Ole wako Kikwete ukileta usanii report ya BOT

nyie humu ndani bado mnatuletea upuuzi hivi rais aliyechaguliwa na wananchi mnataka tusimpe vitisho kwanini? naomba muwe werevu rais anakoromewa na raia bila kujali hali yake rais ni nani kwa raia wewe?

kikwete anawajibika kwa upumbavu wote unaofanyika bila kujali ujinga wake ni gharama kwa damu ya watu, nani hajui Bhutto amekufa na watu wengi sana?

nani hajui kilichowaua ni demokrasia nani hajui gharama ya demokrasia ni ghali sana hata damu ya watu ? mnataka nini tufikie huko kwa uzembe wa kughushi report? anayeogopa kumshinikiza rais awe kimya na atuache sisi tunaojua kila madhara ya kuchezea amani ikipotea kikwete marekani wewe unayeleta mzaha utakuwa wapi sio maiti mimi na wewe?

rais si zaidi ya wananchi uwezo wa kumtisha tunao au unafikiria jeshi linamtii bila kura zetu?

acheni ujinga na mzaha unamuogopa kikwete kwa lipi wakati sisi tunampigia simu na kumtumia email bila kujificha? mbona anakubaliana nasi.

Duu Mshamba wa kijijini ungepunguza ukali wa maneno yako hayo (in bold) post yako ingekuwa nzuri zaidi.
 
unajua kuweka presha kwa serikali ni muhimu sana, lakini si kwa staili ya baadhi yetu. kuna kitu kinaitwa nia njema, mathalani mojawapo ya nia njema ni "KUMWAMBIA RAISI UKWELI ILI AFANYE KAZI YAKE BARABARA". lakini pamoja na nia njema ya kumwambia raisi ukweli bado utakuwa hujafikia lengo husika iwapo unamuambia ukweli huo kwa lugha ya kejeli, matusi na dharau.kuna kitu kinaitwa protocal unapomuadress mtu kama mheshimiwa raisi.

mathalani unaweza kumuita raisi kwa jina lake kabisa mathalani hivi:Kikwete eeh, hongera sana kwa kushughulikia suala kadha wa kadha. kwa kauli kama hiyo hakuna kosa lolote lakini kwa mtu muungwana ataanza hivi, mh raisi(Kikwete) hongera sana kwa kushughulikia suala kadha wa kadha, hii ndiyo protokali.

kumuandikia e-mail raisi na kumuambia eti amemkumbatia "MKOLONI NA MWIZI ROSTAM AZIZI". Iko wapi heshima kwa watanzania wenzako kuheshimu utaifa wao?. chini ya kauli hii umejificha ubaguzi wa hali ya juu na ninamuonea huruma sana muandikaji wa barua hii .hata kama Rostam ni mwizi(japo hakuna mahali aliposhtakiwa na kuthibitika mwizi) ukoloni wake ni upi?. hivi kila Mwizi Tanzania ni mkoloni?.

mimi ninavyojua hata yale majambazi sugu yaliyofungwa kifungo cha maisha, ikifanyika sensa nayo yanahesabiwa kuwa miongoni mwa watanzania, sasa iweje umuite mtanzania mwenzako mkoloni?. this is an obvious hatred.

siwezi kushangaa sana na muandika barua ile ya "kumuintimidate the president of the united republic of tanzania) kwa sababu muandikaji mwenyewe anaamini hivi:

"WELL BEHAVED WOMEN NEVER MAKE HISTORY...."

so no wonder kwamba by not behaving she has find the way to make history,

my advice to the writer of this letter to mr. president is, convice him with truth and logic not with emotions mixed with vain imagination.
 
Gamba la nyoka,

Nadhani umesahau kwamba ili mtu au kiongozi yeyote yule aheshimiwe ni lazima kwanza ajishehimu yeye mwenyewe na wale anaowaongoza.Ni kweli JK ni rais wa kuchaguliwa na anayo haki ya kuheshimiwa ILA pale anapoonyesha kutoheshimu na kutokujali vilio vya wananchi wake hapo hapo anageuka kuwa muhuni na mshenzi na hakuna tena sababu ya kuendelea kumheshimu muhuni au mtu mshenzi.
Ni kwanini namweka rais katika kundi la wahuni??
Kwanza:
Tanzania ni nchi ambayo asilimia kubwa ya wananchi wake wanaishi maisha ya taabu sana.Milo miwili kwao ni starehe na bahati kubwa.Wengi wao huishia kula mlo mmoja na pengine wasile kabisa.Na vilevile bila ya kutaja upatikanaji wa huduma muhimu kama afya,maji safi na elimu.Sasa basi kama rais wetu angelikuwa ni mtu anayejali na kusikiliza vilio vya wananchi wake haya mambo yangekuwa yanamuumiza kichwa sana.Na isingelichukua hata punje ya sekunde wananchi kutambua kuwa raisi wao anasikiliza na anapambana kiume kuweka mambo sawa.Mpaka sasa utendaji wake wa kazi unakatisha tamaa kabisa na haiwezi kumchukua mtu kuwa na PHD ili kutambua kwamba nchi haiendi sawa.Chukua mfano,bei ya vitu muhimu imepanda karibu mara mbili tangu achukue nchi,nchi inanuka rushwa,safari za rais nje ya nchi haziishi,nchi kuuzwa kwa wageni kama njugu huku watu wachache kama Rostam Aziz,Karamagi na wengine wakineemeka huku yote haya yakitokea machoni mwa raisi wetu kipenzi! inasikitisha na kukatisha tamaaa.Hata kwa mfano chukulia ile list ya watu wa madawa ya kulevya aliyopewa raisi na wananchi wake imefikiaa wapi? Mimi nimemweka Rais kwenye kundi la wahuni na kwamba asiyejali taabu na shida za wananchi wake.Sasa wewe sijui wewe utampa jina gani au heshima gani..mtu kama huyu!

PILI
Kwa nini anaoushenzi ndani yake??
Kuwaambia wananchi kuwa maisha mazuri yatakuja mwaka 2010 wakati hali wakifa leo hii kwa kukosa huduma muhimu,Kutoshughulikia suala la rushwa ndani ya serikali yake,kufanya usanii katika ripoti ya BOT,kufikiri kuwa suluhu la kuinua uchumi ni safari zisizoisha za marekani na ulaya,dhereu kwa wananchi wake,kupenda kusifiwa bila ya kufanya kazi,kuishi maisha ya anasa kinyume na wimbo wa kuwa nchi yetu ni masikini..huo tayari ni ushenzi mara milioni.
Sasa ndugu yangu huyo tena ni mtu au kiongozi wa kuheshimu??

-Wembe.
 
Gamba la nyoka
Unaongea kama Joseph Warioba vile.

Rais ambaye hawezi kuuhusisha umasikini wa wapiga kura wake, na ufujaji wa rasilimali za nchi, huyo anaweza kabisa kuitwa mhuni, au kwa kimombo non-serious prezidaa.

Am out.
 
Au Rais ambaye anasema hajui chanzo cha umaskini wa nchi anayoingoza huyo umwiteje basi? Tuache heshima za kinafiki na nidhamu ya woga.
 
Kumekucha , kumbukeni marehemu mama Bhutto, alisema kuwa amejiandaa kwa mazuri na hata kwa mabaya pia, hapa mwanamke wa Africa naye kaamua kujitoa na huu ni ushuhuda kuwa hapa kitaeleweka tuu na wajue kwamba ripoti ipo na iko mikononi mwa watanzania wenye uchugu na fedha zao,
 
Komando wewe kazi hii ya Ukomando uliianza lini, Mwafika wa Kike yuko Mchafukoge Mtaa wa Viglasi namna 16. Yupo hapa hapa kijiweni, naendeleza mapambano kutoka ndani.
 
Gamba la nyoka
Unaongea kama Joseph Warioba vile.

Rais ambaye hawezi kuuhusisha umasikini wa wapiga kura wake, na ufujaji wa rasilimali za nchi, huyo anaweza kabisa kuitwa mhuni, au kwa kimombo non-serious prezidaa.

Am out.

Ni dhahiri kwamba tuna tatizo kubwa sana la umasikini, lakini pamoja na tatizo hilo tunalotatizo jingine la namna ya kukabiliana na umasikini huo.

katika njia zetu nyingi tulizojaribu ambazo tumefeli kwa hakika ipo moja ambayo baadhi yetu wanataka tuijaribu, nayo si nyingine bali ni JAZBA.

lakini kwa nature ya jazba kamwe hatuwezi kufika popote, tumefikia hatua sasa tunaanza kutukana kwa kudhani eti sasa ndo watatusikia na watafanyia kazi mawazo yetu, yaani jazba juu ya jazba, tumefikia hatua sasa tunawaita watanzania wenzetu WAKOLONI, yaani jinsi feeling zinavyokutuma ndo unajenga conclusion bila hata kuprove kama uko sawa au siyo!.

member mwenzetu BRAZAMENI amewahi kufungiwa hapa Jf kwa kumuita mtanzania mwenzetu mshindi wa "bigbrother" Richard kwamba yeye ni Chotara wa kijerumani. lakini leo kuna member mwingine anamuita mtanzania mwenzetu bwana Rostam Azizi kuwa ni MKOLONI lakini hajchukuliwa hatua yoyote kwa tusi hilo dhidi ya utaifa wa Mtanzania mwenzetu!.

kuna watu wanamuita Raisi "Mshenzi" lakini kuna watu humuhumu JF wamepata kupewa onyo kali kwa kuwaita wenzao wapumbavu.

well hoja ninayotaka kuijenga hapa ni kwamba kujenga hoja zenye mantiki na za ushawishi kwa ustaarabu pasi ya jazba ,matusi, kejeli, dharau ,vitisho na kiburi ndizo hoja zinazoweza kusimama na kutusaidia watanzania. lakini hoja za kuwatukana watanzania wenzetu(kwamba ni WAKOLONI) na pia kumtukana Raisi wao ili eti kwa kufanya hivyo ndo kuwashawishi kukubaliana na tunayoyafikiri, katu haziwezi kutusaidia.

hoja hujibiwa kwa hoja wasio na hoja huleta vioja ,kejeli,kiburi,vitisho ,dharau na maudhi
 
Bathiii uthilieee eeeh Gamba la Nyoka

Zile sheria za hapa zinakata usimuite member wa humu lugha ya kukera kama mpumbavu au mshenzi lakini hazikatazi kuwaita watu wa nje kwa kuwa hayo si matusi. Lakini kwa ujumla zinakataza matusi hivyo nikiandika ##$%%%! lazima nitafungiwa. Lakini mkoloni ni mtu anayetawala, Rostam Aziz anatawala kupitia vibaraka wake katika BOT, TANESCO, Wizara ya Nishati na madini na kwingineko. Mjinga ni asiyejua, Rais Kikwete ni mtu asiyejua kwa kuwa yote haya yanaendelea yeye hajui anakwenda likizo Mbugani. Pengine hajui kuwa ripoti ya BOT inakabiribia kuchezewa. kama anajua halafu ananyamaza kama ilivyokuwa kwa Richmond basi ni mpumbavu. Kwa ujumla, Mshenzi ni anayefanya mambo yasiyokuwa ya kiungwana, Rostam ni mshenzi ameghushi nyaraka kuwezesha kampuni yake ya Kagoda kuchota BOT mabilioni, na ni ushenzi huo huo ulitumika kwenye kampeni kumchafua Salim Ahmed Salim. Hawa jamaa tumewaambia kwa lugha tamu toka miaka miwili iliyopita walipoingia ikulu lakini hawatusikii. Na tulizoea kuwaambia Rais hakosei ila anashauriwa vibaya. Tumewapa nafasi ya kurekebisha wametupuuza na wametuita wajinga hatujui nini kinachoendelea serikalini. Sasa tunawaeleza kwa lugha kali zaidi. Labda wataelewa kuwa tumeguswa. Lakini wakipuuza na haya maneno yetu, basi ipo siku tutawaeleza kwa vitendo. Wakina mama tukiamua tunaweza, mwafrika wa Kike songa mbele sister. Niko sambamba nawe katika hili

Asha
 
Gamba: hiyo lugha sisi watz ndio waasisi africa: kuita ukweli uongo na uongo ukweli, kumchekea mtu wakati ndani umekasirika, kumsifia mtu wakati unajua amechemsha, kumwambia mtu amependeza sana wakati amevaa gunia; hii ni zaidi inapokuja kwa viongozi. Wakati umefika sasa watanzania kuishinda roho ya unafiki, tuvae ujasiri wa kuwaambia viongozi wetu ukweli. Wanapokosea tuwaambie, wakijamba tusema wamejamba badala ya kusema shetani mbaya amepita au hewa imechafuka!
 
Gamba la Nyoka
Kuna maeneo ambayo jazba ndiyo njia hasa ya kuleta mabadiliko.

Mtu anayedharau busara yako, unadhani anataka nini zaidi?
 
Bathiii uthilieee eeeh Gamba la Nyoka

Zile sheria za hapa zinakata usimuite member wa humu lugha ya kukera kama mpumbavu au mshenzi lakini hazikatazi kuwaita watu wa nje kwa kuwa hayo si matusi. Lakini kwa ujumla zinakataza matusi hivyo nikiandika ##$%%%! lazima nitafungiwa. Lakini mkoloni ni mtu anayetawala, Rostam Aziz anatawala kupitia vibaraka wake katika BOT, TANESCO, Wizara ya Nishati na madini na kwingineko. Mjinga ni asiyejua, Rais Kikwete ni mtu asiyejua kwa kuwa yote haya yanaendelea yeye hajui anakwenda likizo Mbugani. Pengine hajui kuwa ripoti ya BOT inakabiribia kuchezewa. kama anajua halafu ananyamaza kama ilivyokuwa kwa Richmond basi ni mpumbavu. Kwa ujumla, Mshenzi ni anayefanya mambo yasiyokuwa ya kiungwana, Rostam ni mshenzi ameghushi nyaraka kuwezesha kampuni yake ya Kagoda kuchota BOT mabilioni, na ni ushenzi huo huo ulitumika kwenye kampeni kumchafua Salim Ahmed Salim. Hawa jamaa tumewaambia kwa lugha tamu toka miaka miwili iliyopita walipoingia ikulu lakini hawatusikii. Na tulizoea kuwaambia Rais hakosei ila anashauriwa vibaya. Tumewapa nafasi ya kurekebisha wametupuuza na wametuita wajinga hatujui nini kinachoendelea serikalini. Sasa tunawaeleza kwa lugha kali zaidi. Labda wataelewa kuwa tumeguswa. Lakini wakipuuza na haya maneno yetu, basi ipo siku tutawaeleza kwa vitendo. Wakina mama tukiamua tunaweza, mwafrika wa Kike songa mbele sister. Niko sambamba nawe katika hili

Asha

All the best!
 
Na bado anaendelea kuleta usanii hata baada ya miezi sita!

Mwafrika wa Kike unayosema ni sahihi kabisa, katika RAIA MWEMA inaeleza kwamba ripoti inasema wazi kabisa kwamba wahusika wa makampuni 13 waliochukua 90bn/- wamethibitika kufanya jinai na washughulikiwe na ndipo hatua zinazofuata zichukuliwe kama vile kukusanya fedha kutoka kwa wale wengine na hao waliishitakiwa. Jamaa wakaunda task force ya kina Mwanyika ambayo ikajumlisha wote 22 na kuanza "kuwabembeleza" warudishe fedha, badala ya kuwakamata na kuwanyanganya mali na fedha walizonazo. Hapo ni sanaa kwenda mbele. Nadhani kina Mwanyika ndio wako ukingoni. Tuwaone na wao.
 
MNK na wewe Asha mtatumia silaha gani? tuambieni jamani, hawa jamaa wana jeshi sasa ninyi mtatumia siraha gani? ama mmepata ufadhili toka ng'ambo?
 
Baada ya miezi sita itaundwa tume ya kutathimini mapendekezo yaliyotolewa na task force ya kina Mwanyika another 6 months. Baada ya hapo......
 
Back
Top Bottom