Oa mwanamke mwenye elimu

Oa mwanamke mwenye elimu

At least awe amefika form four, narudia tena at least awe amefika form four.

As far as unajali future ya watoto wako,oa mwanamke mwenye elimu.

Usiwe mbinafsi kwa kutazama vigezo vyako kingono tu.

Oa mama wa watoto wako,

Kumbuka jinsi mke wako alivo ndio hivo pia watoto wako watakuwa.

Watoto wanarithi akili kwa mama yao ,naongea hili with experience.

Ni ushauri
Mkuu kwani elimu na ndoa vinaingiliana?????? Au nyie mliozaliwa 1990,s ndio mmekaririshwa hivyo????
 
Bila shaka unaongelea elimu ya darasani.Pili elimu na akili ni vitu tofauti.Kuna wadada hawajafika diploma au kidato cha 4, sio sababu hawana akili , bali mazingira, familia etc Kuna wadada wanafika hadi masters lkn ukiongea naye akili nzito haifunguki,amesoma kwa msukumo sababu resources zipo..
Bibi zetu hawakwenda shule, wengine hadi mama zetu..lkn hao ndo wamezaa wafanya biashara wakubwa, wanazuoni wakubwa, maprofessor n.k.
Kuoa ni fumbo, na usiwe na mategemeo makubwa sana kwa mwenzako.."You will be disappointed"Kikubwa awe mcha Mungu, akusikilize na kukuamini, awe na akili inayochakata na uelewa, awe na exposure, awe na uwezo wa kuconnect na watu na jamii, asiwe mshirikina...
 
Kuna binti mmoja ana degree ya uhasibu lakini hajui kutafuta asilimia, mpaka nilivyomuelekeza aisee nilishangaa sana
 
Kuna kusahau.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwamba nisijue kutofautisha kati ya kutojua na kusahau? Tena tulikuwa tunatafuta riba ya mkopo wa mama yake, akawa anapiga hesabu uchwara anazunguka ndo nikamuelekeza, kiwango chake cha shule na kozi yake asilimia wanafundishwa siku ya kwanza tu kuingia darasani, sasa km hicho kidogo kachemka mengineyo je? Kwahiyo kwa mfumo wetu wa elimu bado huwezi kutamba eti degree ana akili kumzidi wa la saba nk
 
At least awe amefika form four, narudia tena at least awe amefika form four.

As far as unajali future ya watoto wako,oa mwanamke mwenye elimu.

Usiwe mbinafsi kwa kutazama vigezo vyako kingono tu.

Oa mama wa watoto wako,

Kumbuka jinsi mke wako alivo ndio hivo pia watoto wako watakuwa.

Watoto wanarithi akili kwa mama yao ,naongea hili with experience.

Ni ushauri
Ambao hawajafika Form Four wataolewa na nani sasa?

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Kwani Elimu lazima nadhani huo ni ujinga Elimu ya bongo ni upuuzi Mimi nashauri mtu atafute Mwanamke mwenye akili na sio Elimu yetu ya ku-claim kiima na kiarifu.
kila mara elimu ya bongo, ni hatari sana mtu kujidharau mwenyewe. Ni elimu ya wapi nyingine we umeijaribu. Watanzania utafikiri wamezaliwa na baba na mama moja. Wote wana roho za husda, chuki, wivu. Ni km Msukuma, yule anaumwa kabisa kisa yeye ameshindwa kusoma na vijisenti kidogo. Wasomo wa nchi hii ndiyo wanaoendesha nchi, we utabaki elimu ya bongo, wenzako wameenda nje wamekuta elimu ni ile ile we baki kila siku elimu ya bongo. Ondoka wapeleke watoto wako unakoona kuna elimu bora.
 
sasa mkuu mpaka umefika form four si ndio uthibitisho kuwa angalau una akili..au unazungumzia akili ipi
Kuna wanaomaliza four hawajui hata kusoma wala kuandika huyo sasa unaenda kuopoa ukamwacha akiyemaliza STD 7 akafaulu ila akakosa mtu wakumlipia ada, hapo imekaaje!
 
Hii akili unayoizungumzia ni ya kurithi kwenye DNA au ya wakati wa malezi? Maana ya kwenye DNA huhitaji kwenda darasani kusoma classification. Vipi wazee wetu ambao hawajui darasa (baba na mama) halafu watoto ni vipanga huko shuleni na wamelelewa vizuri au ndo zama zimebadilika!
Na ndiyo walitulea vizuri sana, tulioenda shule hata malezi ya watoto tumeshindwa kutwa kushinda humu
 
Utafika mbali Sana daktari.

Watu wasichokielewa ni kuwa akili za darasani ni tofauti kabisa na za maisha.

Kuwa na uwezo wa kutoboa form foo haimaanishi wewe ni mzuri kiakili zaidi ya ambae hakusoma kabisa.
Akili ya darasani ni tofauti na ya maisha ya kawaida, utakuwa mwanaume anajivunia elimu lakini maisha anayoishi au vitu anavyovifanya ukiambiwa huyu mtu mwenye elimu yake zakutosha mpaka unamuogopa, njoo sasa kwenye maisha ya nyumbani mbuzi si mbuzi ,ng'ombe si ng'ombe ndama si ndama unabaki kushika kichwa, mie nazani na malezi toka kwa wazazi yanachangia, mtoto darasani pia apate elimu ya maisha ya kawaida ,na akili ya kuzaliwa nimuhimu sana( Mungu anahusika)
 
Back
Top Bottom