Uhamisho hasa Ulilenga Wakurugenzi wenye hati chafu report ya CAG mwaka huu

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,712
6,505
Umofia kwenu wakuu.

Juzi kati kuna uhamisho mkubwa sana umefanyika kwa hasa wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halimashauri na pia kwa wakuu wa Mikoa.

Kama mjuavyo report ya CAG iko ukingoni na inatoa wakati wowote ule mwezi huu, na hizi report sio siri kuna vitu huwa vinajulikana mapema kabisa kabla ya report yenyewe kutoka.

Report inaonyesha kuna upigaji wa kutisha kwenye halimashauri, huko wakurugenzi wanahamisha pesa kwa viroba vya cement,kumbukeni ile sakata la juzi kule wilaya ya Serengeti.

Report ya awali baada ya kufika kwa Mama na kuona kuna madudu, alitaka kuwapiga chini Wakurugenzi wote kabla hata report kamili haijatoka. Ila Wazee wa Busara na wanakamati wa Kamati ya kuombea watuhumiwa msamaha kwa Raisi ndani ya CCM wakiongozwa na Mizengo Pinda wakamshauri Mama asiwafukuze awape second chance kwa sababu watakuwa na msaada mkubwa sana mwaka huu na mwakani, na pia wakashauri awahamishe mapema kabisa kabla report kutoka ili hata ikija swala la uwajibikaji ionekane walisha hamishwa.

Hii idea ikapokelewa ila sasa kutengeneza move ikaonekane wahamishwe na viongozi wengine kama Wakuu wa mikoa na wilaya ili kuondoa uwezekano wa watu kuja kuunganusha nukta.

Unless report ibadilishwe, ila fuatilia report itakayo toka angalia Hamishauri ambazo wakurugenzi wake wamehamishwa juzi utagundua hiki ninacho kisema.

Pia kumbuka report ya mwaka jana ya CAG watuhumiwa wote walisamehewa na sio tu kusamehewa pia waliombwa msamaha kimya kimya mara baada ya kutukanwa Stupidy.Hili la kuombwa msamaha halijawekwa wazi ni la ndani sana ila ukweli ni kwamba waliombwa msamaha na hii ndio sababu moja wapo ya Mama kuamua kuwasamehe kwa sababu aliwatukana siku anapokea report hivyo adhabu ya kuwatukana ikaonekana inatosha kabisa.
 
Mamlaka ya uteuzi inashauriwa kuwateua Wakurugenzi wakitokea Serikali za Mitaa kwa sababu wamekulia humo na sheria, kanuni na taratibu zote wanazijua kuliko kuwateua Makada ambao wakiteuliwa ni wapya na hawajui chochote na hapa ndo upigaji unapoanza.
 
Back
Top Bottom