Kwa niliyoona Mwanza basi ziara ya Makonda ilikuwa usanii uliofeli

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,800
71,220
Maandamano makubwa yaliyo fanyika Jana toka pande tofauti za jiji la Mwanza yamehitimisha dhana kuwa Ziara ya mwenezi wa CCM Makonda kanda ya ziwa iliyokuwa ina tafsiriwa ni kifo cha siasa za upinzani hasa Chadema ni usanii mtupu.

Juhudi kubwa imefanyika hasa na media kudhoofisha maandamano hayo lakini ajabu ni kuwa watu bila kusombwa au kulazimishwa kutoka makazini walifurika kutoa ujumbe kwa serikali ya CCM bila woga.

Tuliwaambia kuwa afanyacho Makonda ni kukusanya watu kuinanga serikali ya chama chake na kuwatukana viongozi wake na baada ya show hiyo watu wanatawanyika huku wakiwaacha wenye fikra za kijinga kuona kawasaidia kumbe kawapotezea muda kwa huo usanii.

Ni wazi kwenye uchaguzi huru na haki na ukilindwa na katiba makini basi saa 4 asubuhi CCM chali kabisa.

20240215_201650.jpg


Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Upo sahihi mkuu ... Tatizo CCM inatem... Bahati mbaya sana kwao... Hawajibga wanapungua siku hadi siku! Ili ku maintain status Quo Kuna siku CCM watamwaga damu!
 
Furahisha ya Mwanza naijua vizuri sana, haona miti mingi hivyo, ni eneo limezungukwa na majumba ya watu baada ya barabara
 
Kumbe makonda kwenye ziara yake naye aliitisha maandamano? Mi nilikuwa sijui!
Btw, chama kizima cha siasa kujilinganisha na mtu mmoja ni kijidharirisha.
Wewe unaona Makonda ni mtu mmoja eeh?.Mtu anayemkoromea waziri, mkurugenzi, mkuu wa wilaya bado unasema ni mtu mmoja? Jitafakari upeo wako.
 
Furahisha ya Mwanza naijua vizuri sana, haona miti mingi hivyo, ni eneo limezungukwa na majumba ya watu baada ya barabara
Chama cha Demokrasia na Matapeli hivi Furahisha kuwa na miti ya acacia kama picha inavyoonesha wanahisi watu ni wajinga kama wao.Kweli hiki Chama kimejaa Manyumbu
 
Back
Top Bottom