Ugomvi wa Sendeka, Shekifu waisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugomvi wa Sendeka, Shekifu waisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, May 11, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM).  Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM) na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Henry Shekifu, wamemaliza tofauti zao mbele ya Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha.
  Viongozi hao walishambuliana kwa maneno makali katika kikao cha ndani baada ya kutofautiana kuhusu ugawaji wa hekari 45,000 za ardhi inayotumiwa na vijiji sita mkoani Manyara.
  Wakiwa mbele ya Nahodha, ambaye alikuwa mkoani hapa kwa ziara ya siku moja, viongozi hao walimuahidi kuwa watahakikisha kuwa wanaendelea kuwatumikia wananchi.
  Nahodha aliwataka viongozi wa chama na serikali mkoani hapa kuepuka malumbano yasiyo ya lazima na kuelekeza nguvu zao katika kuwatumikia wananchi.
  Alisema hayo wakati akizungmza na viongozi na wananchi wa Wilaya ya Simanjiro, ambako alizindua shina la wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) la Kata ya Naisinyai.
  Ingawa hakutaja wanasiasa wanaolumbana, aliwataka kutambua kwamba wote wana jukumu la kuwatumikia wananchi na kwamba, wananchi wanataka kuona vitendo na wala sio maneno na malumbano.
  Alisema pamoja na changamoto zinazoikabili serikali katika suala la kuwatumikia wananchi, asilimia kubwa bado wana imani kubwa na chama na serikali yao na kwamba katika baadhi ya maeneo viongozi wamegeuka kuwa vikwazo.
  Nahodha alisema viongozi wa aina zote wana wajibu kuhakikisha kuwa kipaumbele cha kwanza kinakuwa kwa wananchi kwa kutatua kero zao na kujali maslahi yao na wala siyo vinginevyo.
  Alisema kuwapo kwa tofauti za mitazamo miongoni mwa viongozi, ni kitu cha kawaida ila ni vema kama tofauti hizo zikitatuliwa.
  Aidha alikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa CCM wanaodhani kuwa kuvaa mashati ya kijani, kufungua matawi ya wakereketwa na kujenga majengo inatosha kukifanya chama kishinde na akawataka kutambua kuwa wananchi wanachotaka kuona ni kutatuliwa kero zao na maslahi yao kulindwa.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...