OCD adundwa na mgombea Ubunge CCM Polisi wasema ni "jambo la kawaida"

Katika hatua nyingine, mgombea huyo wa CCM alifika kituo cha polisi na kusababisha sokomoko baada ya kumshambulia kwa mateke na kumuangusha chini mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Maswa (OCD), Peter Ndunguru akimtuhumu kuwa wamemwachia Shibuda.

Akizungumza kwa njia ya simu, OCD Ndunguru alisema mgombea huyo wa CCM aliambatana na viongozi wa chama hicho na kuuliza alipo Shibuda, na walipojibiwa kuwa yupo rumande mgombea huyo alimrukia OCD huyo na kuanza kumshambulia kwa mateke kiasi cha kumuangusha chini.

“Alinirukia na kunipiga,” alieleza OCD.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga amethibitisha tukio hilo, akisema kuwa kulitokea kutokuelewana kati ya afisa wake na mgombea huyo, lakini akadai kuwa hilo ni jambo binafsi ambalo analiacha mikononi mwa OCD mwenyewe.

“Suala la Kisena na OCD ni jambo la kawaida kiutendaji na wala siwezi kulizungumzia... kwa sasa hapa ninashughulika na suala zito la mauaji," alisema kamanda huyo wa Shinyanga.

"Suala hilo lilitokana na kutoelewana kati yao... kama OCD anaweza kumfungulia mashitaka ni yeye lakini sisi hatuna haja naye. Lakini nadhani tutawashauri wayamalize kwa kuwa ni ya kawaida kiutendaji.”

Source;Gazeti la Mwananchi



HAPO RED - Ina maana POLISI hawana haki ya kulindwa wakiwa KAZINI??? Kesho ya Tanzania iko wapi? Ujasiri wa Jeshi la Polisi uko wapi? Mmmmmmmmmmmmmm.....
 
This is too much OCD alikuwa na crown I guess iyo ni sawa na kuipiga Jamhuri.
Au CCM wako above the law
 
IGP Mwema umeisikia hiyo?Ofisa wako anabondwa na kada wa CCM halafu RPC anachekelea, kesho akibondwa na kada wa upinzani tunataka tusikie the same coment vinginevyo tutathibitisha kuwa Polisi ni kitengo cha CCM chenye jukumu la kudhibiti upinzani
 
"Suala hilo lilitokana na kutoelewana kati yao... kama OCD anaweza kumfungulia mashitaka ni yeye lakini sisi hatuna haja naye. Lakini nadhani tutawashauri wayamalize kwa kuwa ni ya kawaida kiutendaji."

dah,hivi angekua shibuda hapo ingekua vipi?aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah
 
"Kwa maelezo ya awali ni kuwa inaelezwa wafuasi hao wa CCM walipofika eneo hilo ambalo ni mita chache toka eneo ambalo Shibuda alikuwa akifanya mkutano, waliteremka kwa ajili ya kukojoa na gari la Chadema lilisimama na wafuasi hao wakaanza kushambuliana,"

Sasa shibuda anahusika vipi hapa?
 
Serikali iliyoshindwa!

By the way : Who is Rulling this Country!?

Are we going by the rules of "Animal Farm"?
 
Tangu niwe na akili timamu sijawahi kusikia wala kuona mtu anapigwa katika kituo chake cha kazi wakati akiwa anatimiza wajibu wa kazi yake na akaachwa huru, achilia mbali polisi. Kumpiga polisi ni kumzuia kutenda kazi yake, kumpiga mtu yeyote ni kumdhalilisha na ni jinai. Hapa kuna jinai mbili ambazo zimeachwa bila kuchukuliwa hatua zinazostahili.

Kama kweli polisi wanafanya kazi yao kwa haki basi walistahili kumweka ndani Kisenha pia, kama waliona kuna umuhimu wa kumweka ndani Shibuda.

Sioni namna gani Shibuda anaweza kuhusika bila Kisena kuhusika kama Shibuda hakuwatuma watu wale.
 
Kabla ya tarehe 31 nanunua shati la kijani, then naenda kituo cha polisi kutest zari :smash:
 
Hiki chama cha mafisadi kishapoteza mwelekeo, jukumu letu ni moja tu, kuipoteza thithiemu nje ya ramani ya siasa za bongo!
 
Suala la Kisena na OCD ni jambo la kawaida kiutendaji na wala siwezi kulizungumzia[/B]... kwa sasa hapa ninashughulika na suala zito la mauaji," alisema kamanda huyo wa Shinyanga.


Hahahhaha
jamani hii ni the comedy au IQ yanguya kuelewa nachosoma imeshuka . Si angektaa tu ku comment kuliko kuongea upupu.Yaani kama RPC anatoa majibu ya hivyo sasa hao walio chini yao ndo ..........

hahahhahaha Kama ndo hivi inawezekana hata huyo OCD aliyepigwa mtama naye majibu yake nikama haya.
 
Mijitu mingine inakera kweli, yaani mtu kumdhalilisha mtumishi wa Serikali akiwa kazini jitu linaibuka na kusema ni jambo la kawaida..

Ok, tutaona!
 
Jinsi hili nilivyolisoma hii thread nina ona kuwa huyu mgobea wa CCM ni mtu wa shari na kama anapenda sana uchochezi, sina shaka yeye kutumia tabia hiyo mbaya kwa namna moja katika vurugu iliosababisha kutolewa roho ya maskini dereva wao asiyejua analolifanya, Mungu ampumzishe kwa amani
 
Ubabaishaji huu unatokana na madaraka makubwa ya rais. Viongozi wa juu wa jeshi la polisi kama wangekuwa hawateuliwi na rais kwa maana ya institution hawangelazimika kuwa wanafiki kama tunavyoona. kAMA SI UNAFIKI kwa tukio la mauaji tungeona pia wanachama/VIONGOZI CCM nao wako ndani, lakini ukweli ni kwamba kufanya hivyo huenda kungewachukiza watu Serikalini/CCM. Kama hilo halitoshi OCD anapigwa osifini kwake RPC anasema ni mambo ya kawaida kwa kuogopa kuwaudhi waajiri wake ambao ni Serikali ya CCM. kweli toka lini kupigana hadharani limekuwa jambo la kwaida kwapolisi? Au tuseme ni swala la incompetence maana huu mtindo wa kupewa vyeo na kufanya kazi kwa mazoea. Lakini siamini hivyo na nakubaliana na mwanajukwaa aliyesema kama angekuwa mwanachama chama kingine tofauti na chama tawala huenda angefunguliwa kesi na press conference kuitishwa. Kazi kweli kweli!!
 
Huyo Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM anapaswa kukamatwa mara moja na kufunguliwa mashitaka na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Jakaya alimfukuza kazi Mkuu wa wilaya aliyewapiga bakora waalimu wa shule za msingi kwa ajili ya uzembe uliosababisha wanafunzi wenegi kufeli masomo. Jakaya alisema kwamba Mkuu wa wilaya amevuka mpaka katika kufanya hivyo.
Sasa ninategemea Jakaya ama Makamba watamchukulia hatua huyu muhusika bila kuona haya wala kumung'unya maneno. Na kama watakaa kimya basi wajue kwamba vichapo kwa Ma-OCD vitaendelea nchi nzima toka kwa wanachama wa vyama vyote. Usipoziba ufa utajenga ukuta.
 
Mjumbe.jpg

Pichani:polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwa wamemshikilia Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Kata ya Nyalikungu Wilaya ya Maswa, mkoani Shinyanga, Abel Jombo, kwa tuhuma za kufanya vurugu zilizotokea kati ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizosababisha kifo cha mtu mmoja. source:Nipashe www.ippmedia.com

Kama kada huyu wa CCM anaweza kuwekwa chini ya ulinzi na platoon nzima ya Polisi, inashindikana vipi mgombea wa ubunge wa CCM kwa tiketi ya CCM Bw. Robert Kisena wa jimboni Maswa asikamatwe kwa kufanya vurugu ktk kituo cha Polisi na pia kwa kumshambulia Afisa wa Polisi OCD Ndunguru, tena ndani ya kituo cha Polisi?!

Mimi naamini hii platoon nzima ya Polisi haijafurahishwa na Ofisa wao kudhalilishwa na kupigwa na wanakila sababu ya kwenda kumkamata Mgombea wa Ubunge wa CCM Bw. Robert Kisena ili afunguliwe mashitaka na kuleta hali ya utawala bora kwa kufuata sheria ktk Tanzania.

Na ikumbukwe kuwa RPC mkoa na IGP wa Polisi mna dhamana kubwa ya kuhakikisha utawala wa sheria unafanyika bila kujali kama mtuhumiwa ni wa chama tawala au upinzani au kigogo Yusuf Makamba alikuwapo mkoani Shinyanga na kujaribu kuingilia sakata hilo la Mgombea wao Robert Kisena kumshambulia OCD Ndunguru.
 
Nitawashangaa polisi pamoja na kudhalilishwa huku;bado wakubali kutumiwa na sisiemu kusaidia wizi wa kura.
 
Back
Top Bottom