Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,494
- 113,590
Wanabodi,
Hili ni ombi maalum kwa watu maalum, hivyo hii thread sio thread ya watu wote bali ni thread maalum kwa watu maalum na lengo maalum la
kutuma ujumbe maalum kabisa kwa watu maalum kabisa.
Tanzania sio nchi ya watu fulani tuu au chama fulani tuu, Tanzania ni nchi ya Watanzania wote, wa vyama vyote, wa dini zote, wa makabila yote, wa jamii zote, wa jinsia zote, wa rangi zote, wa hali zote za maisha, matajiri na masikini na Watanzania wa circumstances zote.
Mimi nikiwa mwandishi wa habari, nimeshuhudia chaguzi zetu zote za vyama vingi, zimekuwa zikiendeshwa kwa mtindo wa "Mutatis Mutandis"
Hivyo sasa tunapokwenda kwenye uchaguzi, naomba kutoa ombi maalum na angalizo muhimu kwa wahusika wakuu wa uchanguzi huu wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, uendeshwe kwa kutumia kanuni ya Kilatini ya "ceteris paribus" na sio kutumia zile kanuni zetu za kawaida za "Mutatis Mutandis"!.
Nimesikia sauti, "voices from within" kuwa tukiendelea kufanya chaguzi zetu kwa Mutatis Mutandis, kuna janga fulani litatokea.
Wahusika wakuu wa uchanguzi huu, wakikubali uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2019 na uchaguzi Mkuu ujao wa 2020, kuendeshea kwa ceteris paribus , taifa Letu litabarikiwa, na viongozi wetu wabarikiwa, na sisi wananchi wa kawaida pia, tutabarikiwa na kupata neena na mafanikio makubwa, na nchi yetu kupata ustawi mkubwa wa kisiasa, kiuchumi na kijamii, lakini tukiendelea kutumia ule mtindo wetu wa mutatis mutandis, taifa tutalaaniwa na viongozi wetu watalaaniwa na kuadhibiwa!, and you never know ni adhabu gani viongozi wetu wakuu wataadhibiwa!.
Mungu Mbariki Rais Magufuli, na watendaji wake wapate uwezo, watumie "Ceteris Peribus" kwa vyama vyote na sio kuendeleza "Mutatis Mutandis"
Mungu ibariki Tanzania.
NB. Sijaweka ufafanuzi wa maneno "Ceteris Peribus" na "Mutatis Mutandis" sio kwa bahati mbaya, nimefanya hivi kwa makusudi Maxima, kwa sababu ujumbe huu ni ujumbe maalum na mahsus kwa watu maalum na mahsus ambao mimi nawajua huwa wanatembelea sana jf, kwa vile watu hao, wanayajua maneno hayo. Wengine wasio husika hayawahusu, hivyo sikufafanua ili ujumbe huu uwafikie walengwa tuu.
Hata Mungu alipotaka kumfikishia ujumbe maalum mfalme Belshaza, alimtumia kiganja cha mkono kikaandika kwenye ukuta wake, "Mene Mene Tekeli na Peresi", tukiendelea kufanya chaguzi zetu kwa Mutatis Mutandis badala ya kutumia
Ceteris Paribus, then kuna siku Mene Mene Takeli na Peresi itakuja kuishukia Tanzania na kumshukia kiongozi wetu!.
Nawatakia Weekend Njema,
Paskali.