Nyumba ya Oscar Kambona sasa ni Feza Primary. Nini kimetokea?

Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
2,125
3,130
Wazoefu wa mitaa ya Mikocheni, kwa Nyerere, kwa Mwinyi, kwa Warioba haya ni majina ya vituo vya daladala. Lakini pia Kuna nyumba ya Oscar Kambona mitaa hiyo ila kwa sasa naona imekuwa shule ya msingi Feza.

Nini kilitokea? Iliuzwa? Je Kambona hakuacha familia? Mke na watoto wake wako wapi? Baba akiwa muasi hadi familia yake inachukuliwa kama waasi?

Je, ilikuwa ni nyumba ya serikali au alijenga mwenyewe Oscar?
 
Wazoefu wa mitaa ya Mikocheni, kwa Nyerere, kwa Mwinyi, kwa Warioba haya ni majina ya vituo vya daladala. Lakini pia Kuna nyumba ya Oscar Kambona mitaa hiyo ila kwa sasa naona imekuwa shule ya msingi Feza.
Nini kilitokea? Iliuzwa? Je Kambona hakuacha familia? Mke na watoto wake wako wapi? Baba akiwa muasi hadi familia yake inachukuliwa kama waasi?
Je ilikuwa ni nyumba ya serikali au alijenga mwenyewe Oscar?
Oscar Kambona ana mtoto wa kike ni Askari Magereza gereza la Karanga Moshi. Kama sikosei anaitwa Witness.
Huwezi amini mtoto wa Kambona analipwa mshahara usiozidi TSH laki tano.
 
Hata sijui alimkorofisha nini yule mzee wa Butiama?
Kambona aliamini siasa za ubepari na akiwa Waziri akishaingia mikataba mingi na wawekezaji wa Kiingereza na walimpa cha juu chake. Kwenye account yake alikua na pesa nyingi sana.

Wakati Nyerere aliamini katika Ujamaa, hakuwa na tamaa ya pesa na mpaka anastaafu hakuwa na hekalu alilojimilisha.
 
Kambona aliamini siasa za ubepari na akiwa Waziri akishaingia mikataba mingi na wawekezaji wa Kiingereza na walimpa cha juu chake. Kwenye account yake alikua na pesa nyingi sana

Wakati Nyerere aliamini katika Ujamaa, hakuwa na tamaa ya pesa na mpaka anastaafu hakuwa na hekalu alilojimilisha.
Hayo yote aliyasema Nyerere, vipi upande wa Kambona kuna aliyemsikiliza?
 
Kambona aliamini siasa za ubepari na akiwa Waziri akishaingia mikataba mingi na wawekezaji wa Kiingereza na walimpa cha juu chake. Kwenye account yake alikua na pesa nyingi sana

Wakati Nyerere aliamini katika Ujamaa, hakuwa na tamaa ya pesa na mpaka anastaafu hakuwa na hekalu alilojimilisha.
Lakini Kambona kaonekana ndie aliyekuwa sahihi kuliko Mwalimu. Yafanyikayo sasa ni mawazo ya Kambona ya Nyerere yalishakufa kibudu
 
Kuna gazeti kule jamii photos wameandika "OSCAR KAMBONA MALAYA" Miaka hiyo .....nilichojifunza in life NO PERMANENT FRIEND NO PERMANENT ENEMY
20220105_140747.jpg
 
Feza ni shule binafsi, nyumba ni mali binafsi sasa unaulizia mambo binafsi ambayo watu wamekubaliana wenyewe sisi tutajuaje?

BTW wanaweza kuwa na Mali nyingi wakaamua kuipangisha Ile nyumba sababu inakaa bure tu, pia kuipangisha Feza schools wanapata pesa nyingi sana imagine Ada ya mtoto sio chini ya milioni saba sasa unadhani Kodi ni kiasi gani?
 
Hayo yote aliyasema nyerere vipi upande wa kambona kuna aliyemsikiliza?
Nyerere alikuwa dikteta uchwara, hoja zake zote alizompinga nazo kambona zilikuja 'kuprove failure',kambona alikuwa anaona mbali kutokana na exposure na elimu, Nyerere alikuwa amemezwa na wachina,akaishia kufeli kwnye kila kitu,azamio la Arusha lilifeli,vijiji vya ujamaa vilifeli, ujamaa wenyewe ulifeli aliachia nchi kwa aibu watu wakiwa hawana chakula Wala mavazi!!
 
Back
Top Bottom