Well said mkuu, kama Mandela aliweza kuwasamehe wajahili waliotaka kumtia kitanzi kwa nini hakumsamehe Winnie - hata kama alikuwa hataki kuendelea kuishi naye sioni sababu ya chama cha ANC kuendelea na njama za kutaka kumdhalilisha mbele za wageni? Watu wanacho sahau ni kwamba kelele na vitimbwi vya Winnie kwa Serikali ya makaburu wakati Mandela yuko kifungoni ndio kulikuwa kunaifanya Dunia ikumbuke Nelson Mandela, bila ya Winnie kuwasumbua Makaburu na kufanya vyombo vya habari kuwa vina andika habari zake mara kwa mara Mandela angesahulika, tuwe wakweli hapa - Winnie aliteseka sana na wanawe, aliwahi kufungwa gerezani, nyumbani kwake, kupigwa marufuku asikutane na watu etc, nasema hivi pamoja na mapungufu yake kama binadamu wengine tulivyo sihungi mkono mbinu za akina Jacob Zumma na kundi lake kufanya mbinu za kumu-ignore mama huyu - binafsi nimekasirishwa sana na njama hizi - Baraka Obama atakuwa alighafirika tu awezi kumu-ignore Winnie kimaksudi, si ajabu hajawahi kukutana nae hata Baraka na familia yake walipo kuwa wanakuja kumtembelea Mandela nyumbani kwake nadhani walikuwa wanakutana na Graca sio Winnie, Winnie alikuwa anaishi mbali na Graca. Tuwe wakweli hapa mtu uwezi kuzungumzia Mandela ukamsahau Winnie, looking back now naona wakina Zuma walikuwa wanakasirishwa na kauli za Winnie Mandela ambaye alikuwa anashutumu Serikali ya ANC kwa kuwasahau watu weusi walio pigana kufa na kupona kuiweka madarakani lakini anaona miaka karibu ishirini tangu wapate uhuru bado hali ya Wafrica ni duni sana, wengi wao wanaendelea kuishi kwenye slums, hawana umeme wala maji ya bomba - Winnie yuko outspoken sana katika suala hili na wanachi wengi wanamuhunga mkono - chukulia mfano wa leo pale uwanjani walipo kuwa wanataja jina la Winnie uwanja ulikuwa unalipuka kwa vifijo na makofi lakini sio kwa Graca, hata Zuma alizomewa - kwa nini?