Shikamoo, nakupa heshima kwa umri ulionao.
Leo nimewiwa kukupa salamu ukiwa kama mkongwe katika tasnia ya Muziki ambayo bado unatamba hadi sasa, nasema shikamoo kaka.
Kaka Kiba, kwa umri ulionao sasa wa miaka 42 ni dhahiri umeona na kujifunza mengi katika Muziki. Wenzako uliokuwa nao wakati wako kama Mzee Selemani Msindi (Simba wa Moro), Mzee Joseph Mbilinyi (Sugu), Mzee Joseph Haule (Professor J) Mzee Sogy Dogy, Mzee Suma Lee, Mzee Solo Thang, Mzee Dully Sykes na wengineo.
Hao wenzako wote kwa sasa hawako active katika muziki lakini wewe bado unadunda, hongera sana.
Ujumbe kwako kaka ni kwamba, unajisahau kuwa wewe ni ligendari na kujiingiza kutunga nyimbo za kitoto/vijana wadogo ambazo zimekosa ujumbe maksusi na kukusadifu na umri na ukongwe ulionao.
Wimbo wako wa Mwana Dar es salaam ulikuwa kiigizo chema sana. Lakini huu wimbo hauna ujumbe kwa jamii. Wimbo huu utatamba kwa muda mfupi na kupotea kabisa kwani hauna hisia na kukidhi vigezo vya ligendari.
Nakushauri uache tungo za namna hiyo na ufyatua vitu vya maana kama Mwana.
Nimeambiwa kuwa kuna baadhi ya wanasiasa ambao taswira zao siku za karibuni zimeingia madoa ndio wanaokushabikia. Najua ni haki yao, lakini wasitumie mgongo wako kujisafisha na maji machafu.
Ni hayo tu kaka, shikamoo.