Kindembwile
Member
- Sep 18, 2018
- 62
- 44
Akili kubwa sana hii ya kiuandishiHabalini Wanajanvi.
Zamani zile kabla Tekinolojia haijakua sana hakukua na hizi Wireless Spika zenu za sasa, yaani ili mziki usikike basi Mitambo ilikua ni lazima iunganishwe na Spika kwa kutumia Nyaya.
Sasa siku hizi Spika za kisasa Haziunganishwi kwa Nyaya tena, zinaunganishwa kwa mifumo ya Wireless kama vile mfumo wa Blutooth, au Wi-Fi n.k.
Tatizo la hizi Wireless Spika ni kua zinaweza kuingiliwa na Mitambo tofauti na hivyo Msikilizaji akajikuta anasikiliza mziki usio wa Mitambo yake. Kwa mfano, Spika inaweza kua Dodoma lakini ikaingiliwa ki Blutooth au Ki Wi-Fi na Mitambo iliyopo Dar na hivyo Msikilizaji akajikuta anacheza Mziki wa Dj wa Dar.
Zamani haikua hivyo yaani kama Spika ipo Dodoma basi Msikilizaji atausikia Mziki wa Mitambo ya Dodoma, maana hakukua na njia ya ki Wireless kuunga Mitambo ya Mbali kama ilivyo Leo.
Zamani ilikua Spika ya Dodoma, Mitambo ya Dodoma na Mziki wa Dodoma.
Leo hii ni Spika ya Dodoma, Mitambo ya Dar na Mziki wa Dar.
Kweli Tekinolojia inakuja na Mambo Mapya.

Sent using Jamii Forums mobile app

