Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 58
Yaani Kama mchezo wa kuigiza vile!
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Imefikia wakati sasa wananchi wa Tanzania ambao wamekuajiri kuwa rais wao wapewe heshima na usikivu wanaostahili. Mambo mnayoyafanya kwa sasa dhidi ya watu wa taifa hili yanapita kipimo cha kawaida cha uvumilivu.
Kuna habari kuwa serikali yako ina mpango wa kubadili baadhi ya mambo katika report ya ukaguzi ya BOT. Kuna report kuwa wewe na serikali yako ya sasa mna mpango wa kujitoa kabisa kwenye kashfa hii ambayo wewe binafsi na rafiki yako mwizi na mkoloni Rostam Azizi mnahusika moja kwa moja na kumtwisha lawama zote Dr Balali.
Napenda kukukumbusha kuwa report ya awali iliyotolewa na hao wachovu wa E&Y tayari ipo katika safe za Jambo forums. Ingawa report yenyewe imejaa usanii na lugha za kilaghai za kisheria, watanzania wana kila sababu ya kusoma hii report katika hali yake ya mwanzo (original content) ili waone usanii uliofanywa na Massawe na wenzake.
Juhudi zako za kutaka kubadili hii report ili wewe na mafisadi wako msionekane kuhusika ni mchezo wa kuigiza ambao utakutia hatiani. Kujifanya kuwa huna taarifa za kujiuzulu kwa Gavana wa benki wakati report zote za ikulu zinaonyesha kuwa wewe, Meghji, na yule msaliti - yuda iskarioti - Saliva Rweyemamu mnazo hizi habari kwa muda sasa ni mchezo wa kitoto.
Tafadhari prezid Kikwete. Ulilikoroga ulipokubali pesa za kodi ya Watanzania kuchukuliwa BOT ili wewe ushinde urais kwa kishindo na kudidimiza kabisa upinzani bungeni. Ulilikoroga ulipokubali pesa chafu toka kwa Rostam Aziz na biashara zake chafu na wairani. Ulilikoroga ulipokubali pesa toka kwa tapeli la kimataifa Sinclair na wenzake. Wakati umefika wa wewe kunywa ulichokoroga mwenyewe.
Ole wako ukileta usanii kwenye hii report, inawezekana vijana wako wanaokesha hapa na kujaribu kujua nani ni nani hapa hawana taarifa ya kinachokuja mwaka 2008. Watanzania wenye uchungu na nchi yao bila kujali walipo wamepania kuchukua nchi yao toka mikononi mwa mafisadi unaowalinda kwa nguvu ya dola.
Najua kuwa wasaidizi wako na wewe mwenyewe mtapretend kuwa hii email ninayoituma kwako na kwenye website yako na kisha kuwekwa kwenye forum tukufu ya JF kuwa hamjaiona. Hata hivyo ni vyema umejua ukweli ili usijelalama kuwa hukupewa onyo.
Asante