Ole Sabaya: Doa jeusi kwa utawala wa Hayati Magufuli

Hii kesi inakwenda kuwavua nguo kama ile ya Akwilina. Hakuna mtanzania hata mmoja including hao waendesha mashtaka wa serikali anayeamini kuwa Mbowe ni gaidi. Huu uongo labda mkausemee kule Sudani
Hata mke wake mwenyewe hamwaamini, Sembuse wewe nani!
uliwahi kumsikia Mke wake anakanusha kuwa sio gaidi?
acha kupoteza muda wako.
 
Hakuna binadamu aliyekamilika; hata wewe hapo si ajabu umefanya makosa mengi tu aidha hadharani au kwa kificho. CCM kama ilivyo vyama vingine inaongozwa na binadamu walioumbwa na Mungu. Kukosea kwa mtu mmoja haimaanishi kuwa ni doa kwa chama chote. Wapo viongozi wengi tu wazuri na wanafanya kazi nzuri wanaotoka CCM. Tusijipe mamlaka ya juu ya kuhukumu mapungufu ya mtu isipokuwa kama tu na wewe u msafi kwa 100%
 
Kwa hiyo wewe ndio mke wake sio? Umemiss show naona. Mpelekee kule kule kuna nafasi ya faragha
 
Aliyekwenda angekuwepo leo hii Sabaya angekuwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro/DSM/Dodoma/Arusha, na kila siku angekuwa anamwagiwa masifa kuwa ni mchapakazi na mzalendo!! Hawa watu wanaopenda kujiita wazalendo wa kuogopa sana
Na usalama wa Taifa ulijua hili jambo na haukuweza kufanya chochote maana aliyekwenda ndo mtendaji mkuu huyu sabaya ilikuwa njia tu.
 
Hakuna binadamu aliyekamilika; hata wewe hapo si ajabu umefanya makosa mengi tu aidha hadharani au kwa kificho. CCM kama ilivyo vyama vingine inaongozwa na binadamu walioumbwa na Mungu. Kukosea kwa mtu mmoja haimaanishi kuwa ni doa kwa chama chote. Wapo viongozi wengi tu wazuri na wanafanya kazi nzuri wanaotoka CCM. Tusijipe mamlaka ya juu ya kuhukumu mapungufu ya mtu isipokuwa kama tu na wewe u msafi kwa 100%
Umeandika nini hiki?!🤮🤮
 
Tusitafute sababu za kukwepa uwajibikaji kisiasa kwa makosa dhahiri.
 
Yule wakili wake hajitambui, jana anahojiwa anasema hukumu iliyotoka ni nzuri na yeye ameipenda, sasa kama hukumu ni nzuri unakata rufaa ya nini?
Wakili yeye yuko kazini mkuu...! walikuwa wanajua kabisa tangu mwanzo kwamba hii kesi ya sabaya ni kimeo na kwa ushahidi uliopo hawezi chomoka lakini wao ni lazima wakomae tu na kesi kwa sababu ndiko wanapopatia mkate wao...
 
Hukumu iliyotolewa jana kwa Ole Sabaya, kuwa alikuwa jambazi la kutumia silaha kupora mali za wananchi, vile vile limeupaka matope utawala wa Magufuli.

Kwamba mteule wa Rais, akafanya mambo kinyume na utawala wa sheria na mbaya zaidi ujambazi, ni vigumu kueleweka kirahisi kwa nini haya yaliruhusiwa kutokea.

Utawala wa Magufuli mara kadhaa umelaumiwa kutoheshimu haki za binadamu na mali zao, huu mfano wa Sabaya umejitokeza kukubaliana na hoja hizo.

Kwamba kulikuwepo na wasiojulikana, watu kutekwa na baadaye aidha kupotea au kurudishwa na wasiongee yaliyowasibu, hili la Sabaya linathibitisha uhusika wa viongozi fulani, ndani ya Dola, wakiwa na baraka " kutoka juu".

Kwa vyovyote vile Ole Sabaya ni doa jeusi na ambalo si zuri kwa utawala wa Magufuli.
Magu alidhani anamsadia huyu dogo kimbe ndiyo alimuharibia future yake, huyu mwenda zake nafikiri hata malezi alikuwa ziro
 
Legacy ya JPM haiwezi kamwe kufutika na chuki hizi zinazoendelee.

JPM anabaki kuwa Rais shupavu na hodari tangu Tanzania ipate uhuru akiongozwa na Baba wa Taifa akifatiwa na Mzee Mkapa.

JPM anaishi na ataendelea kuishi huyo ras wenu mwambieni akanyoe rasta aache na kuvuta bangi
PU!!
 
Hukumu iliyotolewa jana kwa Ole Sabaya, kuwa alikuwa jambazi la kutumia silaha kupora mali za wananchi, vile vile limeupaka matope utawala wa Magufuli.

Kwamba mteule wa Rais, akafanya mambo kinyume na utawala wa sheria na mbaya zaidi ujambazi, ni vigumu kueleweka kirahisi kwa nini haya yaliruhusiwa kutokea.

Utawala wa Magufuli mara kadhaa umelaumiwa kutoheshimu haki za binadamu na mali zao, huu mfano wa Sabaya umejitokeza kukubaliana na hoja hizo.

Kwamba kulikuwepo na wasiojulikana, watu kutekwa na baadaye aidha kupotea au kurudishwa na wasiongee yaliyowasibu, hili la Sabaya linathibitisha uhusika wa viongozi fulani, ndani ya Dola, wakiwa na baraka " kutoka juu".

Kwa vyovyote vile Ole Sabaya ni doa jeusi na ambalo si zuri kwa utawala wa Magufuli.

Ya Bashite je?!!!
 
Legacy ya JPM haiwezi kamwe kufutika na chuki hizi zinazoendelee.

JPM anabaki kuwa Rais shupavu na hodari tangu Tanzania ipate uhuru akiongozwa na Baba wa Taifa akifatiwa na Mzee Mkapa.

JPM anaishi na ataendelea kuishi huyo ras wenu mwambieni akanyoe rasta aache na kuvuta bangi😡
Legacy inazidi kuchafuka.
 
Lakini hao hao wateule wa nduli Jiwe wote walikuwa hawamkubali labda mpango tu.

Wakumbali ili iweje ilhali wao ni wateule wake, au hujui hata maana ya kuwa mteule!??

Wananchi ndio tunapaswa kumkubali au kumkataa kiongozi, ila mteule yoyote akiona haendani na matakwa ya bosi wake anapaswa kustep down

Na wananchi tulio wengi tulimkubali sana Magufuli na legacy aliyoaiacha itaishi kwa miaka mingi sana.
Kama babu yangu alinihadhithia utendaji uliotukuka wa akina Nyerere na Sokoine basi nami nitahadithia wajukuu zangu ushupavu wa The Late Magufuli
 
Mkuu ingalau mama Samia kachukua hatua ya kuruhusu uchunguzi wa kijinai ufanyike na mtuhumiwa kupelekwa mahakamani kujibu tuhuma.

Matokeo tumeyaona, kwa mama Samia hili ni tukio chanya, lakini je akitikea Magufuli mwingine itakuwaje?
Nakubali hoja yako lakini haimtoi katika uwajibikaji kwa kuchukua hatua kiduchu. Jukumu la msingi la serikali yo yote inayostahili jina hilo ni kulinda uhai na mali ya raia. Ndiyo maana wastaarabu viongozi wengine husita kusaini kibali cha kumnyongwa raia hata kama mahakama imefikia uamuzi huo! Pia adui vitani ukimteka na hana silaha wala tishio la kupigana huruhusiwi kumwua kwa sheria za kistaarabu. Sasa hii Tanzania wenzetu wanapata wapi kuwanyanyasa binadamu na Watanzania wenzetu. Na kiongozi gani, hata police au mwanajeshi. officer material, ambaye hajui huu ustaarabu kuwa unahitaji kukomeshwa mara moja!?
 
Kuna serious failure ya checks and balance katika nchi yetu.

Viongozi wa juu ni kama wamepewa open cheque na kufanya lolote wanalotaka.
 
Bado ameomba kukata rufaa atajisafisha tu.

Hapa kazi tu.
Yeye akijisafisha basi serikali itakuwa imepakwa kinyesi, Wananchi tutaamini alichokisema Sabaya kwamba alikuwa anatumwa na mamlaka iliyo juu yake.
Sasa sijui Kama hiyo serikali itakuwa na uhalali wa kuendelea kuwepo hata ikiwepo sijui Kama Kuna mwananchi atakuwa na imani nayo.
 
Wahenga walisema kuwa kila masika na mbu wake.

Kweli hakuna marefu yasiyo na ncha hapa duniani.

Tazameni jinsi vijana hawa walivyo kuwa wanakula nchi na majivuno kibao.

Leo hii mida hii anagombea kupanga foreni na bakuli la ammonium akapate ugali.

Hukumu iliyotolewa jana kwa Ole Sabaya, kuwa alikuwa jambazi la kutumia silaha kupora mali za wananchi, vile vile limeupaka matope utawala wa Magufuli.

Kwamba mteule wa Rais, akafanya mambo kinyume na utawala wa sheria na mbaya zaidi ujambazi, ni vigumu kueleweka kirahisi kwa nini haya yaliruhusiwa kutokea.

Utawala wa Magufuli mara kadhaa umelaumiwa kutoheshimu haki za binadamu na mali zao, huu mfano wa Sabaya umejitokeza kukubaliana na hoja hizo.

Kwamba kulikuwepo na wasiojulikana, watu kutekwa na baadaye aidha kupotea au kurudishwa na wasiongee yaliyowasibu, hili la Sabaya linathibitisha uhusika wa viongozi fulani, ndani ya Dola, wakiwa na baraka " kutoka juu".

Kwa vyovyote vile Ole Sabaya ni doa jeusi na ambalo si zuri kwa utawala wa Magufuli.
Hakuna Cha doa jeusi,ule utawala ulikuwa wa kishetani tangu mwanzo,utawala mzima ulikuwa mweusi kama mkaa.
 
Back
Top Bottom