Hamna mtihani mgumu sana kama kuchagua mke yaani kuna sometimes unatamani kuanza maisha ya ndoa ila huyo mwenzako sasa unayempata kisanga.
Ktk maboko yote usithubutu kuoa mke asiye na hofu ya Mungu, asiyekuwa na akili za maisha (utafutaji).Kuna wanawake ni la Saba ila hata ukimkabidhi fedha,anajua kuitunza na kuizalisha,anaheshim fedha na hababishwi na trending hizi material things (fashion na simu nk).Ila type hizi zipo chache, demu anaweza kukuomba elfu 20 ya kusuka, ukamtumia 50 baada ya siku mbili anakuomba efu 5 ya vocha ,sasa kama huyu hata awe nana degree hafai kuwa mke.
Nina mwanangu kaoa dem form ila yule binti ni hustler hakuna na alikuwa anamuwezesha mwanagu kipindi hana issues na kipindi hiko wapo kwenye uchumba.Sasa jamaa sasa hivi mambo yame mnyookea, hela anamkabizi mke anazungusha kwenye biashara zao familia.
Ukija kwetu si wengine demu unamtongoza asubuhi, jioni ana hela ya kula,kodi,king'amuzi hajalipa,luku imeisha, mdogo wake kameza shoka nk,sometimes basi wengine wanatuona tupo single sio kwamba hatutaki kuoa tatizo tunokutana nao.
Wenyewe ndio wanakwambia kumpiga mizinga mwanaume ndio,kipimo cha kujua kama mwanaume wana hela na siku hizi kuna michezo mara vikoba bado anataka presha zake za vikoba na michezo anayocheza uibebe ww na husiombe demu wako ndio awe kijumbe,mana vijumbe wengi wanatabia ya kujikopesha hela za watu za michezo ila uwezo wa kulipa hawana.
Halafu hamna mahusiano eti mama akiwa na elimu labda degree na kuendelea watoto watakuwa hivyo hivyo, kuna wazee kibao wana elimu ila watoto zao wapo hovyo,hivi vitu unaweza kuvijenga kupitia malezi ufuatiliaji na mazingira utakayo yajenga kama mzazi.