OIC: Mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo

OIC: Mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo

Mbona kichwa cha habari hakiendani na content? Maelezo yanaonyesha uzuri wa oic lakini ww kwa chuki zako umeamua kupotosha

Anapotosha au ni kweli? Umeshasoma Katiba ya OIC? Hata wanaong'ang'ania Oic kwa Tanzania ni kweli wana udini wa wazi kwani hiyo ni taasisi ya kidini kabisa na malengo yake yako wazi kabisa. Hakuna sababu ya kuficha kwa sababu katiba yake ipo na malengo yako. Ni organization ya nchi za kiislamu hata kama kuna nchi nyingine zilizojiunga. Ni vema watanzania tukabaki na utanzania wetu ambao umetuweka pamoja. Ogopa sana watu wanaotaka mambo kwa nguvu. Wana lao jambo.
 
Kuna nchi nyingi hapa duniani zimejiunga na oic na wala hakuna matatizo,kwanini watanzania mna chuki? Acheni oic iwanufaishe watanzania hasa wananchi maskini
ndg yng tuambie ni gani zimenufaika kiuchumi na oic,maana kat ya nchi maskini zaid dunian miongon mwao ni niger ,mauritania ,msumbiji,uganda
 
Kwa waislamu kama dini wajiunge tu hakuna shida,Lakini Tanzania kujiunga kupitia katiba ya nchi yaani SHERIA MAMA TUMEKWISHA,Tanzania serikali haina dini,si vema jambo la dini moja kati ya dini nyingi likatiwa katka katiba, ina halalisha kwamba dini ilotajwa katka KATIBA ndo itakuwa dini ya nchi na itatawala madhehebu yote na mengine kufutwa ikibidi ili dini hiyo itawale bila bughuza!kwa tujuavyo dini nyingine misimamo mikali sana!
 
Tanzania tulivyojenga utamaduni wa kulinganisha na kufananisha matukio tutajuta,wanaozani tanzania ikijiunga na oic itafanana na vyama vingi vilivyopo nchini wamenoa,kwamba ccm inatawala nyuma yake kuna chadema.cuf, tlp nk. Kwa dini haitakuwa hivyo,mambo ya kiimani yangeachwa misikitini kwa mashehe na makanisani kwa makasisi kamwe yasichanganywe ktk nchi na siasa kupitia hasa katiba ya nchi,hatujui yakipitishwa miswada yake itakayofuata itasema nini je? Kama dini moja itaandikwa kikatiba halafu wakapitisha muswada wa kusema wakristu wote muingie msikitini asiyetaka anachinjwa na police wanapewa maagizo si tutakwisha? Kwani dhamira yao si nzuri.
 
acha kupotosha watu hebu tuambie kuna nchi nying zimejiunga na OIC na zina idadi kubwa ya wakristo je huko hali ipoje au vita tu. Tatizo lipo kwa mleta mada amejaa udini na hutoweza kusolve tatizo la udini kama umejaa chuki za kidini
 
Nchi hii maamuzi huwa yanatolewa na christians, jambo wakilibarki mapadri na maaskof basi haraka litakuwa...tusubiri kama watabariki soon tutajiunga.(ingekuwa bora km hii tungeiacha) Tuombe tu wakubali hata km wataendelea waislam ili mradi ni watz ndio upendo, kuzuilia kitu cha maendeleo kisa kinalenga imani fulani basi umezuia maendeleo ya tz. Mapadri na maaskof toeni matamko ya kubariki jambo hili lipate msukumo hapo ntaona tz tunapendana,otherwise ikiwa cha waislam wakristo kukipinga na cha wakristo waislam kukipinga tunairudisha nchi nyuma. Km kweli wtz tunapenda maendeleo ya tz tuzipiganie fursa zozote hata zikiwa za kidini ili mradi tu wanaonufaika ni watz. (Cha msingi tuwe wamoja)
 
ndg yng tuambie ni gani zimenufaika kiuchumi na oic,maana kat ya nchi maskini zaid dunian miongon mwao ni niger ,mauritania ,msumbiji,uganda
Mnakataa oic ya Amani na Maendeleo ya waislam ,ok endeleeni na chuki na fitna dhulma then within 5year mtaona pick up with dishker and antieacraft za mujahideen zinakatiza Mitaani.
 
Watanzania wenzangu, nnani amewaloga??? Huo msaada wa IOC, kwa nini uwe na masharti??? Kwani ni lazima tuupate ndio tutaishi??? Kama unataka kunisaidia nikakataa ya nini kunisogezea kila siku huo msaada nisioutaka? OIC tunakuomba peleka kwa wengine, wakifanikiwa mje kutuita tukayaone hayo maendeleo mliowapa sisi tukakataa. Umaskini wetu utatumaliza jamani!!! Kama tungepata viongozi waadilifu tu, gas ya Mtwara ilitosha kutukomboa. Hata hao IOC hawana lolote bila petroli. Jamani, njaa ya siku moja tu haitatuua. Tujadili mambo ya mbole. Gas Mtwara ikilindwa vizuri, hatutahitaji msaada wa masharti. Ati kwa msaada unaokuja liwa na hao hao viongozi waliovimbiwa ulafi, mnataka kutusilimisha. Hatudanganyikiiiiiii. Siku ipo, na sisi tutapata gas na mafuta yetu. Tutauza na kuuza mpaka tusahau njaa zetu.
Mtanzania, kaza buti mwanangu, usikubali kudhalilishwa.
 
Back
Top Bottom