Oa mwanamke anayekupenda

Oa mwanamke anayekupenda

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
3,235
Reaction score
3,666
MWANAMKE ANAONGOZWA NA HISIA ZAIDI KULIKO AKILI.
MAPENZI NI HISIA..
Mwanamke akikupenda AMEKUPENDA KWELI na utajua kuwa unapendwa hata kama wewe hutaona basi walioko pembeni ndugu jamaa na marafiki watajua kuwa huyo mwanamke anakupenda.

HATA KAMA HUNA PESA
atakuvumilia ,tena hatahitaji utumie pesa zako hovyo mana hapo anakupigia hesabu kama MUME anaanza kukuona kama baba wa watoto wake anakuwa na huruma anakuhurumia ,anakujali ,pia anajali kuhusu uchumi wako na familia yako anapenda kila kiti kuhusu wewe.

HATAPENDA utumie HELA HOVYO ama hatakuwa na matumizi ya ovyo ama hatapenda umuhonge kila wakati ATAKUHURUMIA ,tena kuna wakati kama anacho kitu hatakuficha ,haya kama ana pesa kidogo ,na kuna wakati ATAKATAA HATA PESA YAKO ukimpa ,na kuna wakati atatumia pess zake atachangia atakwambia leo nimepata mshahara ama leo usinipe pesa ,,bado ninayo ile ulionipa ,ama baki nayo tu ,

MWANAMKE KAMA hakupendi tambua huwezi kumbadilisha akupende ANAWEZA KUIGIZA lakini tambua Hisia zake ziko kwa mwingine moyo wake uko kwa mwingine ambaye siyo wewe ,ni kama unamlazimisha ni kama umembaka...

HATA UMUHONGE DUNIA pesa hainunui mapenzi ya kweli hainunui hisia za kweli.

Ndio hapa unakuta UNAMUHONGA WEWE pesa na yeye anahamishia kwa yule anayempenda ,

na mwanamke kama hakupendi hana HURUMA NA WEWE anakugeuza ATM MACHINE hata ukisema huna hela hakuelewi ,na hana bajeti ,na kila siku hana hela ,na hata umpe pess kiasi gani ,kila siku hazitoshi..na hata matumizi hana bajeti..hana HURUMA NA WEWE..ndio hao zamani walikuwa wanaita BUZI wanachuna mpaka ngozi.


HITIMISHO
*OA MWANAMKE ANAYEKUPENDA
N:B mwanamke kama hakupendi basi uwe na uhakika tambua kabisa kuna mwingine anayempenda kwa dhati ambaye SIYO WEWE.

Screenshot_20260221-161550.jpg
3b0e267845b8b2e9924004271108003c.jpg
 
OA MWANAMKE ANAYEKUPENDA📌
Kama mwanamke hakupendi basi tambua kuna mwingine anayempenda ambaye SIYO WEWE.

Hata UMUHONGE DUNIA huwezi kumfanya abadili HISIA ZAKE.

UKIMUHONGA SANA atachuma PESS kutoka kwako atahamisha kumpelekea KUMPA BUREE ampendaye.TENA atakuwa ANAKUOMBA HELA mara kwa mara HANA huruma na wewe hata ukisema HUNA hakuelewi.Na hana bajeti hana huruma na wewe.

Kama mwanamke hakupendi ni hakupendi tu hata kama hujamkosea akikuona tu hakupendi huwezi kumbadilisha

mwanamke ,akipenda anapenda kweli.(HUNA HAJA YA KUMUHONGA yeye atakuhitaji wewe zaidi kuliko ya pesa zako na anaweza hata kukupa wewe pesa zake ,na anakuwa anakuhurimia hataki UTUMIE HELA HOVYO hapendi UTOE TOE PESA ovyo,anakuwa na bajeti,hata ukimpa hela anaweza akakataa
 
She is not yours, It's just your turn.

Mwanaume huwezi pendwa bila sababu, huo Upendo wa bila sababu unapata kwa Mama yako mzazi pekee.

Hayo umezungumza yana Ukweli kiasi, But huwa ni kwa muda fulani tu hadi pale atakapotokea atakayekuzidi hilo jambo lililofanya akupende wewe.

Be a Man, yajue ya kuzingatia.
 
Huyo mwanamke labda anakuwa na uhitaji wa ndoa tu.
Anajibadilisha Ili umuone Dhahabu.

Ila akiingia ndani tu kwa uthibitisho wa madhabahuni ujue umeisha.Atajionesha rangi yake Halisi.Na hakuna rangi hutaacha kuona.
 
Kuna umri mwanamke anaweza kupenda mtu akiwa na 16-25. Huu umri anakuwa bado hajajua jinsi ulimwengu ulivyo na mambo mengi ndio anajaribu kwa mara ya kwanza.

Baada ya hapo maisha na mazingira ndivyo vinaamua awe na 'mahusiano' ambayo kiuhalisia siyo upendo ule wa dhati bali ni kwamba umemkuta katika mazingira ambayo lazima awe na mwanaume ili avuke hatua fulani (kimaslahi zaidi) Hapa ndio wanaume wengi wanapoingizwa chaka.😅
 
When the wrong one LOVES you Right.😎

only to find out that you are the one who was WRONG and actually ,she is your missing RIB
😎
Proverbs 18:22 says: "He who finds a wife finds what is good and receives favor from the LORD." (or "obtains favor from the Lord").
AM LIVING THE LIFE OF FAVOUR FROM GOD🙏

Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA
 
Watakuja kukuambia pole haikuwa fungu lako. Na pia hayana mwongozo

Wamatumbi bwana dah😂
 
When the wrong one LOVES you Right.😎

only to find out that you are the one who was WRONG and actually ,she is your missing RIB
😎
Proverbs 18:22 says: "He who finds a wife finds what is good and receives favor from the LORD." (or "obtains favor from the Lord").
AM LIVING THE LIFE OF FAVOUR FROM GOD🙏

Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA
 

Attachments

  • images (67).jpeg
    images (67).jpeg
    36.2 KB · Views: 6
  • images - 2024-10-27T132434.540.jpeg
    images - 2024-10-27T132434.540.jpeg
    51.3 KB · Views: 4
  • images (23).jpeg
    images (23).jpeg
    11.7 KB · Views: 5
Kazi ya kupenda ni ya wanaume
Sisi tumeagizwa kutii
 
.
 

Attachments

  • images (47).png
    images (47).png
    12.4 KB · Views: 4
  • images - 2026-08-10T194352.388.jpeg
    images - 2026-08-10T194352.388.jpeg
    21.7 KB · Views: 4
  • images - 2026-08-10T194656.412.jpeg
    images - 2026-08-10T194656.412.jpeg
    28.3 KB · Views: 5
Back
Top Bottom