Dkt. Slaa adaiwa kubadilishiwa mashtaka kutoka ya uchochezi na kuwa ya uhaini

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,019
144,377
Ameandika kwenye account yake ya mtandao wa twitter:

Usiku huu, Dkt. Wilbroad Peter Slaa, mashtaka yake yamebadilishwa kutoka katika matumizi ya lugha ya uchochezi sasa amepewa mashtaka ya UHAINI.

Dkt. Wilbroad Slaa yupo kituo cha polisi Oysterbay. Taarifa hii ni kutoka kwa wakili wake, Adv. Dickson Matata. Anakuwa mtu wa tatu.
---

1692158543508.png

Mwanzoni Dr.Slaa amehojiwa kwa kosa la Uchochezi kinyume na kifungu cha 55 (1) (C) (d)( e) cha sheria ya Kanuni ya adhabu (penal Code) Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022Baada ya muda tuhuma zikabadilika na kuwa uhaini.

Dkt. Wilbroad Slaa yupo kituo cha polisi Oysterbay. Taarifa hii ni kutoka kwa wakili wake, Adv. Dickson Matata. Anakuwa mtu wa tatu.

Pia Soma:
- Dkt. Slaa akamatwa na watu waliojitambulisha kama Polisi
 
Ameandika kwenye account yake ya mtandao wa twitter:

Usiku huu, Dkt. Wilbroad Peter Slaa, mashtaka yake yamebadilishwa kutoka katika matumizi ya lugha ya uchochezi sasa amepewa mashtaka ya UHAINI. Dkt. Wilbroad Slaa yupo kituo cha polisi Oysterbay. Taarifa hii ni kutoka kwa wakili wake, Adv. Dickson Matata. Anakuwa mtu wa tatu.
Hii DiPiWeldi imeleta matata sana...

DiPiWeldi imefanikiwa kufunga maridhiano na uvumilivu wa kukosoana kwa hoja....

DiPiWeldi inaweza ikarudisha watu magerezani na mahakamani na wengine wakarudi Ubelgiji...

DiPiWeldi limekuwa jitu kuubwa sana....

Yaani Eti Balozi wa Magufuli anataka kumpindua Makamu wa Rais Magufuli....

Hii nchi tukifanikiwa kwenda mbinguni tutakuwa tunalala stoo baada ya kudeki vyoo vya malaika...
 
Huyu mama kachukia sana. ana dili nyingi na waarabu , sasa hii moja imevuja na watu wameishikia bango, ile ya ngorongoro watu walipiga kimnya.

Pia kapoteza mvuto kwa kasi ya 5G.. Hapo anafikiri dili zilizobaki na waarabu zitakuweje? Mwisho wa siku anatoa maamuzi mabovu sababu ya Hasila zake...SIKU YA KUFA NYANI ....
 
Mungu akitaka kukuangusha, sometimes hukunyima maarifa.
Mfalme Nebkadneza aliambiwa na Danieli aache matendo yake dhidi ya Wana wa Israeli la sivyo Atabadilika kuwa Hayawani.

Nebkadneza alikuwa na jeshi zuri lenye nguvu likiongozwa na Jemedali Mwanaye anaitwa Neboporasa.

Baadae pamoja na jopo lake la waganga, wasihiri na wenye hekima ufalme ukaanguka, mfalme akajikuta yuko nyikani anakula nyasi kama wanyama wa mwituni.

Hapa ardhi ya Nyerere kuna mtu aliambiwa atubu akawa amedharau pia.
 
Huyu mama kachukia sana. ana dili za wizi nyingi na waarabu , sasa hii moja imevuja na watu wameishikia bango, ile ya ngorongoro watu walipiga kimnya...pia kapoteza mvuto kwa kasi ya 5G.. Hapo anafikiri dili za wizi zilizobaki na waarabu zitakuweje? Mwisho wa siku anatoa maamuzi mabovu sababu ya Hasila zake...SIKU YA KUFA NYANI ....
Kumtuhumu Mtu kuwa ni Mwizi ni lazima utusaidie na Ushahidi wa Wizi wake maana kosa la Wizi ni Jinai. Kumtuhumu Uongo Rais wa nchi ni Kujidhalilisha Mwenyewe kwenye uso wa Dunia.

Wanasiasa badala ya kutumia Nafasi Vizuri kuviuza vyama vyenu mnaanza kutukana na Kutishia Viongozi sidhani kama ndilo lengo la Demokrasia eti kudhalilishana badala ya kuuza Sera zako.
 
Andiko lako hili limenifanya niwe na wazo kichwani mwangu.

Huyu mwanamke anaweza kuwa kishajiandalia sehemu ya kukimbilia mambo yatakapomzidi kimo.
Sioni huyu akiendelea kuishi humu humu nchini kwa jinsi hali inavyoendelea kujipambanua.

Huyu atakuwa ni Idd Amin wa pili toka ukanda huu kukimbilia uarabuni kwenda kumaliza maisha yake huko.
Natamani mngekuwa na akili kidogo, lakini ndo hivyo kwakuwa mmeamua kutokuwa nazo basi sina namna!!
 
Kumtuhumu Mtu kuwa ni Mwizi ni lazima utusaidie na Ushahidi wa Wizi wake maana kosa la Wizi ni Jinai. Kumtuhumu Uongo Rais wa nchi ni Kujidhalilisha Mwenyewe kwenye uso wa Dunia...
Umeongea ukweli wasiotaka kuupokea. Watu wamepewa uhuru; wamepinga, wanazunguka kila pembe na nakala zao za mikataba kupita 'kuwatafsiria' wanavyojua wao hao wananchi, wameenda mahakamani kufungua kesi iliyopokelewa na kusikilizwa na kutolewa maamuzi. Bado hawaridhiki wanaendeleza vitendo visivyo vya kinidhamu maana yake nini?!!!!
 
Back
Top Bottom