Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,599
- Thread starter
- #41
Nakubaliana na wewe kabisa. Jana mimi nikajiuliza hivi TBC kuweka hewani ule ugomvi nia ni ipi hasa:confused3:!!! Hivi ni kweli maadili yanaruhusu mambo yote yawe tu hadharani? Ni swali tu! Tafadhali mtu asini:brick:, hivi vyombo vya habari huwa havipaswi kupembua na kuona umuhimu wa yale wanayoyatangaza? Hapa nia ilikuwa tuone nini? Ubabe ndani ya CCM au? Upuuzi ndani ya CCM?Natamani ningekuwa naweza ku :whip: wote pale! Pamoja na Tido. Tumegeuka yale mabunge ya ngumi mkononi! Itabidi kila aendae kwenye mkutano awe na pepper spray yake just in case mtu anakuletea fujo
Kuna wakati matumizi ya ngumi ni muhimu. Nadhani mambunge ambayo maji yakizidi unga wanatwangana yanaweza kufanya mambo mengi mazuri kuliko mihuri yetu hii tunayoishadadia. Naamini watu kama jirani zetu wa Kenya watafika mbali wakati sisi bado tunajidai kulinda heshima ambazo hatuna. Tukifikia mahali kama hapo pa kutwangana pale watu wazima wanapotaka kuwafanya wenzao nyau nafsi yangu itakuwa na amani sana.