Nyumba ya mil. 89/- yamtatiza DC

Nyumba ya mil. 89/- yamtatiza DC

Na ile Rasimu ya Katiba ambayo ingeweza japo kugusa maeneo hayo imekuwa kama mbingu na dunia.Imeshakwenda na maji na Aliyeajitahidi kuitayarisha ndiyo huyo anaoga MATUSI na DHIHAKA,tumeletewa hii ya Kuimaliza na kuuza hata miguu yetu,sina uhakika kama tumebaki nayo,maana vichwa vyetu viliishauzwa,sina uhakika wa tumbo na miguu.
Yule babu akagusia hayo kwenye rasimu yake, kwanza hivyo vitu vinataka ukaguzi tu sasa vyombo husika vipo pengine tatizo ni wahusika wavivu (CAG) or to do with resources za kuwawezesha ie capital (equity or human). Njia nyingine ni kuongeza vyombo vya ukaguzi nimeona kuna wengine lakini more needs to be done in terms of improving accountability kwanza hata unamsikia huyo mzee wa rasimu akiangaika na haya yeye muungano tu ndio muhimu kwenye rasimu yake ambayo BLK wanadai katiba mpya ina mapendekezo 81 yaleyale labda yamekwa kisheria zaidi. Sasa sijui bado amezira kwanini ana matatizo yule grumpy old man.
 
Milioni 89?? Basi kazi ipo. Mbona nyumba ya kawaida sana hiyo!

barafuyamoto,

Mwashangaa nini ilhali nyie wenyewe ndiyo mnaowaweka madarakani???Hivi sasa wanatafuta Fueza ya kuwahonga kwene Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015. Ngoja wazichange halafu wakianza Kampeni wanatumia fueza hiyohiyo kuwanunulia WALI MAHARAGE, FULANA,T-SHIRT NA KOFIA ili muwape ushindi wa kishindo!!

Kweli katika Tanzania WAJINGA NDIO WALIWAO!
 
kibogo na ROBERT MICHAEL mnajaribu kuuleta mjadala kwenye uhalisia wa mradi tajwa. Bahati mbaya michango mingi imewafunika sana humu kutokana na ushabiki...
 
Last edited by a moderator:
From Engineering point of view,
Naomba kuelewa eneo ilikojengwa hiyo nyumba, hali ya barabara ilivyo kutoka maeneo yenye vifaa vya ujenzi hadi eneo la ujenzi, bei za vifaa vya ujenzi kwa Igunga, source of local materials kama mawe, mchanga, mbao nk zinakotoka (umbali) na zinauzwaje. Vipimo vya nyumba yenyewe n.k kisha tujue gharama za ufundi zikoje baada ya hapo ndo tumuhukumu jamaa!

Omuregi Wasu, ninaomba utumie hata ule ujuzi wako pamoja na wewe kuwa mwenyeji wa TZ regardless wewe unaishi wapi utoe hukumu yako bila kusubiri hizo data. Hata ingekuwa wapi hiyo mil 89 ni nyingi kwa hiyo nyumba! Chukua costs za vifaa peke yake and double it then uone utakuwa wapi katika mil 89. Si ajabu wewe ni kati ya watu wetu wale '' tuunde kwanza tume ya uchunguzi''
 
Sifa kuu ya Viongozi wote wa MACCM ni wizi, udanganyifu, ufisadi na uhuni wa kila aina.
 
halafu unaweza kuta mjenzi wa hiyo nyumba ni mwanachama wa chadema halafu anasema serikali ya ccm iache ufujaji
Ni kweli nusu ya wakandarasi nchini ni makampuni ya kichagga.
 
kwan mnashagaa nn jaman? mmekuwa wagen wa serikali yetu? acha watendaji, mwalim mkuu, afisa eluim pamoja na mkurugenzi wa igunga wapige hela, hizi hela za umma zitasalimika tu, pale ccm kitakapokuwa chama cha upinzan, yaan hiyo nyumba hifiki ata mil.10. haya yanatokea ba'riz anatunukiwa uprof. na wachina kwa kuwapa gesi teheeeeheee! chezea ccm ww!
 
katika Halmashauri zinazoongozwa na CCM, makandarasi karibia wote wa kazi za serikali au ni wanafamilia wa vigogo wa CCM au au marafiki wa vigogo wa CCM.

Kuna rafiki yangu aliwahi kupata uwakala wa pembejeo, ilipogundulika kuwa ni mwanaCHADEMA mwaka uliofuata alipigwa chini japo ndiye aliyekuwa wakala mwenye uwezo kuliko wote waliobakizwa.

halafu unaweza kuta mjenzi wa hiyo nyumba ni mwanachama wa chadema halafu anasema serikali ya ccm iache ufujaji
 
Wakuu,
Miradi ya Ujenzi katika Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, imeghubikwa na tuhuma za ufisadi, ambapo hivi karibuni imekabidhiwa nyumba ya Mwalimu yenye Vyumba viwili vya kulala na sebule, ikitajwa kugharimu sh. milioni 89, jambo ambalo limeibua utata na kumlazimu Mkuu wa Wilaya hiyo, Elibariki Kingu kuingilia kati.

Gharama ya ujenzi wa nyumba hiyo katika Shule ya Sekondari Ichana Kata ya Chabutwa ni sehemu ya Matumizi ya Milioni 219 zilizotolewa na Serikali kuu kupitia mpango wa maendeleo ya Elimu ya Sekondari[MMES] kwa ufadhili wa bank ya Dunia.

Wakuu naomba tujadili haya matumizi. Nimejaribu kuweka picha kutoka Gazeti la Tanzania daima la Leo.

attachment.php


Mia
This is a joke, right?
 
nyumba-300x171.jpg

Nyumba iliyogharimu 89M

MIRADI ya ujenzi katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, imeghubikwa na tuhuma za ufisadi, ambapo hivi karibuni imekabidhiwa nyumba ya mwalimu yenye vyumba viwili vya kulala na sebule, ikitajwa kugharimu sh. milioni 89, jamba ambalo limeibua utata na kumlazimu Mkuu wa wilaya hiyo, Elibariki Kingu kuingilia kati.

Gharama ya ujenzi wa nyumba hiyo katika shule ya sekondari Ichama kata ya Chabutwa ni sehemu ya matumizi ya kiasi cha sh. milioni 219 zilizotolewa na Serikali kuu kupitia mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.


Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumatano, umebaini kuwa mbali na kiasi hicho pia katika muendelezo wa matumizi ya fedha hizo, sh. milioni 8.6, zimetumiwa kwa ajili ya kujenga tanki la kuvunia maji ya mvua katika nyumba hiyo, hali inaibua maswali kwa wakazi wa Chabutwa kutokana na ubora wa nyumba yenyewe na gharama zinazotajwa kutumika.


Kutokana na utata huo, tayari mkuu wa wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu, ameingilia kati na kutaka malipo ya mradi huo yasitishwe huku akiagiza wataalam wa halmashauri kufanya tathmini upya kuthibitisha kama thamani ya fedha inalingana na ubora wa nyumba.


Oktoba 8 mwaka huu, wakati kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Rache Kasanda akiikagua nyumba hiyo ya mwalimu baada ya kuifunga, alisikika akisifia kuwa ni bora kwa kile alichoeleza kuwa haina dalili yoyote ya nyufa.


Gazeti hili lilipomhoji juu ya gharama zilizotajwa katika taarifa ya halmashauri kama zinarandana na ubora wa nyumba, Kasanda alisema wahusika walimueleza kuwa gharama zilizoandikwa katika taarifa zilikuwa zimekosewa na kwamba nyumba imegharimu sh. milioni 38 na si 89 iliyosoma kwake.


“Wasaidizi wangu ulioongea nao awali waliniambia juu ya hilo na nikafuatilia na mkurugenzi ameniambia walikosea katika kuandika na kwamba gharama zake ni sh. milioni 38,” alisema Kasanda akiwa katika kata ya Simbo.


Nyumba hiyo ina vyumba viwili vya kulala visivyokuwa na vyoo vya ndani, sebule moja pamoja na madirisha manne yaliyowekwa nondo na nyavu, huku sakafu yake ikiwa ya kawaida ya saruji na kuezekwa kwa bati.
Kwa mujibu wa taarifa fupi ya ujenzi iliyosomwa kwa kiongozi wa mbio za mwenge, mbali na sh milioni 89 gharama za nyumba hiyo, pia zimetumika sh .milioni 58.5 kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha maabara, sh. milioni 38.8 kwa ajili ya vyumba viwili vya madarasa na sh. milioni 23.9 kwa ununuzi wa samani.

Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya ukandarasi ya Elisha & Son Ltd ya mjini Igunga, iliyopewa kazi ya ujenzi wa majengo hayo, alipoulizwa gharama za nyumba ya mwalimu alisema hazizidi sh. milioni 50 na si chini ya milioni 40.

“Kama wanasema ni sh. milioni 89 sasa unanifumbua macho labda kuna mkataba unaotuhusu sisi na ule unaohusu taarifa zao mbele ya umma lakini hizo gharama za nyumba hazifiki huko,” alisema.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Igunga, Rustruka Turuka alipoulizwa gharama halisi ya jengo hilo, alielekeza swali hilo kwa Afisa Elimu Sekondari, Aloyce Kaziyareli ambaye alisema gharama zilizosomwa siku ya uzinduzi ndizo zinapaswa kufuatwa.

“Gharama ni hizo hata hiyo nyumba ndiyo gharama yake, sasa ukitaka kujua zimefikaje hayo ni maswali ya Mkandarasi,” alisema Kaziyareli.

Jana, mkuu wa wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu, alizungumza na gazeti hili na kukiri kuwaita badhi ya maofisa wa halmashauri katika ofisi yake kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa ubora wa mradi huo na fedha zilizotumika.


Alisema baada ya kuongea nao aliwaagiza kusitisha malipo kwa mkandarasi na kisha mthamini wa ujenzi wa halmashauri awasilishe taarifa yake ya kukubali jengo hilo la walimu kuwa na thamani ya sh. milioni 89.


Kwa mujibu wa Kingu, baada ya hatua hiyo wataalam mbali mbali wataenda kufanya tathmini upya kuthibitisha kama nyumba iliyojengwa ina thamani ya fedha iliyotajwa.

Huyu aliyepitisha BOQ ya fedha hizo tunamtaka ajieleze kwa kuwa jengo halilingani na thamani ya fedha iliyotajwa,” alisema Kingu.

Tanzania Daima
 
Ndio tatizo lenyewe linalosababisha ufisadi pull inflation kwenye nyumba kwa sababu hizi sansana dar matokeo yake sie wengine tulio wengi tunajikuta tunalipishwa kodi za ajabu mishahara yenyewe hiko wapi ya kumudu maisha kisa tu jirani kauza nyumba ya million 50 kwa millioni 100 kwa hela ya ufisadi.

Kila mtu mtaani anaanza kuamini kweli nyumba yake inathamani hiyo na kupandisha thamani areas unnecessarily matokeo yake tunapandishiwa kodi kila uchao na viwanja vinakuwa gharama kuliko gharama ya kujenga nyumba. Ufisadi unaaribu uchumi wa taifa inatosha wajameni sanasana kwenye nyumba wengi tuna-feel hizi impact.

mpaka mafisadi waishe ndo mtakuwa ha-feel impact za ufisadi!
 
Yule babu akagusia hayo kwenye rasimu yake, kwanza hivyo vitu vinataka ukaguzi tu sasa vyombo husika vipo pengine tatizo ni wahusika wavivu (CAG) or to do with resources za kuwawezesha ie capital (equity or human). Njia nyingine ni kuongeza vyombo vya ukaguzi nimeona kuna wengine lakini more needs to be done in terms of improving accountability kwanza hata unamsikia huyo mzee wa rasimu akiangaika na haya yeye muungano tu ndio muhimu kwenye rasimu yake ambayo BLK wanadai katiba mpya ina mapendekezo 81 yaleyale labda yamekwa kisheria zaidi. Sasa sijui bado amezira kwanini ana matatizo yule grumpy old man.

Kama hawa watu wangekuwa vetted kama Kenya na wakawa huru kweli basi ujue kila kitu kingekuwa wazi zaidi,na auditor ambaye angepokea hongo basi sheria ingeelekeza nini kifanywe.Lakini auditors wenyewe wananjaa wako tayari kuuza utu wao kwa vijisenti vidogo sana.Nafuu hata huyo babu Warioba amekumbuka.

Ukumbuke kulindana nako ni kwingi.Hivi anaenda kumuaudit rafiki,ndugu,kaka,dada,baba ,mama mjombo nk anafanyaje?Kama sheria haiko kali anamuomba mtu vijisenti anawalipa wenzie kitu kinatoka.Upo dada yangu hapo?
 
Na wakiambiwa ni wezi wanakimbilia kulaumu kuwa ni chuki binafsi. Mambo kama haya yako mengi na utawasikia tena ni upepo tu litapita. Kama tulivyoona ya Miss TZ jamaa wanavyo jitahidi kusafisha choo kwa kutumia uchafu wa chooni.
 
kuna choo cha shimo tundu mbili millioni 96 kilikuwa kijengwe stand ya zamani kule geita mwenyekiti wa ccm akahaahamasisha wananchi wakafukia msingi....
hii niliona kupitia ITV
 
Back
Top Bottom