Ole Sabaya asomewa mashtaka mapya 5 ya uhujumu uchumi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha yapewa mamlaka kusikiliza kesi

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,245
24,108
09 September 2021

SABAYA ASOMEWA MAKOSA MAPYA MATANO "ALICHUKUA MILIONI 90 KWA MFANYABIASHARA"

Aliyekuwa mkuuu wa wilaya ya hai Lengai Ole Sabaya na wenzake sita wamesomewa shtaka la uhujumu uchumi lenye makosa matano kwa madai yakuchukua million 90 kutoka kwa mfanyabiashara ili wasimchukulie hatua kwa kosa la ukwepaji wa kodi

Muendelezo / updates

16 September 2021

Arusha, Tanzania

SABAYA MAHAKAMANI "ALISIMAMA NJE YA BENKI MROSO AKATOA MIL. 90"




KESI NAMBA 27 / 2021 YA UHUJUMU UCHUMI
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai lengai ole Sabaya pamoja na wenzake sita wanaoshtakiwa kwenye kesi ya uhujumu uchumi waameanza kusomewa maelezo ya awali huku jamhuri ikitarajia kuleta mashahidi 20 pamoja na vielelezo 16...
....
Source : Millard Ayo

16 September 2021

Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imeelezwa kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita walimkamata na kumpeleka mfanyabiashara, Fransis Mrosso, katika Benki ya CRDB tawi la Murombo na kumshinikiza awape Sh90 milioni baada ya kumtuhumu kufanya biashara bila kutoa risiti na kuingiza vipuri vya magari bila kufuata taratibu.

Akisoma maelezo ya mashitaka ya uhujumu uchumi yanayomkabili Sabaya na wenzake leo Alhamisi Septemba 16, 2021, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Felix Kwetukia amesema Sabaya na wenzake waligawana fedha hizo baada ya kuzichukua benki. Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Patricia Kisinda.

Amesema siku ya tukio Januari 22, watuhumiwa wote wakiongozwa na Sabaya walienda katika gereji inayomilikiwa na Mrosso eneo la Mbauda jijini Arusha na walipomkuta walimwambia yeye ni mkwepa Kodi.

Wakili Kwetukia alidai Sabaya na wenzake walimtuhumu Mrosso kwa kuingiza vifaa vya magari kutoka Dubai na Nairobi kupitia Zanzibar bila kufuata utaratibu wa kulipa kodi.

“Kufuatia kumpatia tuhuma hizi, mtuhumiwa wa kwanza (Sabaya), ulimtishia Mrosso kwamba asipofanya kitu mtampatia kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha. Kufuatia kumtishia huko na bila kufahamu nini afanye, Mrosso alimuuliza Sabaya ni kitu gani anatakiwa kufanya,”alidai.

“Sabaya alimwelekeza atoe Sh 90 milioni kwa washitakiwa wenzake ili awe huru kutokana na tuhuma ambazo wamempatia. Pale mwanzo Mrosso alikataa hilo lakini kutokana na vitisho na pasipokujua kuwa ni matokeo gani yatafuata alikuja kukubali kulipa kiasi hicho,” alidai wakili huyo wa Serikali.

Wakili Kwetukia aliendelea kuieleza mahakama kuwa watuhumiwa hao wakiwa na Mrosso walikwenda benki ya CRDB, tawi la Kwa Morombo ambapo mhanga huyo alitoa kasi hicho cha fedha katika mazingira ya kulazimishwa akiwa katika usimamizi wa karibu wa watuhumiwa wenzake na Sabaya.

Mbali na Sabaya, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27 ya mwaka huu, ni Enock Mnken (41), Watson Mwahomange (27) na John Aweyo, wote wakazi wa Arusha.
Wengine ni Sylvester Nyegu (26), mkazi wa Bomang’ombe, wilayani Hai, Jackson Macha (29), mkazi wa Moshi na Nathan Msuya (31) mkazi wa Msangara Kilimanjaro. Wote wanatetewa na Mawakili Mosses Mahuna,Charles Adiel,Sylvester Kahunduka na Fridolin Gwemelo


Awali Kutoka maktaba:

09 September 2021

Mahakama ya Hakimu Mkazi
Arusha
Tanzania

SABAYA ASOMEWA MAKOSA MAPYA MATANO "ALICHUKUA MILIONI 90 KWA MFANYABIASHARA"

Aliyekuwa mkuuu wa wilaya ya hai Lengai Ole Sabaya na wenzake sita wamesomewa shtaka la uhujumu uchumi lenye makosa matano kwa madai yakuchukua million 90 kutoka kwa mfanyabiashara ili wasimchukulie hatua kwa kosa la ukwepaji wa kodi.

Ole Sabaya na wenziwe wakituhumiwa makosa ya uhujumu uchumi, unyang'anyi wakutumia silaha na utakatishaji fedha.

---
DPP aipa mamlaka Mahakama Hakimu Mkazi kusikiliza kesi ya Sabaya na wenzake

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) imeipa mamlaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake.

Ole Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashitaka matano ikiwemo kujihusisha na rushwa na utakatishaji fedha haramu Sh90 milioni.

Ofisi ya DPP imewasilisha hati ya kuipa mamlaka mahakama hiyo, leo Alhamisi Septemba 9, 2021 kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tarsila Gervas wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi namba 27, 2021 ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda, Wakili Tarsila ameieleza Mahakama kuwa DPP ametoa hati na ridhaa hiyo ya mahakama hiyo ya chini kusikiliza kesi hiyo.

"Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hii, ila DPP chini ya Kifungu cha 12(3) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi ameona kwa maslahi mapana ya Taifa shauri hili lisikilizwe mahakama hii ya chini.

“Tutaanza kuwasilisha hati hizi alizotoa DPP na kwa kuwa Mahakama imekuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hii ni rai yetu kuwasilisha hati ya mashtaka na kuwasomea," amesema.

Baada ya Mahakama kupokea nyaraka hizo Wakili huyo aliwasomea upya mashitaka matano yanayowakabili ambayo ni kuongoza genge la uhalifu, kujihusisha na kitendo cha rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na utakatishaji fedha haramu Sh90 milioni, makosa ambayo washitakiwa hao walikana kuyatenda.

Kati ya makosa hayo matano, Sabaya peke yake anakabiliwa na makosa matatu ambayo ni kujihusisha na kitendo cha rushwa, kujihusisha na vitendo cha rushwa na kuchukua rushwa Sh90 milioni kutoka kwa Francis Mrosso na matumizi mabaya ya madaraka akiwa DC.

Mengine ni kumtishia Mrosso kuwa atamfungulia mashtaka ya kukwepa kodi kitendo ambacho ni kinyume na sheria kwa lengo la kujipatia fedha ya Sh90 milioni.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo na kuyakana kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 13, 2021 ambapo watasomewa hoja za awali za kesi hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom