Ole Sabaya asomewa mashtaka mapya 5 ya uhujumu uchumi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha yapewa mamlaka kusikiliza kesi

Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
9,029
2,000
Daah kazi ipo kwa kweli hii ishu niliisikia kuhusu huyo mzee na walichukua huo mpunga benk kabisa kwa vitisho...
 

chivala

JF-Expert Member
Apr 13, 2021
774
1,000
09 September 2021
Mahakama ya Hakimu Mkazi
Arusha
Tanzania

SABAYA ASOMEWA MAKOSA MAPYA MATANO "ALICHUKUA MILIONI 90 KWA MFANYABIASHARA"

Aliyekuwa mkuuu wa wilaya ya hai Lengai Ole Sabaya na wenzake sita wamesomewa shtaka la uhujumu uchumi lenye makosa matano kwa madai yakuchukua million 90 kutoka kwa mfanyabiashara ili wasimchukulie hatua kwa kosa la ukwepaji wa kodi.

Ole Sabaya na wenziwe wakituhumiwa makosa ya uhujumu uchumi, unyang'anyi wakutumia silaha na utakatishaji fedha.

---
DPP aipa mamlaka Mahakama Hakimu Mkazi kusikiliza kesi ya Sabaya na wenzake

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) imeipa mamlaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake.

Ole Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashitaka matano ikiwemo kujihusisha na rushwa na utakatishaji fedha haramu Sh90 milioni.

Ofisi ya DPP imewasilisha hati ya kuipa mamlaka mahakama hiyo, leo Alhamisi Septemba 9, 2021 kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tarsila Gervas wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi namba 27, 2021 ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda, Wakili Tarsila ameieleza Mahakama kuwa DPP ametoa hati na ridhaa hiyo ya mahakama hiyo ya chini kusikiliza kesi hiyo.

"Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hii, ila DPP chini ya Kifungu cha 12(3) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi ameona kwa maslahi mapana ya Taifa shauri hili lisikilizwe mahakama hii ya chini.

“Tutaanza kuwasilisha hati hizi alizotoa DPP na kwa kuwa Mahakama imekuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hii ni rai yetu kuwasilisha hati ya mashtaka na kuwasomea," amesema.

Baada ya Mahakama kupokea nyaraka hizo Wakili huyo aliwasomea upya mashitaka matano yanayowakabili ambayo ni kuongoza genge la uhalifu, kujihusisha na kitendo cha rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na utakatishaji fedha haramu Sh90 milioni, makosa ambayo washitakiwa hao walikana kuyatenda.

Kati ya makosa hayo matano, Sabaya peke yake anakabiliwa na makosa matatu ambayo ni kujihusisha na kitendo cha rushwa, kujihusisha na vitendo cha rushwa na kuchukua rushwa Sh90 milioni kutoka kwa Francis Mrosso na matumizi mabaya ya madaraka akiwa DC.

Mengine ni kumtishia Mrosso kuwa atamfungulia mashtaka ya kukwepa kodi kitendo ambacho ni kinyume na sheria kwa lengo la kujipatia fedha ya Sh90 milioni.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo na kuyakana kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 13, 2021 ambapo watasomewa hoja za awali za kesi hiyo.

Chanzo: Mwananchi
Huyu kijana Sabaya cheo ndicho kilichomponza
 

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
5,619
2,000
Daah kazi ipo kwa kweli hii ishu niliisikia kuhusu huyo mzee na walichukua huo mpunga benk kabisa kwa vitisho...

Huyo ndio walimuwekea pembe za Ng’ombe wakamdanganya ni pembe za ndovu halafu alikua hazifahamu, yule mzee alikua umoja wa mataifa
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,287
2,000
Wale waliodai huyu mtu atachomoka basi kama kweli atachomoka na kesi zote hizo nitaamini kweli uchawi upo.
Kuna kamchezo hapo....ile kwanza anaweza akapigwa fine au kifungo....zilizobakia zote ni fine pia....analipa zote huyu alikitoa mhanga anewekeza 3bil kwa wafanya biashara Arusha na Nairobi.....alikuwa anajua anafanya nini
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom