Hii article imeandikwa na mkuda mmoja mwenye malengo yake binafsi! Hainiingii akilini Intelligensia ya KGB ya bwana Puttin isilijue hili mpaka ikubali nchi yake ya Russia kuwa miongoni mwa wanachama. Hivi nchi ngapi Africa zimejiunga na OIC hapa Afrika tena nchi ambazo waislamu ni asilimia ndogo sana kama Uganda na Mozambique na je wameathirika na uanachama wao wa OIC? Hebu acheni propaganda zisizo na kichwa wala miguu kwa mambo msiyoyajua:
Wewe mleta hoja kama kweli una uhakika na unachokisema hebu tuletee reliable source hata kama inatokea Vatican nitaikubali! Huna lolote na roho yako ya fitna.
Organisation of Islamic Cooperation - Wikipedia, the free encyclopedia
Member states of the Organisation of Islamic Cooperation - Wikipedia, the free encyclopedia
http://www.oic-oci.org/home.asp
Fuatilia hizo link ujue ukweli kuhusu OIC!
Mozambique haikujiunga kwa sababu OIC ilikuwa na mazuri yoyote bali ilifanya hivyo kipindi Afrika Kusini ikiwa chini ya makaburu na wakati huo kulikuwa na kikundi cha kibaguzi cha Kiyahudi hapo SA amabacho kilikuwa kinaunga mkono wahasi wa Mozambique. Kwa hasira na kama kusema adui yako mpe kero kwa kujiunga na adui yake basi Mozambique ikajiunga na OIC. Uganda nao ni hivyo hivyo walijiunga kipindi inatawaliwa na Idd Amin. Hakukuwa na muafaka wa kitaifa kwa kufanya hivyo but sort of bulldozing. Naiweka record sawa.
Lakini hii haituzuii Watanzania kujadili umuhimu wa kujiunga na OIC kama organisation. Kinacholeta shaka ni kuwa wanaoipigia OIC chapuo ni Waislamu. Kama UMOJA huu una faida kwa watu wa dini zote kwanini sehemu moja ya Watanzania ndio imekuwa inasisitiza kujiunga? Kwanini isiwe ni muafaka wa Watanzania wote? Kama ni misaada kwa Waislamu basi wao na vyama vyao wajiunge kuliko nchi