Nyumba ya mil. 89/- yamtatiza DC

Nyumba ya mil. 89/- yamtatiza DC

Wakuu,
Miradi ya Ujenzi katika Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, imeghubikwa na tuhuma za ufisadi, ambapo hivi karibuni imekabidhiwa nyumba ya Mwalimu yenye Vyumba viwili vya kulala na sebule, ikitajwa kugharimu sh. milioni 89, jambo ambalo limeibua utata na kumlazimu Mkuu wa Wilaya hiyo, Elibariki Kingu kuingilia kati.

Gharama ya ujenzi wa nyumba hiyo katika Shule ya Sekondari Ichana Kata ya Chabutwa ni sehemu ya Matumizi ya Milioni 219 zilizotolewa na Serikali kuu kupitia mpango wa maendeleo ya Elimu ya Sekondari[MMES] kwa ufadhili wa bank ya Dunia.

Wakuu naomba tujadili haya matumizi. Nimejaribu kuweka picha kutoka Gazeti la Tanzania daima la Leo.
attachment.php

Mia
kama tulipata theluthi mbili kwenye bunge la katiba kwa nini nyumba hii isiwe na thamani hiyo?
 
Hapo ni bila VAT. Hujui mwaka 2015 unakuja? Hata sijui nitakuwa wapi, nakusanya virago nikijiandaa kustaafu!
 
Acha na wengine nao walepo mbona na akina Muhongo, Tibaijuka, jaji Werema, Maswe na mafisadi kibao waligawana bilioni 400 za escrow account na hawakuhojiwa? wote hawa ni WAKORA tu. Serikali ya wezi, wahujumu, majangili, mafisadi kuanzia kichwani mpaka kwenye unyayo wa mguu.

Hapo intelijensia ya polisi, usalama wa taifa na vyombo vya dola iko wapi? wanaweza kuona maandamano ya vyama vya siasa ni hatari kwa usalama wa nchi lkn hawa vibaka walipokuwa wanapakia minoti ya IPTL ni usalama kwao. Tujipange tuwabwage mafisadi na serikali dhalimu ya CCM.
 
ngoja wavimbiwe tu wakt wa kuendesha unakuja,tuandalie dawa ya tumbo tu hawa walafi.
 
Kuna maswali mengi ya kuulizwa juu ya hili:-
1. Mkandarasi aliyejenga ni nani?
2. Nyumba iliyotakiwa kujengwa ilikuwa iwe ya aina gani? ni vema Ramani ikaonyeshwa
3. Je ujenzi huo ulipewa baraka na kamati ya fedha ya halmashauri(Finance)?
4. Wakati wa ziara za ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayofanywa na madiwani (CCM) hawakugundua kuwa ujenzi huo hauendani na gharama halisi zilizopitishwa katika vikao vyao?
5. Ni nani aliyeidhinisha malipo hayo huku akijua hayaringani na uhalisia wa kilichojengwa?
6. BOQ ya ujenzi huo inasemaje?
7. Je upatikanaji wa mzabuni huyo ulifuata taratibu zote?

Hayo maswali uliyojiuliza yakipata majibu je itakuwa ni halali au siyo halali?
 
No wonder, CCM wanatunikiwa Uproffesor .................... probably kwa ufujaji wa mali za umma!!
 
Ndani ya serikali ya CCM yote hayo yanawezekana...

kama mnakubali ndani ya serkali ya ccm mkubali na serikali ya ccm ndio iliojenga barabara za rami zote hapa nchini na madaraja yake na mahospitali mavyuo lakini kwa kuwa mnaakili viazi hapo mtakataa
 
vijipesa vya ugoro tu hivyo, acheni wivu wa kike
 
From Engineering point of view,
Naomba kuelewa eneo ilikojengwa hiyo nyumba, hali ya barabara ilivyo kutoka maeneo yenye vifaa vya ujenzi hadi eneo la ujenzi, bei za vifaa vya ujenzi kwa Igunga, source of local materials kama mawe, mchanga, mbao nk zinakotoka (umbali) na zinauzwaje. Vipimo vya nyumba yenyewe n.k kisha tujue gharama za ufundi zikoje baada ya hapo ndo tumuhukumu jamaa!
 
Ujenzi wenyewe wa Igunga, tofali za kuchoma, mbao bei rahisi, hiyo nymba milioni 25 inakamilika na kukabidhiwa kwa sherehe kuuubwa kabisa, vinginevyo, kwa gharama hizo wenyeji tusingejenga.
 
kwa serikali hii ya ccm hili sio la kushangaza sana.

wakati wanaanza bunge maalum la katiba akidi kwa zanzibar ilikuwa inatakiwa wabunge 16 kutoka CUF jamii ikaamini hivyo mpaka mwanasheria mkuu aliwahi kusema kuwa akidi haitatimia.lakini bila wabunge wa cuf na ukawa akidi imetimia na wabunge waliokufa wamepiga kurq.sasa kwanini ushangae nyumba ya milion 15 kuwa ya mil 89? ndo ccm hiyo mambo kuchakachua na kulia sana
 
Kuna maswali mengi ya kuulizwa juu ya hili:-
1. Mkandarasi aliyejenga ni nani?
2. Nyumba iliyotakiwa kujengwa ilikuwa iwe ya aina gani? ni vema Ramani ikaonyeshwa
3. Je ujenzi huo ulipewa baraka na kamati ya fedha ya halmashauri(Finance)?
4. Wakati wa ziara za ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayofanywa na madiwani (CCM) hawakugundua kuwa ujenzi huo hauendani na gharama halisi zilizopitishwa katika vikao vyao?
5. Ni nani aliyeidhinisha malipo hayo huku akijua hayaringani na uhalisia wa kilichojengwa?
6. BOQ ya ujenzi huo inasemaje?
7. Je upatikanaji wa mzabuni huyo ulifuata taratibu zote?

Mkuu umeuliza maswali mazuri sana ambao kwa sisi tunaohusika kwenye sekta ya ukandarasi tumekuelewa.
 
kimusingi tumefikia hatua kama hii si kwa bahati mbaya ila ni kutokana ns utamaduni wetu watz kufanya vitu bila kufikiri kwanza maana hakuna wa kuhoji siasa ni imara zaidi ya taaluma,na hata hili hatutajua mwisho wake
 
From Engineering point of view,
Naomba kuelewa eneo ilikojengwa hiyo nyumba, hali ya barabara ilivyo kutoka maeneo yenye vifaa vya ujenzi hadi eneo la ujenzi, bei za vifaa vya ujenzi kwa Igunga, source of local materials kama mawe, mchanga, mbao nk zinakotoka (umbali) na zinauzwaje. Vipimo vya nyumba yenyewe n.k kisha tujue gharama za ufundi zikoje baada ya hapo ndo tumuhukumu jamaa!

Kwa hiyo hapo mzee unaulizia bill of quantities.
 
From Engineering point of view,
Naomba kuelewa eneo ilikojengwa hiyo nyumba, hali ya barabara ilivyo kutoka maeneo yenye vifaa vya ujenzi hadi eneo la ujenzi, bei za vifaa vya ujenzi kwa Igunga, source of local materials kama mawe, mchanga, mbao nk zinakotoka (umbali) na zinauzwaje. Vipimo vya nyumba yenyewe n.k kisha tujue gharama za ufundi zikoje baada ya hapo ndo tumuhukumu jamaa!
maswali mazur lakin kwa hawa viongozi wetu sijaona kama hata moja litapata jibu hapoo sizani mie
 
Haya ndio matatizo yetu unless we sort accountabilities issues trust will never be forged na maendeleo yatatuchukua muda mrefu sana, njia za uchumi na soko itakuwa ngumu sana kujua uhalisia wake.

Despite maendeleo ya China leo President Xi Jinping kitu cha kwanza kukikomalia ilikuwa ni basics kwa sababu hizi hizi za kipumbavu kutoka kwa watendaji wa serikari na chama chao.

China leo kuna kesi zaidi ya elfu kumi za maafisa wa serikari na zaidi ya watu 2000 wameshajiua kwa aibu ya ubadhirifu wa mali za umma, kuchukuwa rushwa na mengineo ambayo sio stahiki jamaa alishaona sasa wanaelekea kwenye epidemic and matters needed highest authority kabla aijakuwa tabia sugu.

Sisi kila siku tunalalama tu no actions 'maneno matupu ayavunji mfupa' hii mijitu imezidi kwakweli na atuwezi rekebisha chochote au maendeleo kuwafikia wengi kama utaratibu ndio huu.
 
Tatizo kubwa la TZ ndio hilo. mambo yanafanyika kichinichini na maujenzi, yakisha kamilika ndio watu wanataja gharama zilizotumika, na wakati huo ni too late. watu wameshamega la kwao kwa nguvu tu.
Nchi zilzo endela kama wanaaka kujenga kitu au kufanya kitu, kitu cha kwanza wanatangaza na kuweka gharama zote baada ya hapo wananchi wanajadiliana ilikupata ufumbuzi mzuri.

Tusema hapo kama ingetangazwa na kuandika kwenye magazetikuhusu ujenzi wa hizo nyumba, na kuweka uwazi aina ya nyumba na gharama itakayogharimu, na ikiwezekana kuweka picha aina za CAD, picha hizo ni mara mmoja zinachorwa kwenye compter, basi watu wengejua ni kitu gani kinacho endelea na hizogharama ni halali au sio. Hapo isingetokea uwizi kabisa, labda huyo kandarsiachakachue kwenye cement na vifaa.

Tunaoma serekali ifanye kama hivyo, kutangaza kwanza jamboili wananchi wajue na kujadili kwanza, ingawa kuna watakao pinga lakini uwizina ufisadi utapungua sana.
 
Nyie bavicha tabu sana, yaani huto tuvisenti tu...serikali sikivu ya ccm inaboresha maisha ya waalimu kwa kutumia vijisenti vidogo tu hivyo nyie keleleeeeeeee, mnawaza kwa kutumia masaburi haki ya nani...hiyo nyumba gharama halisi ni 150ml. hapo tumebana matumizi matumizi sanaaa ndiyo zikafikia 86ml. bavicha acheni wivu wa kike...hii ndiyo serikali ya ccm, maisha bora kwa kila mdanganyika.

Ha ha haaa, natumai una maanisha kinyume chake ndugu!
 
Back
Top Bottom