bornagain
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 3,383
- 1,354
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIMkuu tupe walau wasifu wake kidogo, alikua anafanya wapi amewahi kushika nyadhifa gani, elimu yake n.k. SIDO ni shirika muhimu sana kwa uchumi wa Tanzania lakini limeshindwa kufanya majukumu yake kama matakwa sheria ya kuanzisha shirika yalivyoanisha. So tungependa kufahamu umakini wa mdau aliyepewa shirika hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Eng. Omari Jumanne Bakari kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO).
Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo umeanza Desemba 04, mwaka huu, 2013. Eng.
Omari Jumanne Bakari ni Mtafiti Mwandamizi katika Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dar es Salaam.
Eng. Omari Jumanne Bakari ni Mtanzania mwenye elimu, weledi na uzoefu ambao umemfanya Mheshimiwa Rais aamini kuwa atakapoongoza SIDO, atasaidia kukidhi matarajio ya taifa kwa kueneza ujasiriamali, uwekezaji,uzalishaji na kutoa nafasi za ajira katika ngazi ya viwanda vidogo na vya kati kama msingi imara wa uchumi wa Tanzania, ikiwemo kwa kuingiza sayansi, teknolojia na ubunifu katika viwanda vidogo vidogo.
Mwisho
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.
16 Desemba, 2013