Ole Sendeka acha kuwalaghai wanakimotok na wanasimanjiro, kwa ujumla huu ndiyo ukweli

Olemillya

Member
Aug 31, 2013
49
79
cleardot.gif

UKWELI WA MGOGORO WA MPAKA KATI YA KIJIJI CHA KIMOTOROK NA MKUNGUNERO GAME RESERVES.
[h=2]UTANGULIZI.[/h] Mgogoro uliopo kati ya Kimotorok na Mkungunero Game Reserve ni unyanyasaji wa jamii iishiyo katika kijiji cha Kimotorok iliyoko katika wilaya ya Simanjiro.
Kijiji cha Kimotorok ni moja kati ya vijiji vilivyomo katika wilaya ya simanjiro, Kijiji hiki kwa sasa kipo ndani ya tarafa ya Emboreet kata ya Loiborsiret, ilianzishwa rasmi mwaka wa 1985. Kabla ya kurasmishwa kuwa kijiji ilikuwa ni kitongoji ndani ya kijiji cha Loiborsiret, na jamii iishiyo hapo kwa sasa ilikuwepo zaidi ya miaka 50 iliyopita. Kijiji hiki kinaundwa na vitongonji vitano (5) ambavyo ni Aladalu kilichopo upande wa Kaskazini Mashariki, Oltotoi kilichopo upande wa Mashariki, Arkasupai kilichopo Magharibi, Kisondoko kilichopo upande wa Kusini na Mbugani kilichopo upande wa Kusini Magharibi. Hivyo ukamilifu wa kisheria kwa kijiji hiki kinaundwa na vitongoji tajwa hapo. Na kijiji hiki kipo kwa utaratibu wa kisheria na inatambulika ndani ya serikali na mamlaka zake. Kulingana na utambuzi wake ndani ya gazeti la serikali la mwaka 2000 (Government Gazette 2000).
[h=2]HISTORIA YA MGOGORO [/h] Mkungunero game reserve inasadikika kuanzishwa miaka ya 2006. Hivyo makubaliano ya uanzishwaji wake ulikuwa wa utashi baina ya Wilaya ya Kondoa na utawala wa pori tengefu la Mkungunero. Kutokana na hali hiyo mipaka ya Mkungunero Game Reserve inapaswa kuwepo ndani ya mipaka ya wilaya Kondoa. Pamoja na kutakiwa kuwepo ndani ya wilaya hiyo inashangaza pori hilo kuwepo ndani ya mipaka ya kijiji cha Kimotorok iliyopo wilaya ya simanjiro na mkoa wa Manyara. Wananchi wa kijiji cha Kimotorok kiutawala Mkungunero Game Reserve haipo katika kijiji cha Kimotorok na wala katika Wilaya ya simanjiro iliyopo kwenye Mkoa wa Manyara.
Mamlaka juu ya ardhi ya vijiji kulingana na sheria ya ardhi ya mwaka 1995 na mabadiliko yake ya mwaka 1999 yako kwenye mikono ya wanananchi wa vijiji husika na ridhaa ya matumizi yake hutolewa kupitia mikutano mikuu ya vijiji husika. Hivyo uwepo wa Mkungunero Game Reserve haukufuata utaratibu huo, hivyo basi pori hili tengefu lipo kinyume na sheria hiyo.
Kijiji cha Kimotorok ni kijiji halali na kinachotambulika kisheria kwa mipaka yake na ukubwa wake. Kijiji hiki kina vitongoji vitano (5), hivyo kitendo cha Mkungunero Game Reserve kuimega vitongoji viwili ambavyo ni Arkasupai na Kisondoko kinafanya kijiji cha Kimotorok kupoteza ukamilifu wake unaotambulika kisheria na kiutawala. Kwa sababu hizo ili kijiji cha kimotorok kiweze kukamilika na kutambulika kisheria na kiutawala ni lazima kuwepo na vitongoji hivyo kwani ndivyo vinavyotengeneza muundo wa kijiji cha Kimotorok kama inavyoonyeshwa na Gazeti la serikali la toleo la mwaka 2000 .
Baada ya serikali kuagiza vijiji vyote ambavyo havina usajili kuanza mchakato wa kusajiliwa ,kijiji cha Kimotorok kilipopeleka maombi yake kwa ajili ya usajili, ndipo mgogoro huo ulipoibuka. Hivyo wananchi wa Kimotorok wamekua na wasiwasi na kuamini kuwa nia ya pori tengefu Mkungunero ni kuendelea kumega eneo la kijiji chetu kinyume na utaratibu wa sheria na matakwa ya wananchi.
Pamoja na kutokutambua uwepo wa Mkungunero Game Reserve katika maeneo yote ya kijiji cha Kimotorok, jamii husika hainufaiki na shughuli na uwepo wa Mkungunero, badala yake uwepo wake umeleta umaskini na adha kwa jamii husika kwani katika eneo lilotengwa hawafanyi tena shughuli za kimaendeleo kama vile ufugaji, kilimo na makazi pia.
Pia kumekua na unyanyasaji wa hali ya juu kwa wanajamii wa Kimotorok kutoka kwa walinzi wa pori hilo, kama vile wizi wa fedha, kuchomewa makazi, kuwateka nyara wanajamii na kuwatelekeza kusikojulikana, watu kupigwa na kulishwa magamba ya nyoka na pia kuwatishia wanajamii kwa silaha za moto, wakina mama kubakwa na walinzi wa mkungunero game Reserve, zilizopelekea wakinamama wengine mimba kuharibika. Hivyo eneo lao halali kisheria na kiutawala ni vyema wakapewa haki ya kutumia kwa maendeleo yao pasipo kuingiliwa na mtu wala taasisi yeyote, ili kuwezesha hili kufanikiwa tunaiomba Kambi Rasmi ya Upinzani Bunge iitake serikali na taasisi zinazo husika kuagiza watu hawa wa Mkungunero Game Reserve Pamoja na walinzi wao waondoke mara moja katika maeneo ya wananchi wa kimotorok walilojimilikisha pasipo ridhaa yao.
[h=2]JUHUDI ZILIZOFANYIKA KUTATUA MGOGORO [/h] Juhudi kadhaa zilifanyika ili kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huu, vikao vya ujirani mwema uliyo wahusisha, Uongozi wa kijiji cha Kimotorok , Wilaya ya Simanjiro, wilaya ya kiteto na wilaya ya Kondoa Pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Mkungunero Game Reserves, kikao hichi kilifanyika tarehe 8-9/05/2006 na nyingine ilifanyika tarehe 29/05/2006 vikao vyote hivi viliketi kujadili tatizo la mpaka kati ya Wilaya ya Simanjiro, Kiteto na MGR na hifadhi ya Taifa ya Tarangire,
Vikao hivi viliazimia kuunda kamati ya wataalam kwenda kupitia kumbukumbu zilizo jadili uanzishwaji wa Pori tengefu la Mkungunero na Simanjiro, Kiteto, na Kondoa.
Pamoja na maazimio haya utekelezaji wake umekuwa ukisuasua kitendo ambacho kinawafanya wananchi wa Kimotorok wasiwe na imani na Kamati iliyoundwa.
Kufatia kufanyika kwa vikao hivyo vya ujirani mwema ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Kondoa iliwaandikia Barua wakuu wa Mikoa ya Manyara na Dodoma yenye kumb. Na. C.60/35/110 tarehe 19 juni, 2006 kikiwataka wakuu hawa wa Mikoa ya Dodoma na Manyara kuhitisha kikao kitakacho wahusisha viongozi wa kisiasa na kiutawala wa mikoa hii miwili kwa lengo la kuwaelimisha usahihi wa mipaka yenye mgogoro jambo lenye kutia mashaka kwamba MGR ndo wanapewa jukumu la kugaramikia kikao hicho jambo linalo ashiria kuwepo kwa mianya ya rushwa.
Katika hatua nyingine Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Simanjiro kupitia kwa Katibu tawala wa Wilaya, ilimwandikia Mhifadhi mkuu wa MGR barua yenye kumb. Na.DC/SM/K.20/71/17 kumtaka wasitishe mara moja zoezi la kuwahamisha wananchi wa Kimotorok katika eneo lenye mgogoro, hata hivyo maagizo hayo yalipuuzwa na MGR kwa kuendelea kuchoma maboma ya wananchi na kuwadhalilisha wakina mama na watoto, ikiwa ni pamoja na kufanya uharibifu wa mali za wananchi wa Kimotorok kwa kuzichoma moto, Pamoja na MGR kupuuza maagizo ya Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Simanjiro hakuna hatua zozote zilizo chukuliwa dhidi yao, kitendo kinacho leta hisia tofauti miongoni mwa Wananchi kwa kuhoji kama MGR iko juu ya Sheria?
Vilevile wakuu wa mikoa ya Manyara na Dodoma na kamati ya ulinzi ya mikoa yote miwili Pamoja na wakuu wa Wilaya za Simanjiro, Kondoa na Mbunge wa Simanjiro walifika katika kijiji cha Kimotorok na kufanya mkutano mkubwa wa Hadhara tarehe 02/09/2012 ambapo wananchi walitoa malalamiko kuelezea adha inayowapata na manyanyaso wanayofanyiwa na MGR Pamoja na kwamba wao walikuwepo hapo hata kabla ya Mkungunero kuwepo.
Wakuu wa Mikoa yote miwili waliahidi mbele ya wananchi kuwa watawaagiza MGR kusitisha mara moja vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wananchi wakati mgogoro huo ukipatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Pamoja na ahadi zote hizo ambazo zilileta matumaini makubwa kwa wananchi wa Kimotorok, vitendo vya unyanyasaji na uonevu mkubwa viliendelea miongoni mwa wananchi kutoka kwa walinzi wa MGR.
[h=2]HALI ILIVYO KWA SASA.[/h]
1.Walinzi wa mkungunero game Reserve husababisha kukosekana kwa amani na utulivu miongoni mwa wanakijiji kufuatia kauli yao kuwa kwamba sehemu kubwa ya ardhi ya kijiji ni ya MGR.walithibitisha kauli hiyo kwa kujenga kambi yao terehe 14/juni/2010 bila kuwasiliana na uongozi wa kijiji. Kufuatia ujenzi huo usiokuwa halali,tiliitisha kikao cha pamoja Tarehe 15/06/2010 kilichoongozwa na mwenyekiti wa kijiji kwa kuwajumuisha Mwakilishi wa MGR, Diwani wa kata na wajumbe wa serikali ya kijiji na kufikia makubaliano kwamba ,kambi iliyojengwa kimakosa na MGR katika eneo la kimotorok ivujwe mara moja na kuhamishiwa na ihamishiwe katika eneo lisilo kuwa na mgogoro.Pamoja na maazimio ya kikao na uwasilishaji wa taarifa mbalimbali katika ngazi za juu yetu, makubaliano hayakuheshimiwa na hadi sasa jengo hilo na kambi hiyo bado vipo katika ardhi ya kijiji Pamoja na kwamba mgogoro wenyewe haukutatuliwa . kwa mujibu wa sheria ya ardhi, shughuli zote za katika eneo lenye mgogoro husitishwa hadi ufumbuzi utakapopatikana. Tunauliza kwamba ni kwanini MGR inavunja sheria hii?
2. Kufuatia ubabe wa walinzi wa MGR wa kudai kwamba ardhi ya kimotorok ni sehemu ya pori la mkungunero.Tarehe 09/09/2009 wananchi waliofanya safari zao za miguu kwa nia ya kwenda kwenye vijiji vya wilaya ya kondoa kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa na mifugo walivamiwa,kupigwa na kiporwa mali zao mbalimnbali kama vile simu,mikuki sita,sime saba na fedha taslim TSh 714’000.Hivi majuzi vyombo vya habari kama RFA,Triple A kupitia kipindi cha magazeti viliripoti kwamba walinzi hao walipora TSh 4’000’000 za wafanya biashara wa kijiji cha Itolwa katika wilaya ya Kondoa .hata hivyo tuna Ngosiyei,Oleshiku Lemwande,Mustafa miraji huenda vifo vyao vimetokana na unyanyasaji huu..Tunaomba kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iitake serikali ifanye uchunguzi wa kina kubaini ukweli ya vifo vya watu hao.
3.Tarehe 01/05/2012 walinzi wa mkungunero kwa kutumia gari no STK 396 waliwinda visivyo halali swala pala digidigi mbili na kuwakamata watoto watatu( umri wao miaka 10,7 na 5) na kwapeleka hadi babati ambako yaliamriwa kuwarudisha mara moja waliko watoa,kwa kuzingatia haki za watoto na busara za kawaida.Siku iliyofuata yaani tarehe 2/5/2012 walinzi hao waliwauwa kwa kupiga risasi punda milia wawili na kuwachuna ngozi .Kijiji kitoa taarifa na doria ya wilaya ikafanyaika chini ya Ndugu Saiguran Mollel jambo lilowafanya walinzi hao kukurupuka na kuziacha ngozi hizo ambazo baadae zilikabidhiwa kikosi zidi ya ujangili Arusha ambayo hadi leo hatujajua hatma hiyo.Uwindaji huo haramu bado inaendelea kwa kasi kubwa sana na kwamba walinzi hao huwatishia usalama wa maisha ya watu waliotoa tarifa hiyo na kupeleka nyara hizo za serikali KDU Arusha.
4.Wananchi wa kijiji cha Kimotorok wamechoshwa na tabia mbaya inayoambatana na vitendo vya unyanyasaji kutoka kwa walinzi wa MGR kwani kila mara wanapoingia katika eneo la kijiji huwapiga wananchi na kupora mali zao kwa hoja kwamba kijiji cha Kimotorok kimeingia katika eneo la MGR.Kufuatia matukio ya uvamizi wa mara kwa mara na unyanyasaji kutoka walinzi wa MGR,utulivu na amani vimezidi kudorora na dhana ya uhifadhi imejigeuza na kuwa uwadui kwa upande wa wananchi,hivyo tunaiomba Kambi Rasmi Upinzani Bungeni iitake serikali iondoe mkanganyiko uliopo ili hatimaye kurejea kujenga na kuimarisha imani ya wananchi kwa serikali yao.
5.Kikao cha halmashauri ya kijiji cha kimotorok kiliwasilisha malalamiko yake dhidi ya MGR kwa mkuu wa mkoa kwa kuzingatia hoja kwamba halmashauri ya wilaya ya simanjiro ilikiri kutokuwa na uwezo wa kushughulikia ombi la kijiji hicho kuhusu kuhakiki na kupima upya mipaka ya kijiji kwa kuzingatia haki za wananchi ili kuepuka na kuondoa kabisa mtafaruku na mgogoro unaofukuta.Barua ya idara ya ardhi ya tarehe 26/2/2010,kumb no hakuna,ilielezea hali ya wilaya kutoweza kutekeleza ombi hilo la kijiji cha kimotorok.
6.Pamoja na hayo yote kijiji cha kimotorok, na wananchi wake wote wamepata hasara kubwa sana inayokadriwa kufikia milioni 800 iliyosababishwa na walinzi hao wa MGR. mhifadhi mkuu wa MGR amefika kijijini na kutaka kutoa fidia kwa uwizi mkubwa waliokuwa wakifanya walinzi wake kitendo ambacho wananchi wenye hasira kali walifika uwamuuzi wa kujichukulia sheria mkononi, na kama sii juhudi za viongozi wao mambo mabaya yangelitokea.
[h=2]HITIMISHO:[/h] Wananchi wa kimotorok wamekuwa na matumaini makubwa kwa Serikali ya Chama cha mapinduzi kwa kipindi kirefu, waliamini kuwa serikali isingeweza kuvumilia vitendo viovu wanayofanyiwa wananchi wake lakini imekuwa kinyume chake, Serikali ya CCM ndiyo imekuwa ikiibeba MGR na kuruhusu wananchi wa Kimotorok kunyanyaswa na kupuuzwa kwenye Ardhi yao na nchi yao.
Wananchi wa Kimotorok kwa sauti moja wanaiomba Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambayo ndo mmekuwa watetezi pekee wa haki za watanzania wote, wanawaomba mlitupie jicho mgogoro wa mipaka kati ya Mkungunero Game Reserve na Kjiji cha Kimotorok, imani yao kama wananchi wa Kimotorok imebaki kwenu.
Wanajua fika kuwa kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Pamoja na kwamba haina Dola lakini kupitia sauti yenu Bungeni na hata nje ya Bunge mnaweza kutetea haki ya watanzania wakiwepo wa Kimotorok.
wananchi wa wilaya ya Simanjiro wanampongeza Waziri kivuli wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh Halima Mdee kwa juhudi ambazo umekuwa ukionyesha hasa za kutetea Ardhi ya watanzania wakiwemo wa Simanjiro kijiji cha Loiborsoit A, hata hivyo tunaamini kutokana Taarifa hii hata sisi wananchi wa Kimotorok utatutetea.
vile vile wananchi wa Wilaya ya Simanjiro inampongeza waziri kivuli wa Maliasili na utalii mh Peter Saimon Msingwa, kwa jinsi alivyosimama kidete Bungeni kutetea Ardhi ya Wafugaji wa Ngorongoro, kupitia sauti ya Mh Msingwa wananchi wa Ngorongoro wamesikilizwa.
by Frank Oleleshwa
 
kwa niaba ya wanasimanjiro wenzangu na wanakimotorok wenzangu napenda nimtakake mbunge wetu na diwani wetu mh olesendeka na mh olemukusi wajitadhini na wajipime waone kama bado wanaweza kuendelea kuwa viongozi wetu, ilhali tunakutana na adha za namana hii.
 
mkuu nami kama mpigakura wa simanjiro naunga mkono hoja.
kwa niaba ya wanasimanjiro wenzangu na wanakimotorok wenzangu napenda nimtakake mbunge wetu na diwani wetu mh olesendeka na mh olemukusi wajitadhini na wajipime waone kama bado wanaweza kuendelea kuwa viongozi wetu, ilhali tunakutana na adha za namana hii.
 
kwa niaba ya wanasimanjiro wenzangu na wanakimotorok wenzangu napenda nimtakake mbunge wetu na diwani wetu mh olesendeka na mh olemukusi wajitadhini na wajipime waone kama bado wanaweza kuendelea kuwa viongozi wetu, ilhali tunakutana na adha za namana hii.

wameshindwa piga nje maccm
 
kwa niaba ya wanasimanjiro wenzangu na wanakimotorok wenzangu napenda nimtakake mbunge wetu na diwani wetu mh olesendeka na mh olemukusi wajitadhini na wajipime waone kama bado wanaweza kuendelea kuwa viongozi wetu, ilhali tunakutana na adha za namana hii.

uwezo wao ndio umeishia hapo
 
Huu ukoo uitwao CCM una laana hakyamungu! Kila wakati ni uongo tu tena uliokithiri dhidi ya wenye nchi waliowaweka madarakani.

Jambo la muhimu ni kuwa mwisho wao umekaribia sana!

CC malcom2
olevaroya.
 
Last edited by a moderator:
Wamasai wanahitaji kuelimishwa sana.Huyu Olesendeka ni mpiga kelele tu na kiboko yake ni Lowasa na hatokaa amseme Lowasa tena! kamwe!!
 
Back
Top Bottom