Obama azidi kuibomoa USA!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Raisi wa USA Barack Obama ambaye ni raisi pekee wa Taifa hilo kubwa na lenye nguvu Duniani ambaye mpaka leo hii amevunja rekodi za uthubutu, yaani amefanya mambo ambayo Maraisi wote 43 wa USA hawajawahi kutuhubutu kuyafanya, sasa ameendelea na hatua yake ya kuzidi kulibomoa Taifa hilo baada ya kwa mara kwanza ktk Historia ya nchi hiyo kuruhusu Mashoga au kama wanavyojulikana huko USA homosexuals kuwa sehemu ya Jeshi sasa amekuja na jipya Jeshi hilo la USA limeruhusu transgender kuwa sehemu ya Jeshi, Transgender ni wale watu ambao wanazaliwa kwenye jinsia ambayo wao wanaona hawakustahili kuzaliwa nayo hivyo huamua kubadilisha yaani aliyezaliwa Ke hubadilisha na kuwa Me na kinyume chake, sasa Obama ameruhusu wawe sehemu ya Jeshi la USA kwa mara ya kwanza!

Cha kushangaza zaidi kila siku anaazidi kumchokoza Mrusi waingie Vitani huku Jeshi la nchi hyio (USA) akijaza Mashoga na transgender!

Hiyo ndiyo sura mpya ya Jeshi la USA, asante Obama!

1413839833194_wps_65_Transgendered_Preview_Tra.jpg

Jinsia mpya ilioanzishwa na Obama baada ya Ke na Me sasa kuna transgender

Obama-Transgender.001.jpeg

ben+carson.jpg
 
Nilimkubali Obama kwa muda wa mwaka mmoja tu wa uongozi wake mwaka 2008 lakini baada ya hapo nikamdharau sana kutokana na kukosa maono na msimamo thabiti kuhusu mahusiano ya kimapenzi kiasi cha kukosa ujasiri wa kuiga waliomtangulia kupiga vita ndoa za jinsia moja.
Ameweka alama moja mbaya sana hususani katika uso wa mtu mweusi mbele ya jamii ya kimataifa
 
Gays na homosexuals wanakubalika Marekani ki katiba sasa kuwazuia wasiingie jeshini ni kuwanyima haki na fursa sawa. Kuwepo kwa magay jeshini hakumaanishi kukiukwa kwa taratibu nyingine za kijeshi hii inamaana hairuhusiwi kuwa na mpenzi jeshini na kama imetokea umempenda mwanajeshi mwenzako unaripoti katika uongozi na mmoja wenu anahamishwa.
 
Sio Obama tu hata wanagombea urais Clinton na Trump wanaunga mkono LGBT.Kwa hiyo mimi sioni tatizo la Obama.
Isitoshe watu wanashindwa kuelewa maamuzi haya yanafanywa na wengi behind closed doors lakini Mkulu anatekeleza. Ukimwuliza Mkulu leo deep down atakujibu 'it's part of my job' tusimhukumu huyu mtu kihiiiivyooo
 
Gays na homosexuals wanakubalika Marekani ki katiba sas kuwazuia wasiingie jeshini ni kuwanyima haki na fursa sawa. Kuwepo kwa magay jeshini hakumaanishi kukiukwa kwa taratibu nyingine za kijeshi hii inamaana hairuhusiwi kuwa na mpenzi jeshini na kama imetokea umempenda mwanajeshi mwenzako unaripoti katika uongozi na mmoja wenu anahamishwa.

Duh, I reserve my comments kuhusu andiko hili, nadhani nimeeleweka....
 
Isitoshe watu wanashindwa kuelewa maamuzi haya yanafanywa na wengi behind closed doors lakini Mkulu anatekeleza. Ukimwuliza Mkulu leo deep down atakujibu 'it's part of my job' tusimhukumu huyu mtu kihiiiivyooo

Acha kuongopa, kwa nini hawa mashoga na transsexual hawakuruhusiwa wakati wa Bush au Reagan? Kwa nini wakati wa Obama tu?
 
Acha kuongopa, kwa nini hawa mashoga na transsexual hawakuruhusiwa wakati wa Bush au Reagan? Kwa nini wakati wa Obama tu?
Things have changed Mkuu. Idadi ya hawa watu imeongezeka kwa kasi kubwa hawana pa kutokea. It's politics Mkuu! Utafutaji wa kura hakuna lingine. Just a reminder' uwe na staha ya maneno sio kila mtu unamwita mwingo elimisha fafanua ni mjadala sio ugomvi!
 
Hauwezi kumtenganisha Obama na Mashoga na transgender, kwa maana kila siku analiongelea hili, hakuna raisi wa USA aliyewahi kuongelea mambo ya Ushoga kama Obama, Obama ndiye Raisi wa kwanza wa USA aliye tamka rasmi kwamba USA is no longer a christian nation!

Haya mambo yameanza zamani yalikuwepo Dunia nzima kama yalivyo mambo mengi tu lkn yamepata sauti baada ya Obama kuingia kwa maana yeye mwenyewe Obama ni muumini wa Ushoga, hilo liko wazi!
Ni kama hapa kwetu tu, mashoga wapo lkn wapo chini chini lkn siku Raisi akija na kusema wazi wazi kwamba wana haki sawa na ni sehemu ya jamii yetu na watoto shuleni wafundishwe kuhusu ushoga utaona jinsi utakavyoibuka!
 
Nilimkubali Obama kwa muda wa mwaka mmoja tu wa uongozi wake mwaka 2008 lakini baada ya hapo nikamdharau sana kutokana na kukosa maono na msimamo thabiti kuhusu mahusiano ya kimapenzi kiasi cha kukosa ujasiri wa kuiga waliomtangulia kupiga vita ndoa za jinsia moja.
Ameweka alama moja mbaya sana hususani katika uso wa mtu mweusi mbele ya jamii ya kimataifa
Ukichanganya na alivyomuua Gaddafi, ndio nazidi kumchoka!
 
Back
Top Bottom