Wakurugenzi waanza kupishana kwa wastaafu ikiwa report ya CAG inakaribia kutoka

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,712
6,505
Kwa wazoefu wa mambo ya Audit wanajua fika kwamna hata kabla ya report ya mwisho kutoka kama taasisi yenu ilishindwa kutoa ufafanuzi basi inakula kwenu.Na huhitaji kungoja report ya mwisho kujua kama hillo bali kabka hata ya report lazima mjue hamko salama kwenye ukaguzi wa hesabu.

Hivyo baasi kabla ya report kutoka mwezi ujao au mwezi wa 4 mwanzoni tiyali Wakurugenzi wa Halimashauriza za wilaya na majiji na Manispaa na wakuruguenzi wa Mashirika ya Umma (SU) wameanza kupishana kwa wastafu ili kujihami na pindi tu report inatoka waombewe msamaha kwa Mama.

Kuna mdau wangu anafanya kazi kwa mmoja wa wastafu amenitonya hili kwamba Wakurugenzi wanapishana kwa apppoint ment za kuonana na Mheshimiwa na kubwa ni mambo ya kutaka waombewe msamaha kwa Rais.

Mtakumbuka report ya Mwaka jana watuhumiwa wote yaani asilimia 100 wamesamehewa na pesa hawajarudisha hata kumi na waliombewa msamaha na hawa hawa wastafu.

Pia mtakumbuka adhabu kubwa kabisa walio pewa na Rais ni kuitwa stupiddy. Hio ndoo adhabu kubwa walio pewa na mkuu wa nchi.

Mfumo wa kuombewa msamaha kwa Mkuu wa nchi imekuwepo kitambo sana hasa awamu ya JK na ulikufa awamu ya Magufuri ila kwa sasa umeanza kwa kasi ya kutisha.

Viongozi wastafu walioko mstari wa mbele kuombea watu msamaha kwa Rais ni pamoja na Mizengwe Pinda, Yusufu Makamba, Kikwete na pia Spika wa Bunge wa sasa.
 
Viongozi wastafu walioko mstari wa mbele kuombea watu msamaha kwa Raisi ni pamoja na Mizengwe Pinda, Yusufu Makamba, Kikwete na pia Spika wa Bunge wa sasa.
Hivi Spika wa Bunge wa sasa ni kiongozi Mstaafu? Nilikua sijui sasa mboni bado yupo Bungeni? Km ni kiongozi Mstaafu anafanya nini Bungeni ikiwa tayari ameshastaafu?
 
Back
Top Bottom