Ole Sabaya asomewa mashtaka mapya 5 ya uhujumu uchumi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha yapewa mamlaka kusikiliza kesi

Huyu jamaa inaonekana alikuwa akitumia ukuu wa wilaya kuongoza genge la wahuni wenzake kupora mali na wanawake wa watu , kama ni kweli acha ashughulikiwe
 
Ukiunganisha doti doti vizuri, utaona ametumiwa kukamilisha jambo kubwa lililopangwa bila Ole Sabaya kutambua yeye kuachwa kufanya uhalifu waziwazi, kwa upande mwingine kulikuwepo wanufaika waliopo pembeni wenye nguvu kubwa ktk parallel state / forces / government kama bwana Polepole alivyosema wakitaka kukamilisha mpango wao ovu wa kuwa na nchi ya chama kimoja.
 
Kwa kweli! Mbona kama tuliambiwa utetezi/ushahidi ulikamilika na tunasubiri hukumu tarehe 1 Oktaba. Imekuwaje tena?
Hilo halijabadilika ila kuna mashtaka mapya na akiyamaliza anapelekwa Moshi akakabiliane na mashata mengine, goma ndiyo kwanza limeanza.
 
16 September 2021

Kesi ya Uhujumu Uchumi ya Sabaya, Mashahidi 20 kuitwa na upande wa serikali (Jamhuri), vielelezo 16 vya ushahidi kuwekwa wazi mbele ya hakimu




KESI NAMBA 27 / 2021 YA UHUJUMU UCHUMI

Mahakama yaelezwa jinsi Sabaya na wenzake walivyochukua Sh90 milioni
Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imeelezwa kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita walimkamata na kumpeleka mfanyabiashara, Fransis Mrosso, katika Benki ya CRDB tawi la Murombo na kumshinikiza awape Sh90 milioni baada ya kumtuhumu kufanya biashara bila kutoa risiti na kuingiza vipuri vya magari bila kufuata taratibu.
Source : Mwananchi Digital
 
30 September 2021
Arusha, Tanzania

Muendelezo wa kesi:
KESI NAMBA 27 / 2021 YA UHUJUMU UCHUMI

KESI ya SABAYA: SHAHIDI ATAJA GARI LA SERIKALI, LINA VIOO Vya 'TINTED', ASHINDWA KUSOMA....

SHAIDI wa tatu upande wa Jamhuri Aida Marandu, ambaye ni mlinzi wa Kampuni ya Mroso Injection Service ameileza mahakama kuwa mnamo Januari 22, 2021 saa nane na dakika 35 zilifika gari tatu katika ofisi hiyo zikiwa na watu saba.

Source : Global TV online
 
Back
Top Bottom