Oa mwanamke mwenye elimu

Oa mwanamke mwenye elimu

Oa mwanamke mwenye akili achana na elimu. Elimu kila mwanamke anayo ila akili wengi hawana

Shauri yenu vijana.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Elimu na kwenda shule.
Mtu anaweza kwenda shule na asiwe na Elimu vilevile mtu anaweza asiende shule na akawa na Elimu.
Nadhani wewe unaongelea kwenda shule na sio Elimu.
Education is the private matter btn the world of knowledge and experience and has little to do with school and college
 
Wengine tumezaliwa na wamama ambao hawakusoma hata darasa moja lakini wametukuza na tumefika mbali sana na tunawashukuru wametufikisha kwenye mafanikio.

Sijui unamaanisha nini unaposema atakavokuwa mke ndio atakavokuwa mtoto??

Sent from my SM-T285 using JamiiForums mobile app
Nimeipenda sana hii line.

Nimeisoma nikiwa natabasamu huku taswira ya mama yangu ikinijia kichwani,Mungu aendelee kuwalinda mama zetu.
 
Akili ya darasani ni tofauti na ya maisha ya kawaida, utakuwa mwanaume anajivunia elimu lakini maisha anayoishi au vitu anavyovifanya ukiambiwa huyu mtu mwenye elimu yake zakutosha mpaka unamuogopa, njoo sasa kwenye maisha ya nyumbani mbuzi si mbuzi ,ng'ombe si ng'ombe ndama si ndama unabaki kushika kichwa, mie nazani na malezi toka kwa wazazi yanachangia, mtoto darasani pia apate elimu ya maisha ya kawaida ,na akili ya kuzaliwa nimuhimu sana( Mungu anahusika)
Kuna ule upumbavu wa ndani/tabia ya mtu huwa hauondoki hata kwa elimu ndio maana unaweza kutana na mtu msomi lakini anayoyafanya utastaajabu ni upuuzi mtupu hata mtu ambae hakufika shule ana afadhali.

Akili ya Maisha haifundishwi shule na hiki kinafanya mzani ubalansi. Nakubaliana nawe malezi nayo huchangia kwa kiasi kikubwa utimamu wa mtu.
 
Kuna ule upumbavu wa ndani/tabia ya mtu huwa hauondoki hata kwa elimu ndio maana unaweza kutana na mtu msomi lakini anayoyafanya utastaajabu ni upuuzi mtupu hata mtu ambae hakufika shule ana afadhali.

Akili ya Maisha hayafundishwi shule na hiki kinafanya mzani ubalansi. Nakubaliana nawe malezi nayo huchangia kwa kiasi kikubwa utimamu wa mtu.
100%
 
Back
Top Bottom