KUHUSU "SEDUCE ME"
☆ Wimbo umetulia,unakupa mood ya kurelax...hakuna makelele na upayukaji wa kinaijeria
☆ Production nzuri hasa eneo la sound mixing
☆ Video nzuri, simpicity, originality, colour toning....clear resolution....less boobs, nudity, marangi rangi na ming'aoming'ao isiyo ya lazima
☆ Wimbo una mada inayoeleweka.
☆ Probable critisism kwa wimbo huu ni kwenda tofauti na upepo uvumao kwa sasa...uandishi wa kinaija..beat ya kinaija...na slow tempo...watu sasa wanapenda nyimbo zenye kasi ya singeli or something close enough to that...ndiyo maana wengi wanawaza itakua vipi Kiba akifanya show CCM Kirumba ataamsha mashabiki na wimbo huu? Mziki ni vibes tu ndiyo maana haishangazi kuona R. Kelly anaamsha mashabiki kwa kwaya yake ya "Storm Is Over" au The Passengers na "Let It Go".
☆ Athari za team zinafanya kusiwepo na uhalisia wa judgement za kazi za sanaa hasa kwa Daimond na Ali Kiba, kwenye uwepo wa team basi hutokea kitu kinaitwa ligi...na lengo la ligi ni team flani kua mshindi..sasa nani awe looser? Hapo ndipo kazi ilipo