OCD adundwa na mgombea Ubunge CCM Polisi wasema ni "jambo la kawaida"

Unajua hapa tatizo ni kwamba Simon mgembea wa CCM alipita kwa pesa na waliokula hela zimeisha ndio wamegundua kwamba mambo
ya zamani kwamba atapita tuu hakuna.
Sio chagula la watu pale huyu bwana namjua sana ni Fisadi kuliko ujuavyo. Ana miaka mitatu toka aondoke huko alirudi sasabu kuna utamu
ameupata sehemu na hivyo ameingia kenye ubunge kibiashara ila ni tapeli suiambiwe na lugha laini ya kinywaranda.
Ni mnywaranda baba na mama msukuma.
Na miradi mingi ambayo inaenda kitapeli na pia aliwarussha Ushirika shirecu ni kweli na aliwarusha wananchi pamba ni kweli na pia
alipojenga kiwanda chanke alirusha ardhi ni kweli. Ana lugha nzuri kama vile nyoka ila kukumeza kwake si dakika.
Wananchi tukae chonjo na matumizi ya hea ya uchagzi kuliko kujuta the whoe life 5yrs.
Sasa ana frustration maana jimbo limeponyoka na hela kibao amepoteza. kumbuka ni mfanya biashara amesha realize loss tofauti
na mwanasiasa anainvest reasonable.
 
Imeandikwa ukipigwa shavu la kulia geuza na la kushoto. Aliyepigwa hajalalamika sasa sisi tunalalama kwa siye ndio tuliosikia maumivu ya kugaragazwa sakafuni. After all kama amepewa mshiko sawa na mshahara wake wa mwaka ili anyamaze we unafikiri ataongea na ukizingatia wakati anapata kibano mkewe hakuwepo maana angekuwepo si ajabu angechukua hata silaha!!
 
Unategemea nini ndugu yangu toka kwa majeshi ya thithiem zaidi ya kuonyesha jinsi yalivyojaa uoga wa kufuata haki dhidi ya wagombea wa thithiem?

VYOMBO VYA USALAMA SI HURU MUDA WOTE WAMEBEBA MBELEKO YA KUWABEBA SISIEM KWA GHARAMA NA AIBU ZA KUTISHA HATA IKIBIDI KUVUNJA SHERIA, OCD KUSHUSHWA MTAMA NA MGOMBEA PENGINE HATA CROWN ILIDONDOKA CHINI, BADO BILA AIBU RPC ANASEMA NI JAMBO LA KAWAIDA MBONA RAIA ASIPOTII AMRI YA ASKARI (POLISI) UNAWAJIBISHWA? Tuelewesheni wanataaluma wa sheria, nadhani huu ni uchakachuaji na udhalilishaji wa taaluma Ama kweli yetu masikio/macho Hawa maafande ni waumini wazuri wa sheria lakini matendo yao yanaashiria huenda chombo hiki cha umma kinabinafsishwa. Maana kwa wafuasi wa vyama na raia wengine offer hizi hazitolewi, ama hawajichanganyi kiasi hiki Tumuombe Bwana wa mavuno aguse nyoyo zetu tuuone ukombozi wa kweli hapo 31/10/2010:amen:
 
Huyo OCD kapewa kipozea jasho cha ngwara. Its too sad, hiyo yote ni taifa kujengwa katika misingi ya uoga, kunyenyekea kila kitu hata pale ambapo watu wanapaswa kuona na kuokoa utu wanaogopa. Leo hii wagombea wengi ndani ya ccm ndo wenye hela, ndo majambazi wengi, ndo kila aina ya roho mbaya zinazosikika mtaani ndo wanaogombea uongozi, hapo utegemee nini jamani?
Unapomchagua kiongozi ambaye yuko tayari kuua kwa ajili ya hela za ubunge au udiwani tegemea maumivu tu hakuna lingine. Ndio hicho kinachoonekana saizi.
 
Katika hatua nyingine, mgombea huyo wa CCM alifika kituo cha polisi na kusababisha sokomoko baada ya kumshambulia kwa mateke na kumuangusha chini mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Maswa (OCD), Peter Ndunguru akimtuhumu kuwa wamemwachia Shibuda.

Akizungumza kwa njia ya simu, OCD Ndunguru alisema mgombea huyo wa CCM aliambatana na viongozi wa chama hicho na kuuliza alipo Shibuda, na walipojibiwa kuwa yupo rumande mgombea huyo alimrukia OCD huyo na kuanza kumshambulia kwa mateke kiasi cha kumuangusha chini.

“Alinirukia na kunipiga,” alieleza OCD.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga amethibitisha tukio hilo, akisema kuwa kulitokea kutokuelewana kati ya afisa wake na mgombea huyo, lakini akadai kuwa hilo ni jambo binafsi ambalo analiacha mikononi mwa OCD mwenyewe.

“Suala la Kisena na OCD ni jambo la kawaida kiutendaji na wala siwezi kulizungumzia... kwa sasa hapa ninashughulika na suala zito la mauaji," alisema kamanda huyo wa Shinyanga.

"Suala hilo lilitokana na kutoelewana kati yao... kama OCD anaweza kumfungulia mashitaka ni yeye lakini sisi hatuna haja naye. Lakini nadhani tutawashauri wayamalize kwa kuwa ni ya kawaida kiutendaji.”

Source;Gazeti la Mwananchi

Thats how low our law enfocement team can go... kupiga ni jambo la kawaida kama wewe ni mwanaCCM, lakini kupiga inadeserve mada case kama wewe ni mpinzani
 
Sijaona tatizo hapa! licha ya blah blah nyingi za wafa maji

Eeh! hakuna tatizo hapo? kweli sisem ufisadi umewalevya mpaka mnafikiri mko juu ya sheria. OCD kapigwa, kadhalilishwa, bado huoni kuna tatizo la kimfumo na rushwa? raia unapata wapi kiburi cha kumshambulia OCD kituoni? oooh, my God, kweli tusipochukua hatua za haraka za kuwang'oa mafisadi (CCM) wataanza kutembea kwenye vichwa vyetu.
 
thithiem wanaumwa matumbo ya kuhara sasa wanahaha kutafuta pa kuhara hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaa chadema tunasonga mbele
 
Katika hatua nyingine, mgombea huyo wa CCM alifika kituo cha polisi na kusababisha sokomoko baada ya kumshambulia kwa mateke na kumuangusha chini mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Maswa (OCD), Peter Ndunguru akimtuhumu kuwa wamemwachia Shibuda.

Akizungumza kwa njia ya simu, OCD Ndunguru alisema mgombea huyo wa CCM aliambatana na viongozi wa chama hicho na kuuliza alipo Shibuda, na walipojibiwa kuwa yupo rumande mgombea huyo alimrukia OCD huyo na kuanza kumshambulia kwa mateke kiasi cha kumuangusha chini.

“Alinirukia na kunipiga,” alieleza OCD.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga amethibitisha tukio hilo, akisema kuwa kulitokea kutokuelewana kati ya afisa wake na mgombea huyo, lakini akadai kuwa hilo ni jambo binafsi ambalo analiacha mikononi mwa OCD mwenyewe.

“Suala la Kisena na OCD ni jambo la kawaida kiutendaji na wala siwezi kulizungumzia... kwa sasa hapa ninashughulika na suala zito la mauaji," alisema kamanda huyo wa Shinyanga.

"Suala hilo lilitokana na kutoelewana kati yao... kama OCD anaweza kumfungulia mashitaka ni yeye lakini sisi hatuna haja naye. Lakini nadhani tutawashauri wayamalize kwa kuwa ni ya kawaida kiutendaji.”

Source;Gazeti la Mwananchi

duh hapo nimepata shida kuelewa yani kumpiga OCD ni jambo la kawaida??
 
Sijaona tatizo hapa! licha ya blah blah nyingi za wafa maji

Hata mimi sijaona tatizo lolote hapo..hawa pipoz pawa watanyamaza muda si mrefu, tena jamani tunawakaribisha kwenye sherehe za kumuapisha JK pale uwanja wa taifa..mje kwa wingi eeh
 
Hii watu husema...uki staajabu ya Mussa utaona ya Firauni!!! mwaka huu......
 
Kama hili litapita kimya kimya hii Tanzania ya Kikwete itakuwa ya aina yake!
 
Kama OCD anapigwa ofisini kwake na mbele ya askari wa chini yake, hana hadhi tena kuendelea na wadhifa huo! On the other hand, inawezekana hata askari wa chini yake wamemchoka ndiyo maana hakupata msaada wowote toka kwa askari wake wa chini.
 
Hii kali sana,kapigwa afisa wa ngazi za juu wa polisi akiwa tena na mavazi aliyopewa kwa heshima ya kulinda katiba ya jamhuri ya Muungano wa TZ tena kwenye kituo chake cha kazi lkn RPC leo hii anasema hilo ni tendo la"kawaida"?

Dr Slaa zungumzia leo hili suala kwenye mkutano wako,polisi sasa wanajidhihirisha wazi kabisa kuwa wao ni CCM-B;kisheria POLISI walitakiwa wamshtaki mara moja Mgombea ubunge huyu kupitia CCM kwa kulidhalilisha Jeshi na wala sio kama kamanda Siasi anavyojaribu kupindisha sheria eti ni suala lao binafsi!

Lingekuwa suala lao binafsi kama tu angempiga mbali na kituo cha polisi tena akiwa OCD huyu hajavaa nguo za kikazi;hata kama angekuwa kwake au popote pale lkn kavaa nguo zake za kazi bado jamaa huyu angeweza kushtakiwa kwa kesi ya kulidhalilisha jeshi la Polisi!

RPC Zoba hilo yaani linaona ni jambo la kawaida afande kupigwa ngwala akiwa na nguo za heshima??? Hii ni ya kufungia mwaka imewahishwa tu ilipaswa isubiri hadi Disemba!! Wananchi na sisi siku ya uchaguzi wakileta ujinga tuwapige ngwala kumbe ni jambo linalokubalika!! JK Mvue madaraka huyu zoba!!
 
Hii tabia ndiyo inasababisha wananchi kuchukulia sheria mikononi. Mwana CCM akikosea anatetewa na vyombo vya dola, lakini wa vyama vingine wanashughulikiwa. Hii inaudhi, inaumiza na inasababisha wananchi kukerwa. Uleaji huu wa vyombo vya dola ndo utakuwa mwanzo wa kumwagika damu (Sorry tayari ilishamwagika).

I don't care huyo aliyepoteza maisha yake anatoka chama gani, lakini hakupaswa kupoteza maisha yake kwa sababu tu ya kampeni. Vyombo vya dola mnapokuwa na upendeleo wa chama fulani hayo ndiyo yanatokea.
Tuwe makini katika kulinda sheria za nchi.
 
Nitafurahi siku CCM wakimtandika huyo RPC wa Shy maana ni kawaida. Natumaini Slaa atafuta ujinga huu wa serikali kuwa kama Mungu
 
Back
Top Bottom