Ombi: Serikali ya Tanzania ipeleke agenda African Union (AU) ya kuwakatia eneo la makazi waafrika waliochukuliwa utumwani ili warejee nyumbani

Eti Eminem hua anasema anaamini yeye ni mwafrica huku Pdiddy akisema anaamini yeye asili yake ni Ethiopia/Somalia.

Maanina hawa jamaa wanacheza waje huku wajionee mziki mnene eti huko US mtu mmoja tu anauwawa then wanaandamana mpk police wanapiga magoti kuomba msamaha aje ajionee huku kwa afande Mroto mtu anapigwa anakufa na nyie mliobaki mnaambiwa mtapewa kichapo cha mbwa mwizi na maisha yanaendelea poa kabisa.
Africa polisi akiuwa anapandishwa cheo au anahamishwa kituo,Hakimu akimfunga mpinzani anapata ujaji, Kenya polisi wameuwa jumla ya watu 15 Hadi Sasa kisa lockdown,wao mtu mmoja tu wanaandamana wote.
 
Ni heri wabakie kwenye ubaguzi kuliko waje Africa wakutane na mziki wa wasiojulikana,umbishie polisi ukipona pona ukionewa huruma utakuwa ICU,ufunue mdomo upigwe uhujumu 10 yrs ndani ushahidi haujakamilika,au ukalete cheti cha Bibi yake babu.Au udai Kodi ya miaka 20 nyuma.Huku ushenzini watuachie sie uncivilized
 
Huo umoja wa Africa unaoutaka ufanye maazimio hayo hawana tofauti na bunge la dugai Kama waliweza kukaa kimya Gadaffi akiuliwa Hali wangeazimia asingeuwawa.
 
Hatuwahitaji wabaki hukohuko, pamoja na kuwa wanabaguliwa wale black American huwajui walivyo dharau na ngebe!

Je unafikir pia huku ni salama, ni wangapi wameuliwa na Polisi hapa Tizii au sababu ni black ameua black mwenzake?

Pia hao black Americans wanauana sana wenyewe kwa wenyewe kuliko hao wachache wanaouliwa na Polisi!
 
Watarudije Africa na wakati wakija huku watahitajika vibali!serikali za Africa zingeweka utaratibu Wa kiwaruhusu kuja kuishi freee yaani ka anahitajika kufanya Tanzania kuwa kwake anakaribishwa,na Kenya nao wafanye hivyo ,mean nchi zote za Africa zifanye hivyo kwao
 
... subutu! Black Americans wanaishobokea Marekani kuliko wazungu wenyewe! Bongo yenyewe na duniani kote watu wako tayari kujilipua ili wakaishi Marekani sijui unaleta stori gani mleta mada!
 
Mm nadhani nadhalia yako haina matiki kwa maana huwezi kuwaambia wamarekani weusi watoke mfano Canada waje shithole country kama Tizii,kwa kigezo kuwa kuwa huku hawatobaguliwa lakn umesahau sisi huku tunaishi kawa wasaidizi wa watawala kwamaana wao kila siku wanatunga sheria za kuwafanya miungu mtu huku sisi tukiachiwa kwenye sheria Kali za kufungwa pale wanapo hitaji bila kuulizwa na yeyote..watz wengi tunaishi kwa shida naanyanyaso kuliko mweusi aliyeko marekani.
 
Kuna gereza kijiji kule linaitwa Angola,humo wamo wengi mno Waafrika hawa black American,wanalima,wana tv yao kila kitu unachopata mtaani unapata humo,hamna fence ila hata ukitoroka utaenda wapi?unarudi mwenyewe.
google
 
Warudi kufanya nn..maisha popote tu..kuna hao wachache wanaoteseka lkn kuna maelfu waliofanikiwa sana....maelfu....mpaka mtu kama Oboma kawa Rais wa Taifa kubwa duniani.

Wakae huko wafanyekazi...watume hela kuwekeza Africa..kuliko kuja huku kurundikana tu
 
Wakija huku wenyewe ndio watageuka wabaguzi dhidi yetu wabaki tu hukohuko wajikomboe hukohuko
 
Sawa ila wapunguze madharau.wengi wao wanasema wao na sisi ni tofauti.Wao ni hebrew sisi ni hamites na tuliwauza Utumwani hivo wana kisirani na sisi.
 
Wakija huku wenyewe ndio watageuka wabaguzi dhidi yetu wabaki tu hukohuko wajikomboe hukohuko
Kuna ukweli hapo.dawa wasiwe wengi sana kwenye nchi moja ya kiafrika.watawanye kila nchi iwe na wachache wachache.Ni Ndugu zetu ila ni wakorofi sana na madharau sana.hasa wakutoka Marekani
 
Umoja wa Africa hawana tofauti na bunge la ccm.Sijui ni umoja wa nn Sasa Hali unashindwa kutatua shida za waafrika, kuzuia udikteta, wakimbizi,nk.Gadafi anauwawa mchana tena live wao wanachungulia madirishani bila msaada.
 
Back
Top Bottom