OCD adundwa na mgombea Ubunge CCM Polisi wasema ni "jambo la kawaida"

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,813
11,123
Katika hatua nyingine, mgombea huyo wa CCM alifika kituo cha polisi na kusababisha sokomoko baada ya kumshambulia kwa mateke na kumuangusha chini mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Maswa (OCD), Peter Ndunguru akimtuhumu kuwa wamemwachia Shibuda.

Akizungumza kwa njia ya simu, OCD Ndunguru alisema mgombea huyo wa CCM aliambatana na viongozi wa chama hicho na kuuliza alipo Shibuda, na walipojibiwa kuwa yupo rumande mgombea huyo alimrukia OCD huyo na kuanza kumshambulia kwa mateke kiasi cha kumuangusha chini.

“Alinirukia na kunipiga,” alieleza OCD.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga amethibitisha tukio hilo, akisema kuwa kulitokea kutokuelewana kati ya afisa wake na mgombea huyo, lakini akadai kuwa hilo ni jambo binafsi ambalo analiacha mikononi mwa OCD mwenyewe.

“Suala la Kisena na OCD ni jambo la kawaida kiutendaji na wala siwezi kulizungumzia... kwa sasa hapa ninashughulika na suala zito la mauaji," alisema kamanda huyo wa Shinyanga.

"Suala hilo lilitokana na kutoelewana kati yao... kama OCD anaweza kumfungulia mashitaka ni yeye lakini sisi hatuna haja naye. Lakini nadhani tutawashauri wayamalize kwa kuwa ni ya kawaida kiutendaji.”

Source;Gazeti la Mwananchi
 
Nipashe

Kamanda huyo alisema kuwa baada ya wafuasi wa CCM kupata taarifa hizo akiwemo mgombea, Kisena, walikwenda hadi kituo cha polisi mjini Maswa na kukutana na OCD, lakini katika mazungumzo yao kulitokea kutokuelewana na vurugu zingine kutokea kituoni hapo.
Katika vurugu hizo OCD, Peter Ndunguru, alipigwa ngwara na mgombea wa CCM na mgombea huyo kutoweka.
Hata hivyo, Kamanda Siasi alipoulizwa ni kwa nini mgombea wa CCM (Kisena), hajakamatwa wakati Shibuda alikamatwa, alikataa kuzungumza.
"Inategemeana na mazingira ya vurugu hizo ndiyo maana tumemshikilia Shibuda na watu wengine 12…vurugu hizo za kituoni ni baada ya kuhojiana maswali ya kiutendaji na kutokuelewana na OCD na hivyo kusababisha vurugu," alisema.
"Kuhusu Robert (Kisena), hilo tuachie sisi, ikibidi tutamkamata kama kuna ukweli, tutachukua hatua…mbona mnang'ang'ania," alisema.
Kamanda huyo akionyesha kukerwa na maswali zaidi ya waandishi wa habari alisema: "Nasema juu ya Robert (Kisena) hilo tuachie sisi..nasema wewe tuachie," aliongeza.
 
next time afwande atachambwa "doRe" harafu riafande ritasema ni utaratibu katika geshi ra PORISI kada wa sisiem kuchovya PORISI....Aroooo...
 
Hii kali sana,kapigwa afisa wa ngazi za juu wa polisi akiwa tena na mavazi aliyopewa kwa heshima ya kulinda katiba ya jamhuri ya Muungano wa TZ tena kwenye kituo chake cha kazi lkn RPC leo hii anasema hilo ni tendo la"kawaida"?

Dr Slaa zungumzia leo hili suala kwenye mkutano wako,polisi sasa wanajidhihirisha wazi kabisa kuwa wao ni CCM-B;kisheria POLISI walitakiwa wamshtaki mara moja Mgombea ubunge huyu kupitia CCM kwa kulidhalilisha Jeshi na wala sio kama kamanda Siasi anavyojaribu kupindisha sheria eti ni suala lao binafsi!

Lingekuwa suala lao binafsi kama tu angempiga mbali na kituo cha polisi tena akiwa OCD huyu hajavaa nguo za kikazi;hata kama angekuwa kwake au popote pale lkn kavaa nguo zake za kazi bado jamaa huyu angeweza kushtakiwa kwa kesi ya kulidhalilisha jeshi la Polisi!
 
Shame on you.......aibu kwa jeshi la polisi nimeamini maneno ya afisa wa polisi kamanda........................aliyesema jeshi la polisi limepoteza hadhi
 
Huyo RPC kalidhalilisha Jesho na Crown la Polisi.

Lakini Yana Mwisho yote haya!

People's Power
 
nasubiri mmachinga mmoja afyatuke na kumtia kabila Inspekta fulani!!!! jamani hata kama ndio kubeba kweli ndio kubebwa namna hii?
 
Ingekua vp ka raia wa kawaida mwananchama wa pipoz, angemrukia vichwa uyo OCD? Cpat picha, kweli RPC popompo!!!!! Shame on u RPC. Ningekua mi OCD ningeacha kazi leo leo nikajiunga na CHADEMA.
 
katika hatua nyingine, mgombea huyo wa ccm alifika kituo cha polisi na kusababisha sokomoko baada ya kumshambulia kwa mateke na kumuangusha chini mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya maswa (ocd), peter ndunguru akimtuhumu kuwa wamemwachia shibuda.

Akizungumza kwa njia ya simu, ocd ndunguru alisema mgombea huyo wa ccm aliambatana na viongozi wa chama hicho na kuuliza alipo shibuda, na walipojibiwa kuwa yupo rumande mgombea huyo alimrukia ocd huyo na kuanza kumshambulia kwa mateke kiasi cha kumuangusha chini.

"alinirukia na kunipiga," alieleza ocd.

kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga amethibitisha tukio hilo, akisema kuwa kulitokea kutokuelewana kati ya afisa wake na mgombea huyo, lakini akadai kuwa hilo ni jambo binafsi ambalo analiacha mikononi mwa ocd mwenyewe.

"suala la kisena na ocd ni jambo la kawaida kiutendaji na wala siwezi kulizungumzia... Kwa sasa hapa ninashughulika na suala zito la mauaji," alisema kamanda huyo wa shinyanga.

"suala hilo lilitokana na kutoelewana kati yao... kama ocd anaweza kumfungulia mashitaka ni yeye lakini sisi hatuna haja naye. lakini nadhani tutawashauri wayamalize kwa kuwa ni ya kawaida kiutendaji."

source;gazeti la mwananchi

kwahiyo?
 
No comment. kwa kweli tulipofika inahuzunisha kwelikweli. Tanzania ni zaidi uijuavyo
 
Katika hatua nyingine, mgombea huyo wa CCM alifika kituo cha polisi na kusababisha sokomoko baada ya kumshambulia kwa mateke na kumuangusha chini mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Maswa (OCD), Peter Ndunguru akimtuhumu kuwa wamemwachia Shibuda.

Akizungumza kwa njia ya simu, OCD Ndunguru alisema mgombea huyo wa CCM aliambatana na viongozi wa chama hicho na kuuliza alipo Shibuda, na walipojibiwa kuwa yupo rumande mgombea huyo alimrukia OCD huyo na kuanza kumshambulia kwa mateke kiasi cha kumuangusha chini.

"Alinirukia na kunipiga," alieleza OCD.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga amethibitisha tukio hilo, akisema kuwa kulitokea kutokuelewana kati ya afisa wake na mgombea huyo, lakini akadai kuwa hilo ni jambo binafsi ambalo analiacha mikononi mwa OCD mwenyewe.

"Suala la Kisena na OCD ni jambo la kawaida kiutendaji na wala siwezi kulizungumzia... kwa sasa hapa ninashughulika na suala zito la mauaji," alisema kamanda huyo wa Shinyanga.

"Suala hilo lilitokana na kutoelewana kati yao... kama OCD anaweza kumfungulia mashitaka ni yeye lakini sisi hatuna haja naye. Lakini nadhani tutawashauri wayamalize kwa kuwa ni ya kawaida kiutendaji."

Source;Gazeti la Mwananchi

IGP MWEMA ATANISHANGAZA KAMA ATAACHIA MTU AMBAYE AMEDHALILISHA kAMANDA WETU MBELE YA kITUO CHA POLISI ,MBELE YA UMMA WA WATANZANIA,KUMDHALILISHA ASKARI MKUU WA KITUO ALIYE VAA KOFIA YENYE NEMBO YETU ETI ALIYEMPIGA HAKAMATWI KUHOJIWA KWA SABABU YUSUPHU MAKAMBA NA JAKAYA KIKWETE WAMEEAGIZA INA MAANA YUSUPHU MAKAMBA NA KIKWETE WAKO JUU YA SHERIA,KWELI NCHI HII IMEHARIBIKA KWA KWELI TUNAHITAJI MABADILIKO YA UONGOZI HUU NI USHENZI AMBAO HAUJAWAHI KUTOKEA TOKA NIZALIWE
ASKARI WADOGO WA KITUONI HAPO NA VITUO VINGINE WATAMUHESHIMU KWELI MTU KIONGOZI ANAPIGWA NGWALA MBELE YAO ,HUYO RPC AFUTWE KAZI

SHIBUDA HAKUWEKO KWENYE TUKIO LAKINI WAMEMUWEKA NDANI KWA KOSA LIPI
HAWA ZAMA ZAO ZIMEISHA BADO KITAMBO KIDOGO WATALI A NA KUSAGA
JAKAYA KIKWETE NCHI IMEMUSHINDA
TBC WAMEONYESHA UPANDE MMOJA WA HADITHI HAWAKUULIZA WANACHADEMA KITU GANI KILIJIRI WHAT SORT OF NOSENSE TIDO MHANDO KAISHIWA KABISA UPUUZI MTUPU NA UBAKAJI WA DEMOKRASIA TIDO YOUR DAYS ARE NUMBERED
 
Shame on you.......aibu kwa jeshi la polisi nimeamini maneno ya afisa wa polisi kamanda........................aliyesema jeshi la polisi limepoteza hadhi

Unategemea nini ndugu yangu toka kwa majeshi ya thithiem zaidi ya kuonyesha jinsi yalivyojaa uoga wa kufuata haki dhidi ya wagombea wa thithiem?
 
Suala la kumpiga KAMANDA akiwa kwenye uniform ya kazi ni kosa kubwa, na ni sawa na kuisigina katiba!...Polisi kwenye uniform anabeba dhamana ya serikali, na hivyo kumvamia na kumpiga ni dharau moja kwa moja kwa serikali...Lakini ajabu huyo kamanda wa mkoa anasema kuwa ni issue ya kawaida!
Ngoja tuandike historia hii, ili ije kuwa kama precedence huko mbele ya safari, wasije kukana baadaye!
 
Inamaana wanachi wangeamua kuteka kituo baada ya kamanda kugalagazwa chini bila kuwa na uwezo wa kutoa amri ya ulinzi wangesema ni jambo la kawaida ,Lazima RPC afutwe kazi kwa kudhalilisha Jeshi letu hatuwezi kukubali hata kidogo hakuna aliyejuu ya sheria
wanachi mara ngapi wachukua hatua mkononi mara ngapi wameua wakisingizia vibaka,wachawi,wazinzi kwani hiyo kesi ni mara ya kwanza au wanataka kuwachafulia Chadema hatutakubali kabisa
 
Duh! OCD Kala Ngwara ha ha ha watoto wa Kihuni wanasema Jamaa Amekata halafu Amefunua, OCD Chali halafu Kidume kinaendelea Kupiga Kampeni na Geshi Rinasema wanakitafuta

By The Way

Hivi Ile Ishu ya CCM Kuumiza Wanachadema kule Musoma Mjini, Mgombea wa CCM naye Alikamatwa au Ndiyo Mambo ya Ushuzi ajambe mwana CCM Akijamba Mwana CHADEMA kachafua hewa

Eti Hili ndio lichama la Baba wa Taifa LoL!

Dr. Slaa siyo mbaya ukamuuliza IGP mwema amechukua hatua gani Kwa OCD wake Kufumuliwa Mateke Kituoni
 
IGP MWEMA ATANISHANGAZA KAMA ATAACHIA MTU AMBAYE AMEDHALILISHA kAMANDA WETU MBELE YA kITUO CHA POLISI ,MBELE YA UMMA WA WATANZANIA,KUMDHALILISHA ASKARI MKUU WA KITUO ALIYE VAA KOFIA YENYE NEMBO YETU ETI ALIYEMPIGA HAKAMATWI KUHOJIWA KWA SABABU YUSUPHU MAKAMBA NA JAKAYA KIKWETE WAMEEAGIZA INA MAANA YUSUPHU MAKAMBA NA KIKWETE WAKO JUU YA SHERIA,KWELI NCHI HII IMEHARIBIKA KWA KWELI TUNAHITAJI MABADILIKO YA UONGOZI HUU NI USHENZI AMBAO HAUJAWAHI KUTOKEA TOKA NIZALIWE
ASKARI WADOGO WA KITUONI HAPO NA VITUO VINGINE WATAMUHESHIMU KWELI MTU KIONGOZI ANAPIGWA NGWALA MBELE YAO ,HUYO RPC AFUTWE KAZI

SHIBUDA HAKUWEKO KWENYE TUKIO LAKINI WAMEMUWEKA NDANI KWA KOSA LIPI
HAWA ZAMA ZAO ZIMEISHA BADO KITAMBO KIDOGO WATALI A NA KUSAGA
JAKAYA KIKWETE NCHI IMEMUSHINDA
TBC WAMEONYESHA UPANDE MMOJA WA HADITHI HAWAKUULIZA WANACHADEMA KITU GANI KILIJIRI WHAT SORT OF NOSENSE TIDO MHANDO KAISHIWA KABISA UPUUZI MTUPU NA UBAKAJI WA DEMOKRASIA TIDO YOUR DAYS ARE NUMBERED

AFTER THOSE DAYS WHO IS BEING PREPARED TO TAKE OVER? Betty Mkwasa, Charles Hillary, ........who?
 
Back
Top Bottom