyuoni kuna wepesi ambao unaiumiza serikali unapofika wakati wa kuhitimu mafunzo.

Polisi wengi wale wanaopata ufaulu mbovu sana kwenye mitihani ya kidato cha nne, kwenda upolisi kumeendelea kuwa ni kimbilio la wale wanafunzi waliofeli masomo magumu.

Hivyo hata wanapohitimu mafunzo yao na kuingia mitaan wanawakilisha akili zile zile za mwanafunzi anayeshika nafasi ya mwisho katika mitihani yake ya shuleni. Huu ni ufa mbaya sana na ni kama vile tumeamua kutotafuta suluhisho la kupata mapolisi imara wenye kuja kufanya maamuzi sawa na watu wenye upeo mkubwa.

Wale failures wetu maishani ndio wanapelekwa wakasomee upolisi halafu tunategemea kuwa na askari mwenye weledi wa kawaida tu!.

Tasnia ya habari ni pana kuliko ile ya upolisi. Huku ndio ule mwenendo mzima wa kijamii unapotengenezwa mara kwa mara [narrative]. Huku wameachiwa wale wanaopata ufaulu hafifu kwenye mitihani ya kitaifa ndio wawe wanaoipa jamii ule mwelekeo wa kimawazo.

Hili ni tatizo linaloitesa serikali kwa awamu kadhaa sasa. Tuna udhaifu mkubwa katika suala zima la nchi kuwa na Public Relation Managers wenye uwezo na wenye kuendana na kasi ya mabadiliko ya kidunia.

Maafisa habari tulionao wanafanya kazi kwa mazoea na wanakosa uelewa wa fani wanayoitolea ufafanuzi mbele ya waandishi wenzao wa habari. Jamii inakuwa na uelewa mdogo kwa sababu wenye wajibu wa kuelezea masuala nyeti ya kiserikali hawana uwezo wenye kulingana na ushindani wa kidunia tuliomo.

Wakenya wanatuacha mbali kila kukicha. Niliutazama ule mkutano wa kimataifa uliofanyika hivi majuzi hapa Dar, yule MC ni Mkenya na akatupiga madongo kwamba tuna tatizo la kuijua lugha ya kingereza, naamini ujumbe ni mpana zaidi ya kuwa na uelewa na ujuzi wa kingereza.

Tatizo lipo kwenye kuwa na watu sahihi wenye kuweza kutafsiri kile kinachofanywa na taasisi au wizara zetu mpaka kikaeleweka mbele ya jamii.

Leo hii huko mipakani petroli lita moja inauzwa mpaka shilingi elfu nane, watu hawaelewi nini kinachoendelea na mawaziri wametulia tu Dodoma bila ya kufahamu namna sintofahamu inavyotapakaa kila mahali. Huu ulikuwa ni muda wa mtu wa mawasiliano wa wizara ya nishati kuelezea kwa kina nini kinachoendelea na utatuzi wake utapatikana kwa njia zipi.

Kuna sintofahamu ya Ngorongoro na yenyewe haina mtaalam wa mawasiliano mwenye kuitolea ufafanuzi ili jamii iweze kutulizwa na kufahamishwa nini haswa kinachoendelea. Kila mtu anakuja na tafsiri yake kulingana na anachotumiwa kwenye simu yake ya mkononi!.

Kuna suala lenye kuhitaji sana ufafanuzi la uendeshaji wa bandari zetu, halipewi kipaumbele na kila mtu anakuja na maoni kulingana na uelewa wake juu ya nini kinachoendelea.

Huu ulikuwa ni muda wa mkurugenzi wa mawasiliano wa TPA kuja na habari ya kina kwamba DP World alipatikana kwa njia single source Procurement kwa sababu ya umiliki wa madini yaliyo kule DRC na Rwanda.
Angeeleza kwamba hawa waendeshaji wanaotafutwa muda huu inatumika njia nyingine ya procurement kuwapata, jamii ingeweza kutulia baada ya ufafanuzi wa kina kuwekwa wazi.

Awamu ya kwanza Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuifanya hii kazi ya ukurugenzi wa mawasiliano yeye mwenyewe akiwa kiongozi mkuu wa Taifa, kiasi ambacho hakuna aliyeona kuwa tunatengeneza ombwe kwa kuwa na wahitimu wenye ufaulu hafifu sana wa tasnia nzima ya habari.

Na tuanze kuamka, tukifahamu kwamba tuna ombwe la tasnia ya habari lililotengenezwa kidogo kidogo mpaka sasa limekuwa kubwa sana, haishangazi kuona mastaa wa miaka ya sasa wakiakisi jamii nyepesi sana tuliyonayo. Huwezi kuvishangaa vituko vya mcheza sinema au mwanamuziki aliyekulia kwenye jamii yenye wapasha habari wenye viwango duni vya elimu.
Hili ni ombwe limetengenezwa kupitia mfumo wetu wa elimu.
 
Back
Top Bottom