1 Wakorintho 13:4-8, ( "Wimbo wa Upendo".)
Tabia na sifa halisi za upendo na maana ya Sifa Hizi
• Huvumilia: Upendo una subira kubwa, hauchoki mapema, na unavumilia mapungufu ya wengine.
• Haufadhili: Unatenda wema na kuonyesha fadhili kwa vitendo
• Hauhusudu (Hauoni wivu):Upendo hauna wivu
• Hautakabari (Haujisifu): Upendo hautafuti sifa za kijinga wala kujikweza mbele ya wengine.
• Haujivuni: Upendo hauna kiburi cha moyoni wala dharau kwa walio chini.
Lakini UPENDO ni kujitoa kwa AJILI ya wengine,Kwa maana hata Mungu alitupenda hata akaota kwa AJILI YETU Tena kutoa kitu Cha thamani,
ANAYEKUPENDA hayupo tayari kukupoteza ,atajitoa kwa AJILI ya kukua KWAKO na kukua kwa familia Yako ,atajitoa kwa familia Yako atajitoa kwa AJILI Yako.
Hata kama WEWE huoni ata walioko karibu Yako watakwambia huyu binti anakupenda sana hata wazazi WAKO ama ndugu zako watakwambia huyu ANAKUFAA..hata kama WEWE umetiwa upofu WA kumtazama huku na HUKO kutafuta mwingine ..watakwambia walio karibu Yako huyu binti anakupenda ..ila kama ukitulia chini ukachunguza vizuri utaweza kugundua UPENDO WA KWELI haujifichi ni kama KIKOHOZI hakijifichi ama chafya ..ama tumbo la mimba hakijifichi..