Official Video: Seduce Me by Ali Kiba

Official Video: Seduce Me by Ali Kiba

unafiki shingapi kwani apo kila mtu anatafuta mashabiki na kufufuka kujulikana mjini akili kiki na kugawana mashabiki mchezo
 
Nikiwa kama miongoni mwa watu wanaofuatilia mziki wa kizazi kipya nimeona itakuwa sio mzuka kutotia tia neno katika wimbo ambao ni homa ya majiji makubwa yote duniani wanaojua mziki mzuri..kwa tafiti yangu ya siku chache nimegundua wimbo huu wa Ally una maajabu kumi kama ifuatavyo:-

1.Kautoa bila interview wala kuipeleka redioni lakini ndani ya dakika chache maDJ wote wa redio wanayo

2.Imegonga view million ndani ya masaa 38

3.Kafunika pengo la NEYO katika verse ya mwisho kwa verse kali inayofanya ajisifie NEYO kutakuwepo kwani angemharibia wimbo

4.Ni wimbo uliosababisha mpinzani wake kimziki apanic na kutoa wimbo si wimbo comedy si comedy akiwa na mawigi usiku wa manane...for the first time ukiona huo wimbo unaweza ukajua Eric Omond katoa kichekesho kumbe ni wimbo

5.wimbo huu umefanya kipigo cha arsenal,draw ya yanga na ushindi mnono wa Simba S.C isiwe habari ya kuzungumziwa kwa wanamichezo

6.Wimbo huu umefanya tukio la mlipuko ofisi za IMMA ADVOCATES iwe ni habari ya kawaida wakati ni tukio kubwa

7.Imeunganisha maadui wengi katika mitandao ya kijamii

8.imezima story za hamisa mobeto kuzalishwa na Nasib

9.huu wimbo imefanya WCB waingie jikoni kutengeneza booster iizime (soon mtasikia diamond kamuoa zari au diamond kamkubali mtoto aliyezaa na hamisa mobeto)...

10.huu wimbo umefanya niikumbuke password yangu ya kuingilia humu JAMII FORUMS
 
Dah, kweli nimeamini wakinadada wengi wanamchukia Diamond, yaani wimbo wa Kiba kila mtu anajifanya mchambuzi na mtoa statistic za kila aina, sasa ukiusikiliza wimbo wenyewe huoni cha maana, sio mashairi wala video
 
Namba 5 umetisha sana mkuu. Mwenyewe mnazi sana wa Arsenal. Baada ya filimbi ya mwisho niliplay ngoma hii, na nilikuwa nimeshasahau kabisa kama jana vijana wa mzee Wenger walidhalilishwa pale Anfield. Hakika Seduce Me inamaajabu!!
 
Back
Top Bottom