Omari Nundu: Stand up and be counted!

George Smiley

JF-Expert Member
Oct 24, 2011
471
266
I've had enough na kutazamana machoni

Yes ni mchapakazi and all lakini as time goes by I'm getting tired of this guy.

Whats so difficult kuwajibisha lile jeshi la wazugaji lilojazana pale Airport Dar?

DEPARTURES:

Vinyesi vinavyonuka nje ya airport, na vyoo vilivyokuwa blocked

1.Airport haina proper lighting

2 Aiport haina ventilation

3. Wafanya kazi wananuka vikwapa

4. Escalators zisizofanya kazi

5. Usumbufu wa toka kwa immigration pale juu ambako kuna maofisa 11 kwenye ku can mizigo na kuchekiwa tena passport

6.Wireless internet isiyofanya kazi

7.Duty Free Shops ambazo ni sub standard

ARRIVALS:

1. Foleni ya wanaojaza visa forms (kwa nini msiwape watu wa mashirika ya ndege zikajazwa kabla ndege haijaland)?

2. Poor Ventilation (air condition zisizofanya kazi)

3. Conveyor belts zisizofanya kazi na kama zikifanya kazi ziko slow

4. Customs officials ambao wako bize kupekua mabegi ya abiria ambao hawana cha ku declare

5. Customs officials ambao hawataki kutumia scanners za mabegi na masanduku ya abiria yanapotolewa kwenye ndege

7. Jeshi la wapuuzi pale mlangoni kabla hujatoka wanaojifanya USALAMA WA TAIFA/IMMIGRATION/ANTI DRUGS/PCCB/ ambao kazi wanayofanya pale ni kuwasumbua na kuwauliza maswali abiria na kutazama passports zao bila sababu za msingi

Considering Dar Airport ni funguo kwa mgeni anayekuja Tanzania ni vyema tukahudumiwa kama customers na sio wanyama ndio maana tunalipa airport Tax na mengineyo.

I think its about time hawa wapuuzi wa TAA hapa chini wawajibishwe:




Management Team

S/NNamePosition
1 Engineer S.S. Suleiman Acting Director General
2Mr. L.K.M. MwiguneDirector of Human Resources and Administrator
3Mr. Thomas HauleActing Director of Regional Airports
4Mr. Mosses S. MalakiDirector of Julius Nyerere International Airpiort
5Engineer White R. MajulaActing Director of Engineering and Technical Services
6Mr. Daniel E. C. D. MsuyaChief Internal Auditor
7Mr. Mtengela HangaHead of Procurement Management Unit.
8Mr. Raphael W. BokangoAdvisor of Director General
9Mr. Ramadhan A. MaletaLegal Secretary
10Mr. Mshamu NjimbwiChief Fire Officer
11Mohamed MillangaChief Compliance Officer





Managerial Advisory Board (MAB)

S/NNamePosition
1 Engineer Lambart Ndiwaita Chairman
2Madam Jane LymoMember
3Mr. Mumtazhusein Roshan AlooMember
4Prof. Lucian A. MsambichakaMember
5Dr. Mohamed S. MhitaMember
6Capt. Kenan MakindaMember
7Engineer Edwino T. H. MujwahuziMember


Managerial Advisory Board (MAB)


N
undu nakushauri uende Nairobi ukatazame wenzako wanavyofanyakazi pale JKIA na below ndio mipango yao ya kuitanua

jkiaexpansion4cjim6.jpg


3360435366_9cddb98791_b.jpg
 
  • Thanks
Reactions: JS
Duh hiyo namba 3 kwenye departure!!

Kuna kazi ya kuagiza na deodorants pia


Mimi kinachoniudhi zaidi ni kulazimisha watu kufanyiwa check-in baada ya kuingia ndani bila ya kuwawekea walau mizani ya kupima mizigo yao
 
Nchi imelogwa hii!
Hata personal hygiene inabidi mkurugenzi aingilie kati!
Hilo la ventilation ni la muda mrefu!
Usisahau mende,usiombe uwe na delay ya usiku! Inabidi ujichunge manake hukawii saa unashuka mende anafanya ziara begani ama anatokea kwenye handbag!
Flamingo restaurant ni chafu ajabu! Sakafu, kuta, mende,it is simply disgusting!
Kule terminal 1 kuna ile mama ntilie,wakati unatoka kushoto hapo aibu tupu! Wanauza soda na maandazi!
 
7. Jeshi la wapuuzi pale mlangoni kabla hujatoka wanaojifanya USALAMA WA TAIFA/IMMIGRATION/ANTI DRUGS/PCCB/ ambao kazi wanayofanya pale ni kuwasumbua na kuwauliza maswali abiria na kutazama passports zao bila sababu za msingi

Hawa wapuuzi huwa wananikera yaani hakuna intelligence yeyote wanafanya zaidi zaidi wamekaa kirushwa rushwa tu!!!!!
 
interesting piece, kama tunashindwa hivi vidogo, je maendeleo kwa ujumla yaani miundo mbinu ya kutosha, kazi kwa vijana, mazingira huru ya ushindani kibiashara, elimu nzuri, huduma za afya, maji safi, uzuiaji wa mifumoko ya bei, na mazuri mengine si yanaonekana kama fizikia ya unajimu
 
Mie sijui kwanini hatuna management zenye watu wachapakazi na wabunifu kama Nehemia Mchechu wa NHC! Wengi wa CEO wetu ni "business as usual!" Tatizo ni kubebana kwenye hizo posts. Lazima tubadilike sana
 
Mie sijui kwanini hatuna management zenye watu wachapakazi na wabunifu kama Nehemia Mchechu wa NHC! Wengi wa CEO wetu ni "business as usual!" Tatizo ni kubebana kwenye hizo posts. Lazima tubadilike sana

Nehemia Mchechu kweli anafanya kazi ni kwa kipindi kifupi tu toka ameteuliwa. hivi haiwezekani akapewa na jukumu la ku-handle airport??awe kama ana-oversee na kutoa maelekezo/ushauri tu???
 
......Ndugu zangu Hapa hakuna cha NUNDU wala Mkia tatizo Sekali haina uwajibikaji kuanzia juu watu hawafanyikazi NIkucheka cheka tu
nanii umesikia anawajibisha mwingine? labda magufuli .....na hata huko rais na hata pinda wana mwonea wivu TZ
imeoza sehem kibao ..Pale mtu anachukua passport yako anakuuliza huwaunasafiri sana wewe ....eti vipi...kwanini begi lako zito? ni upuuzi mkubwa sana basi tu wa TZ tuna mengi ya kubadilisha sana LAKINI SAA IPO YAJA ..................
 
Nehemia Mchechu kweli anafanya kazi ni kwa kipindi kifupi tu toka ameteuliwa. hivi haiwezekani akapewa na jukumu la ku-handle airport??awe kama ana-oversee na kutoa maelekezo/ushauri tu???

Kweli tatizo ni kubebana kusiko na msingi!!Katika hiyo Management Team nashangaa kumuona Mr Haule(3)kwamba naye yuko wakati kakiwanja kadodgo kama Arusha aiport/airstrip palimshinda!!jamaa alikula hela za kutosha,malalamiko yalipozidi,kumbe wakaenda kumpa ulaji zaidi!!OMG
 
Ukisoma cv zao na ukaambiwa idadi ya viwanja vya ndege wametembelea duniani kuona wenzao wanavyofanya kazi unabakia unajiuliza Tanzania tulirogwa na nani!!! Jibu ni moja tu, teua DG mpya mchapakazi. Timua hawa jamaa. Hawana ubunifu wowote wa kuondoka hapo walipokwama. Wakiulizwa kisingizio itakua ni pesa ya kutosha kuendesha viwanja.
 
imekuwaje tena?

mmeanza kugeukana wenyewe kwa wenyewe?

au ule msemo wa protecting our own mmeamua kuutupa nje ya dirisha?
 
Kweli tupu Airport yetu inakera na huduma ni mbovu.

Nundu wacha mambo ya kitanga yakhe, majukumu hayo.
 
Avatar, umenena vema. Huyu Nundu aachane na kuhangaika kutafuta jinsi ya kujenga Miundombinu ya Uchukuzi aanze rasmi kazi ya kuwaogesha hao wanaonuka vikwapa na wasiopiga miswaki hapo kiwanjani Dar es Salaam. Ninakubaliana nawe asilimia mia kuwa hiyo ndio kazi ya Waziri wa JamiiForum.
 
Ninawashukuru nyote kwa michango yenu, vyovyote iwavyo - yenye chuki, yenye upendo, yenye kupeana nguvu na matumaini na hata ile inayolenga kunivunja nguvu na kunikatisha tamaa, yote ninaipokea na kuwashukura.

Bila Shaka nimewafungulia uwanja.

Omari Rashid Nundu
 
Ninawashukuru nyote kwa michango yenu, vyovyote iwavyo - yenye chuki, yenye upendo, yenye kupeana nguvu na matumaini na hata ile inayolenga kunivunja nguvu na kunikatisha tamaa, yote ninaipokea na kuwashukura. Bila Shaka nimewafungulia uwanja. Omari Rashid Nundu
Mheshimiwa hapa hakuna aliye na wivi au chuki lakini mpaka watu wanaingia humu ujue kuwa watu wako desperate kwani hakuna nayesikiliza kilio chao

Tunajua kuwa pesa au bajeti yenu ni ndogo na binafsi nimesoma strategic plan yenu yapo iko ambitious lakini la kusikitisha ni kuwa kuna mambo madogo madogo ambayo to be honest ni aibu hata wewe kushughulikia kama hayo ya utendani ya watendaji wako na TAA kwenye main airports zetu

Whats so hard kuwa na proper coordination kati ya Immigration, TRA na wafanyakazi wa airport?

How hard is it ku replace zile escalators au proper ventilation au kuwepo kwa usafi au kuwaambia wale immigration waache ku abuse wageni ambao pia ni wateja wenu?

how hard is it kupata private contractors wakufanya usafi mle?

Yes hatuna pesa ya kufanya makubwa lakini kidogo tulichonacho tukitunze kitutunze

no one is asking for much mheshimiwa
 
Back
Top Bottom