Ofisa JWTZ ahofiwa kutorokea Rwanda

jk hana tofauti na halima mdee kijeshi wote ni makuruta wa jkt, hivi inawezekana mwalimu wa katiba ya CCM jeshini akapanda mpka kuwa kanali.
Hii kali!! Mkuu vijana wote wa lika la Mh.JK waliokuwa wanamaliza FORM SIX walikuwa wanapashwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria kwa muda wa miezi sita kabla hawaja jiunga na Vyuo Vikuu nk - kwa hiyo mambo ya ukruta na kupiga fang fang lillikuwa jambo la kawaida kabisa. Mkuu naona uamini kwamba mwalimu wa siasa anaweza kupanda cheo mpaka kufikia ngazi za juu, nashanga sana kwa nini unauliza swali hilo, je una uelewa gani kuhusu mfumo wa kijeshi? Hivi unafikili jeshini hakuna Mainjinia(Electrical, Mechanical, Electronics, Communication, Civil, Computer etc) wenye vyeo vya Lt.Kanali, Wadaktari Wenye Vyeo vya Lt.Kanali, (Wanauchumi, Agriculture, Political Commissar)-wenye vyeo vya Lt.Kanali and above. Sasa nakwambia hivi ma ofisa wote hao wanapitia kwenye tanuri la moto kabla hawaja tunikiwa nyota, hakuna cha lele mama kuna wengine upoteza maisha yao wakiwa kwenye mafunzo/mazoezi i.e - nyota hazitolewi kwenye silver plate. Jeshini kuna division of labour kama zilivyo establishment nyingine, siyo kila mwanajeshi yupo kwenye kikosi cha Infantry. Kwa hiyo mkuu uwezi kusema mwalimu wa siasa jeshini (wakati huo) si lolote si chochote, mtu ambaye aelewi vizuri suala la vyeo JESHINI anaweza kusema lolote due to ignorance.
 
Mkuu NICHOLAS hapa tunazungumzia mambo ya usalama wa Taifa letu, nchi unazo zizungumzia hazijawahi kuvamia nchi jirani na kuondoa watawala madarakani na kuweka wanaowapenda, narudia kupindua Serikali halali au kutishia uhai wa Kiongozi mwenzake - Baba wa Taifa na Mzee Jomo Kenyatta hawakuwa in good terms lakini hatukuwahi kusoma mahali kwamba Kenyatta au Kambarage akimtishia maisha mwezake hata Iddi Amini alizungumzia mambo ya kuingia ulingoni (Ngumi) na Kambarage kama utani. Raia wengi unao wazungumzia hapa ni economic refugees hawana an hidden agenda za kujitanua kwa njia yoyote ile hata kama ni kupigana vita ili watimize malengo yao wako radhi kabisa - watu wengi tishio hili lililo dhahili wala hawalioni!!!!! Hebu niambie ni nchi gani za jirani ziliwahi kuweka/penyeza moles kwenye JWTZ, Polisi kawaida, Uhamiaji and the list goes on. Mkuu Nicholas je nchi jirani kupenyeza moles kwenye vitengo nyeti in peace time kunashiria nini?

Unless unataka niambia hujui kabisa kuna first time...hata france hawakuwahi amini kuwa senegala wangewapiga bao.Ingawa walishaona Brazil ilichomfanya Ureno kwa miaka nenda rudi, au Agentina na spain.

Jomo Kenyata ulimuona hivyo kwa sababu ya back ground values,zao Pro life huwa hawapendi fanya suicidal actions.Idd Amin hakuwa pro life na kwa taarifa yako alimaanisha alichosema...kuna mengi sana ya kushangaza n akuchekesha Idd amini alisema kw auhasilia wake, na jinsi fikra zake zilivyomuonyesha yupo sahihi.Sijui kwanini unataka danganya hapa tena....Sijui na wewe ni suicidal.

Kuna kitu suschokijua, kuna matukio fulani na values fulani chache sana zinazoweza geuza watu na kuwafanya wapende asili yao kuliko utaifa.Kwanza Dini....,pili kabila..mtu asiyeogopa ,au kulionea aiu kabila lake haswa anapojion akuwa yupo si sehemu ya watu wa taifa jipya, au kuchukia watu wanaodhalilisha watu wake.ni rahisi sana kugeuza mapenzi ama kwa uwazi ama kwa siri....unless na watu wake wamkatae.

Sijui unabisha ku achive nini hapa, economic refugee ndio wana imune na hali ziwafungazo wengine?Wazungu kila siku wanaoana na watu wa mataifa wanaotaka uchumu tuu, ulaya watu wanakimbilia uraia kule il ahawana uzalendo kule......wazenj waliopo serikali ya Bara hawana uzalendo kabisa na si bara tuu il ahata nchi kabisa,kwani wanatakamani sana Sultani awe kiongozi wao wa maisha..

Waislam wangapia wamesoma Seminary na leo wapo tayari kuongea uongo dhidi ya makanisa huku walishuhudia wafadhili na volunteers wakija na hela, wakijitolea kil akitu kuanzia majengom hadi upishi na mengine.Unadhani kwanini...
 
mleta uzi kaja kuwatisha tu mbona hazungumzii wa tanzania walioko katka jeshi la rwanda ambae wa cheo cha juu sasa ni kanali au majasusi wa tz waliopo vyuo vikuu vya rwanda kama malecturers

nachelea sema mengi ..sijui km Universities za kiraia zina urahisi hivyo wa kuchunguza jeshi..kwani hata Waliosoma na kuwa malecturer wakubwa tuu mzumbe, UDSM, etc wapo rwanda sasa hivi ni mawaziri, ingawa walikuwa ni raia tanzani tena waliohesabika kuwa ni wa Ngara, wahaya au makabila mengine ya magharibi mwa nachi hii.
 
Itabidi Tanzania ikubaliane na hali hii kwa muda mrefu sana, na ni muhimu kuwa na uongozi wa juu ulio thabiti na makini sana katika mambo ya usalama wa taifa. Kwa muda mrefu sana ilikaribisha wakimbizi wa kutoka nchi za jirani na kuwatunza kama raia wa kawaida. Vizazi vya wakimbizi hao ni raia halali wa Tanzania wenye haki sawa na raia wengine, ikiwa ni pamoja na haki ya kuwa maofisa wa jeshi, mawaziri na hata kuwa rais. Sasa hapo ndipo uthabiti wa usalama wa taifa unapoingilia. Nikichukulia mfano wa nchi ya Marekani ambako hata uraia wa kuomba pia unampa mtu haki karibu zote isipokuwa ile ya kugombea uraisi, linapokuja utoaji wa madaraka nyeti yanayowea kugusa usalama wa nchi wanakuwa makini sana, hata kwa raia ambaye babu wa babu yake alizaliwa hapo hapo Marekani. Wana kitu kinaitwa background check ambacho wanakifanya kwa makini sana ili kujua kama mtu huyo akipewa madaraka hayo hataweza kusaliti taifa. Na hata pale mtu ameshapewa madaraka, vile vile kuna kitu kingine kinaitwa security clearance, ambacho ni kikwazo kingine ambacho mtu anatakiwa akiruke ili awezeshwe kupata habari nyeti za kiuslama. Kuna wabunge na maseneta wengi ambao hawana hiyo security clearance.

Ingawa mara kwa mara kunatokea kuwapo kwa uvujaji wa siri kama huo wa Snowden, lakini inatokea kwa nadra mno- Snowden alikuwa mfanyakazi wa kima cha chini kwenye kampuni iliyokuwa imepewa tenda na serikali. Major Nidal Hasan aliyeua wenzake kule Texas alikuwa anaangaliwa kwa makini sana na hata kupandishwa kwake cheo kulifanyika baada ya kushauriana sana ndani kwa ndani kwa vile hakuonekana kuaminiwa vya kutosha. Kutokana na hali hiyo, hakuwa na access na information nyeti kiusalama, yaani hakuwa na security clearance.

Tanzania hapa tumewahi kuwa na hata mkuu wa usalama wa Taifa akiwa ni wa kutoka Rwanda, na hapo ndipo tunapotakiwa kujiangalia tena kwa makini sana kuhusu usalama wa nchi hii. Mtu hawezi kubaguliwa kutokana na wazazi wake walikotokea, lakini vile vile tuamini tena kuwa ni vigumu mtu kuwa na allegiance kwa nchi mbili sawasawa.
Sidhani kama uko right sana hapa Vipi Professor Barack Obama yeye si Mkenya tu lakini sasa ni president wa YUESIEI
 
Taarifa kama hizi ziliwahi kutolewa kwa kirefu na Mwenyekiti wa chama cha DP Mch Christopher Mtikila juu ya Kagame kupenyeza watu wake ndani ya vyombo vya ulinzi na taasisi nyeti za serikali ya Tanzania watu wakamkejeli lakini sasa naona ukweli unaanza kudhihiri wenyewe.

Jamani vyombo vyetu vyenye dhamana ya ulinzi fanyeni kazi yenu mliyoiomba na mkapewa.

tatizo serikali yetu haishauriki inasubili litokee kwanza ndio waanze kulifanyia kazi.
 
Tatizo sio Raia wa Nchi Fulani kufanyia nchi nyingine, iwe Mrwanda, Mganda Mkenya nakuendelea, tatizo ni Committment a mtu huyo kwa nchi anayo fanyia kazi, mtu huyo akitaka kutumikia mabwana wawili au mtu mwingine, basi huyo hafai. Na Tatizo watu wengi wageni au wasio na asili ya nchi husika, in general terms hawana committment, kwa USA unaweza usiwe na committment lakini kwa resource waliokuwa nazo wanaweza kukufuatilia nyendo zako kabla hujaleta madhara. na wakati wa Mwl security system yetu mara nyingi ilikuwa ahead of events.
 
Sidhani kama uko right sana hapa Vipi Professor Barack Obama yeye si Mkenya tu lakini sasa ni president wa YUESIEI
Usiongee jambo usilokuwa na uhakika nalo.

Obama alizaliwa na mwamanke wa kutokea Kansas Marekjani, aliyepewa ujazuzito na mwanaume kutokea Kenya. Obama alilelewa na babu na bibi yake wa huko Kansas ingawa alitumia muda kidogo huko Indonesia baada ya mama yake kuolewa kule. Obama si Mkenya ila ni mmarekani! Kabla hajagombea urais alikuwa State Senator wa Illionis kwa muda mrefu kabla hajawa US Senator na baadaye kuwa Rais wa Marakeni. Obama kuwa na ndugu huko Kenya, hakumfanyi awe mkenya; ana ndugu pia huko Marekani, Indonesia, Canada, na China. Hata Rais Kennedy alikuwa na ndugu zake huko Ireland!

Itakusaidia sana iwapo hutakuwa unakurupukia mambo usiyyoyajua kwani kufanya hivyo unakuwa unatangaza udhaifu wako, jambo ambalo siyo zuri
 
Hapa inatakiwa watu wawajibike sana!
Inawezekenaje akatoroka wakati jeshi letu limekuwa likimfuatilia? Nani kamtorosha na wahusika wa hilo tukio wako wapi?
Kuna maswali mengi yanayotakiwa kujibiwa!

maana yake hawa waliokua wanamfuatilia baadhi yao wana uhusiano nay ndo maana akapata data na kusepa
 
Hii kali!! Mkuu vijana wote wa lika la Mh.JK waliokuwa wanamaliza FORM SIX walikuwa wanapashwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria kwa muda wa miezi sita kabla hawaja jiunga na Vyuo Vikuu nk - kwa hiyo mambo ya ukruta na kupiga fang fang lillikuwa jambo la kawaida kabisa. Mkuu naona uamini kwamba mwalimu wa siasa anaweza kupanda cheo mpaka kufikia ngazi za juu, nashanga sana kwa nini unauliza swali hilo, je una uelewa gani kuhusu mfumo wa kijeshi? Hivi unafikili jeshini hakuna Mainjinia(Electrical, Mechanical, Electronics, Communication, Civil, Computer etc) wenye vyeo vya Lt.Kanali, Wadaktari Wenye Vyeo vya Lt.Kanali, (Wanauchumi, Agriculture, Political Commissar)-wenye vyeo vya Lt.Kanali and above. Sasa nakwambia hivi ma ofisa wote hao wanapitia kwenye tanuri la moto kabla hawaja tunikiwa nyota, hakuna cha lele mama kuna wengine upoteza maisha yao wakiwa kwenye mafunzo/mazoezi i.e - nyota hazitolewi kwenye silver plate. Jeshini kuna division of labour kama zilivyo establishment nyingine, siyo kila mwanajeshi yupo kwenye kikosi cha Infantry. Kwa hiyo mkuu uwezi kusema mwalimu wa siasa jeshini (wakati huo) si lolote si chochote, mtu ambaye aelewi vizuri suala la vyeo JESHINI anaweza kusema lolote due to ignorance.

Kweli kabisa ....role za watu kama Brigadia Moses Nnauye ambaye naye alikuwa commisar wa siasa kama JK ...ILIKUWA kubwa hasa kuwapa HAMASA NA KUWATIA MORI NA KUWACHOCHEA [UCHOCHEZI] askari pale wanapoelekea kushindwa..asikudanganye mtu ...kwenye mapigano unaweza kuwa na kila kitu...lakini ukakosa morali......ukapigwa ...hapo ndipo watu kama Nnauye au Natepe wanaojuwa kucheza na mindset za askari walipokuwa wakiitwa na kupiga domo na askari.........wakimaliza tu askari wote wanasimama na kusonga mbele hapo ndio watu wa mitulinga ambao kusema sema hawajuwi kama Musuguri,Kiaro,Chacha marwa,Walden,Lupogo,Mayunga ........wanaswaga askari na kusonga mbele
 
mwamunyange%20davis.jpg

Mkuu wa JWTZ, Meja Jenerali Davis Mwamunyange

*Adaiwa kutoweka na nyaraka nyeti
OFISA wa cheo cha juu katika Jeshi la Wananchi (JWTZ), anayeaminika kuwa na asili ya Rwanda, ametoweka katika mazingira ya kutatanisha, huku akiacha wingu la mashaka kwamba, hatua yake hiyo inaweza ikawa imeambatana na kupotea pia kwa baadhi ya taarifa muhimu za kijeshi.

Taarifa za kutoweka kwa ofisa huyo mwenye cheo cha luteni kanali, zinalihusisha tukio hilo na hatua za makachero wa JWTZ kufuatilia nyendo zake na zililifikia gazeti la MTANZANIA Jumapili kwa mara ya kwanza katikati ya wiki hii.

Vyanzo vya habari vya kuaminika vinaeleza kuwa, tayari maofisa wa JWTZ wameshaanza kufuatilia kwa karibu tukio la kutoweka kwa ofisa huyo, ambalo pia limezusha hali ya sintofahamu kwamba, huenda akawa ameondoka na nyaraka nyeti za kijeshi.

Kabla ya kutoweka ofisa huyo, ambaye nyendo zake zimekuwa katika darubini kali za makachero wa JWTZ, alikuwa akifanya kazi katika kitengo cha teknolojia ya mawasiliano ya kijeshi (IT).

Hatua ya kutoweka kwa ofisa huyo wa juu wa JWTZ anayetajwa kwa jina moja la Selumbo, imekuja siku chache tu baada ya kuibuka kwa msuguano wa kauli baina ya Ikulu ya Dar es Salaam na ile ya Kigali.

Chanzo cha msigano huo wa maneno uliogeuka na kuwa mzozo wa kidiplomasia, ni ushauri uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa Rais Paul Kagame wa kumtaka awe tayari kukaa meza moja na waasi wa kundi la FDLR wanaopigana Rwanda, kutoka mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Tayari msigano huo wa Kikwete na Kagame umeanza kutajwa na baadhi ya wadadisi wa mambo kuwa tishio kubwa la kwanza la ustawi, uimara na misingi ya mshikamano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo mataifa hayo mawili ni wanachama wake.

Siku chache baada ya ushauri huo, Kagame alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Rwanda akimkejeli Kikwete, hata kufikia hatua ya kutoa kauli zenye mwelekeo wa vitisho dhidi yake.

Kauli hizo za Kagame zilisababisha Rais Kikwete, kupitia katika hotuba yake ya mwishoni mwa Julai, kujibu mashambulizi, huku akieleza bayana kushangazwa na kushtushwa na kejeli na matusi yaliyokuwa yakielekezwa kwake.

Akitumia maneno ya kidiplomasia ambayo yametafsiriwa na baadhi wa wachambuzi wa masuala ya diplomasia na sayansi ya siasa kuwa yanabeba ujumbe mzito, Rais Kikwete alisema alikuwa amesikia yote yanayosemwa kutoka Rwanda na alikuwa hakusudii kuyapuuza.

Kauli hiyo ya Kikwete ambayo ilitanguliwa na ile aliyoitoa siku chache mkoani Kagera ya kuwataka wahamiaji haramu kuondoka nchini, ilifuatiwa na matukio ya kuondoka nchini kwa Wanyarwanda wanaokadiriwa kuzidi 5,000.

Wakati hali ikiendelea kuwa ni ya mashaka na kutoaminiana kati ya Tanzania na Rwanda, katikati ya wiki hii, gazeti dada la MTANZANIA Jumatano, lilikuwa na habari kubwa yenye kichwa cha habari kisemacho; ‘Nini kinamtia Jeuri Kagame?’ ambayo pamoja na mambo mengine, ilieleza namna watu wenye asili ya Rwanda walivyojipenyeza katika taasisi mbalimbali nyeti za umma.

Kuvuja kwa taarifa za kurejea Rwanda kwa maelfu ya wahamiaji haramu sambamba na hizi za sasa za kutoweka kwa ofisa wa juu wa JWTZ kunathibitisha kuhusu kuwapo kwa mwelekeo huo wa mambo.

Vyanzo vya habari vya gazeti hili, vinamtaja ofisa huyo kuwa ni mmoja wa makachero wenye asili ya Rwanda waliokuwa wakifanya kazi ndani ya JWTZ na ambao wanahofiwa kuwa watu wenye mawasiliano ya karibu na serikali ya Rwanda, kwa malengo ambayo bado hayajawekwa bayana.

“Ni kweli, huyo ofisa ametoweka jeshini na sijui sababu zilizo nyuma yake…hili suala la kuwa anakusanya taarifa za siri za jeshi letu na kuzipeleka Rwanda nadhani ziligunduliwa na watu wetu ambao wapo kwenye mfumo wa kijeshi,” alidokeza mmoja wa watoa taarifa wa MTANZANIA Jumapili.

Msemaji wa JWTZ, Meja Erick Komba, alipoulizwa na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu ukweli wa taarifa hizo, alishindwa kukubali au kukataa, kwa kile alichoeleza kuwa suala hilo ni zito hivyo alikuwa akipaswa kuzungumza kwanza na viongozi wake kabla ya kulitolea taarifa.

Meja Komba alieleza kuwa, wanajeshi wanaotoroka ni wengi na wapo waliofungwa kwa kosa hilo la utoro.

“Jamani suala hili ni zito, naliogopa, nyinyi hamlioni kama ni zito? Sio kwamba sipendi wananchi wapate habari, suala hili tupeni muda kwanza tulifanyie ‘analysis’, mbona wanajeshi wengi wanatoroka na hamripoti! Waliotoroka ni wengi, wangine wametorokea Rwanda na kwingine na wamefungwa.

“Ni lazima kwanza niongee na mabosi wangu ndiyo nizungumzie vizuri hili… njoo ofisini Jumatatu (Kesho),” alisema Meja Komba.

Sanjari na tukio hilo, taarifa zaidi zilizonaswa na gazeti hili zimedai kuwa sasa imebainika pasipo shaka kuhusu kuwapo kwa makachero wa Serikali ya Kigali wanaodaiwa kupandikizwa katika taasisi na idara nyeti za serikali kwa ajili ya kufanya ushushu kwa maslahi ya Rwanda.

Inadaiwa kuwa intelijensia ya JWTZ iliyo na mizizi ndani na nje ya nchi ilibaini mapema kuwapo kwa majasusi wa Kinyarwanda ndani ya mfumo wa dola na nyendo zao zimekuwa zikichunguzwa kwa muda mrefu na zilibainisha hali hiyo.
huyu mtu katoweka ama katoweshwa? maana katanzania ketu nako tunakajua wenyewe kwa kucreate scenes tata halafu kanakaa pembeni.....wewe na mimi tunabaki hoi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kagame anamiliki Command ya watu 300 Daressalaam na Tanzania yote, Battalion hii ina utaalamu wa hali ya Juu katika mauaji (assasins) je yawezekana huyo mwana JW alikuwa mmoja wao?
 
Hivi huyo Askari Wananchi wameshamfahamu na kumtambua au ndio mambo ya Jeshi hayavumi uraiani?
 
mwamunyange%20davis.jpg

Mkuu wa JWTZ, Meja Jenerali Davis Mwamunyange

*Adaiwa kutoweka na nyaraka nyeti
OFISA wa cheo cha juu katika Jeshi la Wananchi (JWTZ), anayeaminika kuwa na asili ya Rwanda, ametoweka katika mazingira ya kutatanisha, huku akiacha wingu la mashaka kwamba, hatua yake hiyo inaweza ikawa imeambatana na kupotea pia kwa baadhi ya taarifa muhimu za kijeshi.

Taarifa za kutoweka kwa ofisa huyo mwenye cheo cha luteni kanali, zinalihusisha tukio hilo na hatua za makachero wa JWTZ kufuatilia nyendo zake na zililifikia gazeti la MTANZANIA Jumapili kwa mara ya kwanza katikati ya wiki hii.

Vyanzo vya habari vya kuaminika vinaeleza kuwa, tayari maofisa wa JWTZ wameshaanza kufuatilia kwa karibu tukio la kutoweka kwa ofisa huyo, ambalo pia limezusha hali ya sintofahamu kwamba, huenda akawa ameondoka na nyaraka nyeti za kijeshi.

Kabla ya kutoweka ofisa huyo, ambaye nyendo zake zimekuwa katika darubini kali za makachero wa JWTZ, alikuwa akifanya kazi katika kitengo cha teknolojia ya mawasiliano ya kijeshi (IT).

Hatua ya kutoweka kwa ofisa huyo wa juu wa JWTZ anayetajwa kwa jina moja la Selumbo, imekuja siku chache tu baada ya kuibuka kwa msuguano wa kauli baina ya Ikulu ya Dar es Salaam na ile ya Kigali.

Chanzo cha msigano huo wa maneno uliogeuka na kuwa mzozo wa kidiplomasia, ni ushauri uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa Rais Paul Kagame wa kumtaka awe tayari kukaa meza moja na waasi wa kundi la FDLR wanaopigana Rwanda, kutoka mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Tayari msigano huo wa Kikwete na Kagame umeanza kutajwa na baadhi ya wadadisi wa mambo kuwa tishio kubwa la kwanza la ustawi, uimara na misingi ya mshikamano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo mataifa hayo mawili ni wanachama wake.

Siku chache baada ya ushauri huo, Kagame alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Rwanda akimkejeli Kikwete, hata kufikia hatua ya kutoa kauli zenye mwelekeo wa vitisho dhidi yake.

Kauli hizo za Kagame zilisababisha Rais Kikwete, kupitia katika hotuba yake ya mwishoni mwa Julai, kujibu mashambulizi, huku akieleza bayana kushangazwa na kushtushwa na kejeli na matusi yaliyokuwa yakielekezwa kwake.

Akitumia maneno ya kidiplomasia ambayo yametafsiriwa na baadhi wa wachambuzi wa masuala ya diplomasia na sayansi ya siasa kuwa yanabeba ujumbe mzito, Rais Kikwete alisema alikuwa amesikia yote yanayosemwa kutoka Rwanda na alikuwa hakusudii kuyapuuza.

Kauli hiyo ya Kikwete ambayo ilitanguliwa na ile aliyoitoa siku chache mkoani Kagera ya kuwataka wahamiaji haramu kuondoka nchini, ilifuatiwa na matukio ya kuondoka nchini kwa Wanyarwanda wanaokadiriwa kuzidi 5,000.

Wakati hali ikiendelea kuwa ni ya mashaka na kutoaminiana kati ya Tanzania na Rwanda, katikati ya wiki hii, gazeti dada la MTANZANIA Jumatano, lilikuwa na habari kubwa yenye kichwa cha habari kisemacho; &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Nini kinamtia Jeuri Kagame?' ambayo pamoja na mambo mengine, ilieleza namna watu wenye asili ya Rwanda walivyojipenyeza katika taasisi mbalimbali nyeti za umma.

Kuvuja kwa taarifa za kurejea Rwanda kwa maelfu ya wahamiaji haramu sambamba na hizi za sasa za kutoweka kwa ofisa wa juu wa JWTZ kunathibitisha kuhusu kuwapo kwa mwelekeo huo wa mambo.

Vyanzo vya habari vya gazeti hili, vinamtaja ofisa huyo kuwa ni mmoja wa makachero wenye asili ya Rwanda waliokuwa wakifanya kazi ndani ya JWTZ na ambao wanahofiwa kuwa watu wenye mawasiliano ya karibu na serikali ya Rwanda, kwa malengo ambayo bado hayajawekwa bayana.

"Ni kweli, huyo ofisa ametoweka jeshini na sijui sababu zilizo nyuma yake&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];hili suala la kuwa anakusanya taarifa za siri za jeshi letu na kuzipeleka Rwanda nadhani ziligunduliwa na watu wetu ambao wapo kwenye mfumo wa kijeshi," alidokeza mmoja wa watoa taarifa wa MTANZANIA Jumapili.

Msemaji wa JWTZ, Meja Erick Komba, alipoulizwa na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu ukweli wa taarifa hizo, alishindwa kukubali au kukataa, kwa kile alichoeleza kuwa suala hilo ni zito hivyo alikuwa akipaswa kuzungumza kwanza na viongozi wake kabla ya kulitolea taarifa.

Meja Komba alieleza kuwa, wanajeshi wanaotoroka ni wengi na wapo waliofungwa kwa kosa hilo la utoro.

"Jamani suala hili ni zito, naliogopa, nyinyi hamlioni kama ni zito? Sio kwamba sipendi wananchi wapate habari, suala hili tupeni muda kwanza tulifanyie &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];analysis', mbona wanajeshi wengi wanatoroka na hamripoti! Waliotoroka ni wengi, wangine wametorokea Rwanda na kwingine na wamefungwa.

"Ni lazima kwanza niongee na mabosi wangu ndiyo nizungumzie vizuri hili&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; njoo ofisini Jumatatu (Kesho)," alisema Meja Komba.

Sanjari na tukio hilo, taarifa zaidi zilizonaswa na gazeti hili zimedai kuwa sasa imebainika pasipo shaka kuhusu kuwapo kwa makachero wa Serikali ya Kigali wanaodaiwa kupandikizwa katika taasisi na idara nyeti za serikali kwa ajili ya kufanya ushushu kwa maslahi ya Rwanda.

Inadaiwa kuwa intelijensia ya JWTZ iliyo na mizizi ndani na nje ya nchi ilibaini mapema kuwapo kwa majasusi wa Kinyarwanda ndani ya mfumo wa dola na nyendo zao zimekuwa zikichunguzwa kwa muda mrefu na zilibainisha hali hiyo.
Kwahiyo na huu ulikuwaga uzushi.....!!
shikamoni wabongo
 
Hii Habari ingekuwa ni Leo hii gazeti hili lingefungiwa milele!
 
Back
Top Bottom