Ole Sendeka akaribia kuzipiga kavu kavu na RC wa Manyara kwenye mkutano

Nakubaliana na wewe kabisa. Jana mimi nikajiuliza hivi TBC kuweka hewani ule ugomvi nia ni ipi hasa:confused3:!!! Hivi ni kweli maadili yanaruhusu mambo yote yawe tu hadharani? Ni swali tu! Tafadhali mtu asini:brick:, hivi vyombo vya habari huwa havipaswi kupembua na kuona umuhimu wa yale wanayoyatangaza? Hapa nia ilikuwa tuone nini? Ubabe ndani ya CCM au? Upuuzi ndani ya CCM?Natamani ningekuwa naweza ku :whip: wote pale! Pamoja na Tido. Tumegeuka yale mabunge ya ngumi mkononi! Itabidi kila aendae kwenye mkutano awe na pepper spray yake just in case mtu anakuletea fujo

Kuna wakati matumizi ya ngumi ni muhimu. Nadhani mambunge ambayo maji yakizidi unga wanatwangana yanaweza kufanya mambo mengi mazuri kuliko mihuri yetu hii tunayoishadadia. Naamini watu kama jirani zetu wa Kenya watafika mbali wakati sisi bado tunajidai kulinda heshima ambazo hatuna. Tukifikia mahali kama hapo pa kutwangana pale watu wazima wanapotaka kuwafanya wenzao nyau nafsi yangu itakuwa na amani sana.
 
hapa tutaongea juju tu, lakini shin ala hayo yote ni EL, EL yupo kwenye mkakati mzito wa kumwangusha Ole Sendeka, na hilo OS keshalijua na wala sio siri tena, katika kuangaika jinsi ya kumshusha OS, EL aliamua kumtumia RC na kuelezea jinsi hilo eneo litakavyomegwa na mwisho wa yote ni kuligawa hilo jimbo kwenye pande mbili, ile inayomsupport OS itaenda upande mwingine na ile inayompinga ndio atabaki nayo, kwa maana kuwa wakati wa uchaguzi jamaa atabaki na jamaa wasiomtaka, kwa hiyo mgawanyo huo unafanywa kisiasa zaidi na wala sio kimaendeleo ya kieneo, na watu wengi hawakupendezewa na hilo na ndio alipotokea jasiri mmoja na kumwambia huyo RC hicho kitu unachokifanya akikubaliki na ndio akaonekana ni kama mchonganishi na mleta fujo bila kuwa judged na hoja zake na ndipo RC alipoamua kumtoa nje, hicho kitendo cha huyo Morani kutolewa nje kilimuuzi sana OS na ndipo alipogoma huyo jamaa asitoke nje

all in all angalau sasa Watanzania tumeanza kuamka kwamba hata Mbunge na Mkuu wa Mkoa wanapandishiana adharani nadhani huu sasa ndio mwanzo wa mwisho wa CCM na Kampeni chafu za kisiasa bila kujali maendeleo ya raia wake
 
Mimi nimeona hiyo habari TBC1. Kasheshe limeanza baada ya mwananchi mmoja kupingana na RC kuhusu mgawanyo wa vitongoji. Ndipo RC akatoa amri atolewe nje ya mkutano. Sendeka alianza kumtetea kwa sauti ya chini ila baada ya hapo ndio wakaanza kupandishiana na RC. Kweli Sendeka alionekana anagonga meza lakini hata RC alikuwa anatembeza vitisho. Ndipo wakubwa wa wawili wa polisi walipofika kwenye meza kuu na kuanza kuongea na Sendeka ambaye alisikika akisema kuwa ameamua kunyamaza. Na hapo hapo RC akaendelea kurusha maneno mazito mazito ya vitisho na kwamba anaweza kumsweka ndani (detention). Siwezi kusema nani kamkosea mwenzake ila kitendo walichofanya ni cha utovu wa nidhamu kwani hakukuwa na haja ya kuzusha kasheshe kama hilo kwenye mkutano. Hata hivyo nadhani hawa wakubwa wanatakiwa kupunguza vitisho vya matumizi ya dola.

Thanks! umeeleza vizuri issue ilivyokuwa. Kama ndivyo sioni kosa la Sendeka kwa hapa. Kama ni mimi naona RC alilianzisha mwenyewe kwa sababu kama kilikuwa kikao umewaita watu wasikilize mawazo yao pia siyo kufanya hotuba wao wakusikilize tu. Kipimo cha uvumilivu wa mtu tunatofautiana hata mimi angenitisha tungetunishiana kwani hakuwa na hekima hadi atumie ubabe? Viongozi wetu tunawajua wenyewe jinsi walivyo vimeo na vyeo wanavipataje tunapojadili tusifanane nao.

Tunapoongelea issues wengine tunajikita katika historia za ugomvi na nani anamchukia nani. Hata kama unamchukia mtu, kunapokuwa na hoja jadili hoja badala ya attack zisizo na msingi. Mambo yale yale ya Rais unaongelea mgomo wa wafanyakazi unaanza kumshambulia mtu (personalizing) kutukana na vijembe, unaongelea ugeni bado vijembe. Hii nchi kama ya mipasho!
 
Jana jioni nilikuwa naangalia taarifa ya habari ya TBC1, moja kati ya habari zilizonivutia na kunishitua kidogo ni ile juu ya Mkuu wa mkoa wa Manyar bwana Andrew Shekiffu kumvukuza ndani ya mkutano huo Mbunge wa Simanjiro Ole Sendeka. Kwa mujibu wa habari hiyo sakata hilo lilianza baada ya mkuu huyo wa mkoa kutaka kumfukuza ndani ya mkutano huo mwananchi mmopja aliyekuwa anapinga kuanzishwa kwa kata mpya bila ya kijiji chao kuajumuishwa, sasa Sendeka ndio akasimama na kupinga agizo hilo. Baada ya hapo Shekifu akamjia juu Sendeka na kuaagiza nae pia atoke mkutanoni kwa vile alikuwa anavunja AMANI ndani ya mkutano. Vuta ni kuvute ilianza baada ya Sendeka kugoma kutoka mkutanoni kwa madai kuwa yeye ni mbunge wa eneo lile hivyo hawezi toka mkutanoni! Sakata hilo liliendelea kwa nusu saa na hata baada ya polisi kuingilia kati ,bado ilishindikana Sendeka kutoka., na mwisho kwa mujibu wa habari ile na walivyosikika wenyewe ( sendeka na shekifu), Sendeka aliendelea kubaki mkutanoni ila alisema hatoongea kitu, na shekifu alikubali kumuacha ila aliwaagiza polisi kumkamata Sendeka na kumfungulia mashtaka mara atokapo mkutanoni!

Sasa nauliza je kuna mwenye habari zaidi juu ya sakata hili?
 
Huu ni ubabe wa viongozi wetu waliopo kama unavyoona hata baba yao mwenyewe anavyotukana wananchi wake wanapodai maslahi yao. Kwa kifupi hawa wakuu wa mikoa wamejiona kama miungu watu na ndio maana mambo yanaenda hovyo sehemu nyingi. ni kwamba kila wakati hawataki kubishiwa kuwa taarifa fulani siyo ya kweli au hili siyo zuri. Badala ya kuseme hili siyo kweli, basi twende tukaone watakufukuza katika kikao kile, na pia badala ya kubishana kwa hoja hadi kitu hicho kikubalike basi watakufukuza katk kikao ambacho wao wanakuwa wenyeviti. (Hii imetokea sasa huu ni mkoa wa tatu -pengine na zaidi- watu wakibisha "TOKA NJE!! na matusi juu!"
matokeo ya haya mambo ni kwamba mambo ya maendeleo yanapotoshwa, na watendaji waovu wanajilinda kwa kuwa upande wao na hivyo kupitia udikteta uliozagaa Tanzania yetu wadangayika wataendelea kuumia kwa mipango ya uwongo
Mimi naona tuna hali ngumu sana ukutegemea watu wengi hawajafunguka kuhoji na kuwa ngangari kama Mh. Ole Sendeka (Kamanda halisi)
 
simpingi sendeka kwani imefikia sasa watu kupata ujasiri wa kusimamia haki za watu tunaowawakilisha, lakiniit depends on who called for the meeting, kama ni wa kimkoa then sendeka amekosea... ila kama ni kikao cha kijimbo then he was right
Boss wangu DN, mimi ni mhandisi so bear with me kwenye some of my lines of argument. Nadhani ili tuweze kupata results nchi hii yaonekana inabidi kuwa na watu ambao wako mechanical kidogo kwa sababu there's nothing that makes sense otherwise kwa these political animals in our midst, and that includes "kiranja" wetu mkuu. Mathalani, mgomo ni mechanical approach ambayo if pulled off by TUCTA am sure tungeona results. Nakumbuka migomo ya enzi hizo late 80's pale UDSM bila kutumia mechanical means migomo isingekuwa inafanikiwa (wale mnaokumbuka, ma-engineer wa mwaka wa pili walivyokuwa wanakwenda hall 3 ili kwenda "kuwashirikisha" dada zetu kuja kwenye "baraza" pale Nkrumah hall. Ilifanya kazi! Na kwa Shekifu & co.....nadhani mechanical brains za the Ole-Sendeka's of this world zilifanya kazi na siku nyingine Shekifu hawezi ku-bully watu tena hata kama platform ni yake! Hata mafisadi nadhani wanahitaji mechanical handling!
 
Labda tungepata alichosema yule mwanakijiji tungelijua yupi ni chanzo kati ya mwanakijiji RC na OS maana warusha habari walichoona na kutuletea ni vurugu tu je yale maneno yalikuwa hayajibiki? baada ya kuelewa alichosema ndipo tuje suala la RC na OS maana wengi tunaangalia action hatuangalii course of action

Ule mkutano ulikuwa wa kugawa vijiji, RC aliitisha ili atoe directives au kupokea maoni, kama ni kutoa directives kulikuwa hakuna haja ya kuitisha mkutano angeyafanya hivyo ofisini kwake, kama ni kupokea maoni basi RC alitakiwa awe mvumilivu kwa vile si wanakijiji wote wenye maoni sawa, alitakiwa kumsikiliza yule mwanakijiji hoja zake na kumjibu kwa sababu mipaka inatakiwa iridhiwe na wakaazi wa pale si kuwekewa kama tulivogawanywa kule Berlin Conference na wazungu.

mwisho aliye karibu zaidi na wananchi ndiye atayajua matatizo yao kiundani yawezekana ni mipaka ya mashamba, sehemu ya malisho ya mifugo, koo nk, mbunge wa Simanjiro hawezi kuhamishwa kuwa mbunge wa Kyela lakini RC kesho anaweza kuhamishwa kwenda kuwa RC wa Kigoma je atayajua matatizo ya ndani ya watu wa Mwandiga kwa muda mfupi? kwahiyo ingawa mkutano ule uliitishwa na RC lakini aliyekuwa na uelewa mkubwa wa matatizo ya mipaka ni mbunge, kwa hiyo RC hakuwa na busara kumtimua mtu muhimu anayetakiwa kuwepo na kujibu baadhi ya maswali badala yake angetumia diplomasia kumaliza tatizo hilo badala ya kutishiana kwa vyeo.
 
Mkuu Pasco naamini wewe ni mtu makini na huwa unajitahid kuchangia hapa jamvin kwa umakin wa kutosha... heshima mbele!!

Kwa hili la RC Shekifu na Ole Sendeka tuwe honest kidogo mkuu Sendeka alimkosea adabu RC....kwa kikao kile kimeitishwa na RC na munge yeye ni mwalikwa tuu ofcourse kwa kofia yake ya uwakilishi...
ishu nzima ilivyokuwa ni kwamba wakati RC anatoa maelezo ya namna vitongoji hivyo vinavyogawanywa kuna mtu alikuwa anabisha bisha tuu bila utaratibu kile alichokuwa anaeleza RC... kwa mamlaka yake as RC akasema mtu huyo atolewe nje Sendeka akasema asitolewe ghafla akazua zogo kwamba hapo ni kwenye jimbo lake hakuna wakumwingilia huku anapiga meza infact RC anaona na Sendeka anamdharau wakati anamwomba taratibu kwa chini chini atulie noway lazima sometime atumie cheo chake akataka atolewe nje na OCD mwishowe akakiri kikao ni cha RC na Sendeka akakiri hatatoka atanyamaza...

ukitizama ishu nzima utagundua Sendeka anakuwa na wasiwasi hata kwenye mambo yasiyostahili hili halina uhusiano wowote na Umasai au Umorani mkuu ....

hakuna mtu mkuu yupo juu ya Sheria... na hili ni jambo limesahauliwa na wakubwa wengi ...
wewe mkuu Pasco ni mjuzi wa sheria mtu anapokukumbusha kuhusu sheria flani na matumizi yake hakutishi anakuonya as the matter of fact RC anamkumbusha Sendeka sheria ya detention...

Kumuingiza Lowasa kwny ishu hii ya Sendeka kukosa adabu kwa RC nikumwonea Lowasa bure tuu mzee...

kwa hili mkuu Sendeka alichemsha as a leader hakupaswa kutetetea mtu anayeleta vurugu kwenye vikao halali tena kwa nguvu kubwa kiasi cha kuharibu personality yake....

kule Simanjiro Sendeka asimwone kila aliye against naye katumwa na Lowasa... by the way yupo kijana analitaka jimbo hili anatumia vizuri udhaifu wa vita vya Lowasa/Kone na Sendeka....nitarudi kukufahamisha maendeleo yake

SENDEKAAA TIGIREEE!!!!

Ole Lengeri.
Mkuu anabisha tuu bila utaratibu ndo maana yake nini. RC akatumia madaraka yake ndo nini? hapo ndo tatizo lilipotokea.Kama ulikuepo basi ungeweka wazi anabisha nini na kama alijibiwa au la. Inaonekana ilikuwa ni mkutano wa ushirikishwaji wa wananchi kwenye maamuzi.Tuwasikilize then tuwaelemishe nadhani ndo hoja ya ushirikishwaji. tusiende na majibu kabla ya kuwasikiliza.
 
Shekifu hakupenda kupingwa kwenye kile kikao, yule jamaa kuna jambo hakukubaliana nalo akanyanyua mkono kulipinga, ndipo Shekifu akamtaka yule jamaa atolewe nje, lakini Sendeka akaona yule jamaa anaonewa kwa kutolewa nje ndipi mtiti ukaanza, mpooooo, habari ndo hiyo, Akili ya mwezio changanya na ya kwako.
 
Ha ha ha ha ha, naona huu msemo unawaingia sana WADANGANYIKA Hata kama ni KIMEO uchanganye tu?
 
Mimi nimeona hiyo habari TBC1. Kasheshe limeanza baada ya mwananchi mmoja kupingana na RC kuhusu mgawanyo wa vitongoji. Ndipo RC akatoa amri atolewe nje ya mkutano. Sendeka alianza kumtetea kwa sauti ya chini ila baada ya hapo ndio wakaanza kupandishiana na RC. Kweli Sendeka alionekana anagonga meza lakini hata RC alikuwa anatembeza vitisho. Ndipo wakubwa wa wawili wa polisi walipofika kwenye meza kuu na kuanza kuongea na Sendeka ambaye alisikika akisema kuwa ameamua kunyamaza. Na hapo hapo RC akaendelea kurusha maneno mazito mazito ya vitisho na kwamba anaweza kumsweka ndani (detention). Siwezi kusema nani kamkosea mwenzake ila kitendo walichofanya ni cha utovu wa nidhamu kwani hakukuwa na haja ya kuzusha kasheshe kama hilo kwenye mkutano. Hata hivyo nadhani hawa wakubwa wanatakiwa kupunguza vitisho vya matumizi ya dola.

Ha hahaaa, kwani huyu nae sio Captain, luteni, ama luteni kanali kama yule tuliyemsikia juzi akipiga bit la Tabasamu?
 
Habari kamili, Shekifu ni pandikizi la mafisadi hasa Lowasa. Mnafahamu kuwa Lowasa alianza kujizatiti kwa kupanga safu ya wakuu wa mikoa na Wilaya? Hasa Arusha na Manyara!!! RCs na DCs? Japo jamaa alishashtukia maana sidhani kama uswahiba upo mkali kama awali au ni ka unafiki kanatawala. Ole Sendeka chapa makofi huyo!!! Yaani naye RC anatishia kama baba yake alivyotishia Nyau TUCTA!!!?? Kweli chama chetu ni cha wababe!!!!!
 
Mkuu Pasco naamini wewe ni mtu makini na huwa unajitahid kuchangia hapa jamvin kwa umakin wa kutosha... heshima mbele!!

Kwa hili la RC Shekifu na Ole Sendeka tuwe honest kidogo mkuu Sendeka alimkosea adabu RC....kwa kikao kile kimeitishwa na RC na munge yeye ni mwalikwa tuu ofcourse kwa kofia yake ya uwakilishi...
ishu nzima ilivyokuwa ni kwamba wakati RC anatoa maelezo ya namna vitongoji hivyo vinavyogawanywa kuna mtu alikuwa anabisha bisha tuu bila utaratibu kile alichokuwa anaeleza RC... kwa mamlaka yake as RC akasema mtu huyo atolewe nje Sendeka akasema asitolewe ghafla akazua zogo kwamba hapo ni kwenye jimbo lake hakuna wakumwingilia huku anapiga meza infact RC anaona na Sendeka anamdharau wakati anamwomba taratibu kwa chini chini atulie noway lazima sometime atumie cheo chake akataka atolewe nje na OCD mwishowe akakiri kikao ni cha RC na Sendeka akakiri hatatoka atanyamaza...

ukitizama ishu nzima utagundua Sendeka anakuwa na wasiwasi hata kwenye mambo yasiyostahili hili halina uhusiano wowote na Umasai au Umorani mkuu ....

hakuna mtu mkuu yupo juu ya Sheria... na hili ni jambo limesahauliwa na wakubwa wengi ...
wewe mkuu Pasco ni mjuzi wa sheria mtu anapokukumbusha kuhusu sheria flani na matumizi yake hakutishi anakuonya as the matter of fact RC anamkumbusha Sendeka sheria ya detention...

Kumuingiza Lowasa kwny ishu hii ya Sendeka kukosa adabu kwa RC nikumwonea Lowasa bure tuu mzee...

kwa hili mkuu Sendeka alichemsha as a leader hakupaswa kutetetea mtu anayeleta vurugu kwenye vikao halali tena kwa nguvu kubwa kiasi cha kuharibu personality yake....

kule Simanjiro Sendeka asimwone kila aliye against naye katumwa na Lowasa... by the way yupo kijana analitaka jimbo hili anatumia vizuri udhaifu wa vita vya Lowasa/Kone na Sendeka....nitarudi kukufahamisha maendeleo yake

SENDEKAAA TIGIREEE!!!!

Ole Lengeri.
Lengeri, asante kwa taarifa hizi. Ole Sendeka keshajulikana yeye moto, kwenye vita dhidi ya ufisadi ni kamanda, kwenye ile kesi ya kumpiga Ole Milya, ameshinda tuu kwa hoja za kisheria, yaani legal technicalities, wanasheria wake ni wazuri, walikuwa wakilipwa na Ole Mangi, kama hakimu atalipwa mshahara wa mwaka mzima kwa kazi ya siku moja, kwanini asifanye?.

It is a fact Sendeka alitembeza kichapo kwa Ole Milya, huu ni ubabe, hata akiongoe bungeni utamjuas kabisa ni hot tempared, hataki mambo yoyote ya kupuuzi puuzi, na CCM lazima imsimamishe tena Simanjiro, haijalishi inampenda au haimpendi vinginevyo Jimbo la Simanjiro linajiunga na kambi ya upinzani kwani chama chochote atakachosimama, anapita.

Viongozi wa serikali wanahitaji sana watu wa type ya Ole Sendeka kuwashikisha adabu, wengine wanajisahau na kujiona miungu watu, upuuzi huo Sendeka hautaki, na hicho kitisho cha MM kuwa ana powers za 48 hours detention order without trial, angethubuti kukitumia kwa Sendeka, mbona Arusha angehama!.
Amuulize RC mwenzake kilimkuta nini pale Wamasai walipochoma nyumba nne za viongozi wa CCM Masaini, akawashika na kuwatia ndani, mbona Arusha palitaka geuka dimbwi la damu, mwenyewe aliwaachia!.

Jamani mbabe Sendeka Mwacheni, bunge lijalo tutafute kina Ole Sendeka weka, kichapo kitakuja kumshukia mpaka spika akileta za kuleta kama alivyoimaliza hoja ya Richmond!.
 
kuna utaratibu wa kuuliza maswali............kiongozi akishamaliza ku-deliver ujumbe wake anaruhusu kama kuna maswali watu waulize.......vinginevyo muuliza swali katikakti ya hotuba anaweza kuambiwa swali lako litajibiwa kipindi cha maswali na majibu...........huwezi kuzuia watu wa aina hii kuwepo kwenye mikutano ya hadhara.....................Sijui Mbunge alisema nini...............lakini kama aliingilia alitakiwa amshauri mpiga kura wake kuwa asubiri mpaka wakti wa maswali na majibu.....................

........kama muda wa maswali na majibu haupo then mwananchi anaweza kushauriwa....aende ofisi husika ili apate majibu (akisaidiwa na mwakilishi wake)...........

Kitendo cha viongozi kuonyeshana ubabe mbele ya wananchi ni UTOVU WA NIDHAMU............PERIOD
 
Naona adabu karibu inarudi, ili tuheshimiane inatakiwa siasa safi na siasa safi hailetwi kwenye kisahani inatakiwa wawepo watu type ya kina Sendeka ngumi mkononi uungu mtu wa maRC na maDC karibu utakwisha nafikiri sisiem si wajinga hawatarudia makosa ya kumtupa kwenye kura za maoni kama walivyomfanya Slaa, keep on keeping on divide sisiem and rule.
 
Wengi wa viongozi wetu bado hawajaikubali wala kukubali ukweli kwamba sasa hivi ENZI za ndio mzee kwa kila kitu hata kiwe cha kipuunzi zimepita. Wanapotokea watu shupavu katika kuhoji mambo kama Ole Sendeka viongozi wanapata shida sana. Itabidi sasa wabadilike tu hawana namna.
 
Kazi kweli kweli, ukitetea haki unaonekana unataka kuvunja amani.
 
watapambana sana na hicho kifaa. Ole Sendeka anaandamwa na mzimu wa kifisadi, mara kataka kumpiga Millya, mara anavunja amani...mmmh kweli kutetea haki hapa Tz ni kazi kubwa!
Songa mbele shujaa, wamasai wanasifika kwa ujasiri na uaminifu, kasoro masai feki, EL.
 
ndo tatizo la kuweka wakuu wa mikoa majenerali na maluteni wanajeshi, sijui kama huyu naye ni mwanajeshi, ubabeubabe tu. nilikuwa sijapata picha kamili hapa. wakuu wengi wa mikoa hawana lolote ktk ufahamu na uongozi, wanawekwa tu ili kulinda maslahi ya ccm. nakumbuka kipindi kile wengi walichukuliwa kupelekwa uingereza sijui Russia kujifunza computer, ukikamata wengi hapo hawajui hata kinachoendelea hapa JF, bado wa miaka ileeee ya nyereereeee, dictatorship. huyo mkuu wa mkoa naona amejiaibisha tu, na hakufanya kwa hekima pia.
 
Huyu Sendeka, mbunge kutoka CCM, anatishiwa kuswekwa ndani na RC - je angekuwa mbunge kutoka Chadema au CUF, si ndiyo ingekuwa balaa ! Yaani hakika kuna mambo siyaelewi vizuri hapa;

  • Kwanza, Mbunge kapigiwa kura na wananchi lakini RC kateuliwa na Raisi.
  • Pili, Mbunge anawakilisha wananchi wa eneo lakini RC anamwakilisha Raisi.
  • Tatu, Mbunge hawezi kuhamishwa lakini RC anaweza kuhamishwa na Raisi muda wowote na kupelekwa mkoa wowote.
  • Nne, wapi iliko mipaka kati ya hii mihimili miwili ya dola, Bunge na Serikali ?
Mwenye majibu sahihi naomba anielimishe tafadhali.
 
Back
Top Bottom