View attachment 195418
Nyumba ya mil. 89/-MIRADI ya ujenzi katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, imeghubikwa na tuhuma za ufisadi, ambapo hivi karibuni imekabidhiwa nyumba ya mwalimu yenye vyumba viwili vya kulala na sebule, ikitajwa kugharimu sh. milioni 89, jamba ambalo limeibua utata na kumlazimu Mkuu wa wilaya hiyo, Elibariki Kingu kuingilia kati
KAMA SIJAKOSEA HII SHULE IPO PEMBENI YA BARARABA KUU SINIDA TO TABORA, UMBALI MDOGO TOKA OFISI ZA HALMASHAURI YA IGUNGA AU KAMA SIO NI ILE ILIPO KAMA UNAENDA NZEGA KWA KUTUMIA BARABARA YA VUMBI.
Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumatano, umebaini kuwa mbali na kiasi hicho pia katika muendelezo wa matumizi ya fedha hizo, sh. milioni 8.6, zimetumiwa kwa ajili ya kujenga tanki la kuvunia maji ya mvua katika nyumba hiyo, hali inaibua maswali kwa wakazi wa Chabutwa kutokana na ubora wa nyumba yenyewe na gharama zinazotajwa kutumika
SIJAWAELEWA TANZANIA DAIMA HAPA, MARA TANKI MARA NYUMBA. KINACHOWASHANGAZA NI KUTUMIA NILLION 6 KUJENGA TANKI? SAS HAPA NAJIULIZA NI AINA GANI LA TANKI, TANKI LA ZEGE? LA USAWA WA ARDHI? CHINI YA ARDHI? AU LA JUU? JE HIYO PESA IMETUMIKA KUJENGA TANKI TU AU PAMOJA NA MFUMO MZIMA WA MAJI YAANI MABOMBA NA FREMU KAMA LIPO JUU YA ARDHI? JE SHULE ILIKUWA NA MAJI KABLA? KAMA ILIKUWA HAINA, MAJI YALIKUWA YAPO UMBALI GANI?
Kutokana na utata huo, tayari mkuu wa wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu, ameingilia kati na kutaka malipo ya mradi huo yasitishwe huku akiagiza wataalam wa halmashauri kufanya tathmini upya kuthibitisha kama thamani ya fedha inalingana na ubora wa nyumba
MPAKA MKUU WA WILAYA ANAINILIA KATI DED ALIKUWA WAPI? ALIKUWA HAJUI WAKATI YEYE NDIYE MTENDAJI MKUU WA HALMASHAURI. NI NANI ANAYEIDHINISHA MALIPO? NI DED AU MHANDISI WA WILAYA? WATAALAM WA WILAYA WAFANYE TATHIMINI UPYA TENA? TANU NYUMBA INAANZA KUJENGWA KWANI WATAALAM WALIKUWA HAWAJUI? NI NANI ALIYEANDAA TENDER DOCUMENTS/ BOQ? KESI YA NYANI ANAPEWA NYANI TENA..........
Gazeti hili lilipomhoji juu ya gharama zilizotajwa katika taarifa ya halmashauri kama zinarandana na ubora wa nyumba, Kasanda alisema wahusika walimueleza kuwa gharama zilizoandikwa katika taarifa zilikuwa zimekosewa na kwamba nyumba imegharimu sh. milioni 38 na si 89 iliyosoma kwake
KWA HIYO KOSA LIMEFANYIKA KUTOKA 39M MPAKA 89M? KAZI IPO
Nyumba hiyo ina vyumba viwili vya kulala visivyokuwa na vyoo vya ndani, sebule moja pamoja na madirisha manne yaliyowekwa nondo na nyavu, huku sakafu yake ikiwa ya kawaida ya saruji na kuezekwa kwa bati
KAMA SIJAKOSEA DIZAINI YA SHULE HIYO NI KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI. JE HAWAJUI KWAMBA KUNA DESIGN YA SHULE ZA SEKONDARI? KWA SEHEMU KAMA IGUNGA NILITEGEMEA KAMA WATATUMIA MCHORO WENYE VYOO VYA NDANI.
Kwa mujibu wa taarifa fupi ya ujenzi iliyosomwa kwa kiongozi wa mbio za mwenge, mbali na sh milioni 89 gharama za nyumba hiyo, pia zimetumika sh .milioni 58.5 kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha maabara, sh. milioni 38.8 kwa ajili ya vyumba viwili vya madarasa na sh. milioni 23.9 kwa ununuzi wa samani
MILIONI 58.5 KWA AJILI YA UJENZI WA MAABARA? NAFIKIRI SIO MAABARA ZA ZAMANI YAANI ZENYE VYUMBA VITATU KWA AJILI YA BIOLOGY, CHEMISTRY NA PHYSICS.
Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya ukandarasi ya Elisha & Son Ltd ya mjini Igunga, iliyopewa kazi ya ujenzi wa majengo hayo, alipoulizwa gharama za nyumba ya mwalimu alisema hazizidi sh. milioni 50 na si chini ya milioni 40
TEN PERCENT NAHISI ILIKUWA NDANI YA HIZI PESA.
Kama wanasema ni sh. milioni 89 sasa unanifumbua macho labda kuna mkataba unaotuhusu sisi na ule unaohusu taarifa zao mbele ya umma lakini hizo gharama za nyumba hazifiki huko," alisema
HAPA PANA UKWELI SANA TU.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Igunga, Rustruka Turuka alipoulizwa gharama halisi ya jengo hilo, alielekeza swali hilo kwa Afisa Elimu Sekondari, Aloyce Kaziyareli ambaye alisema gharama zilizosomwa siku ya uzinduzi ndizo zinapaswa kufuatwa
WANARUSHIANA MPIRA HAO
Jana, mkuu wa wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu, alizungumza na gazeti hili na kukiri kuwaita badhi ya maofisa wa halmashauri katika ofisi yake kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa ubora wa mradi huo na fedha zilizotumika
INABIDI WATAFUTE WATAALAM WA NJE ILI WAJUE UKWELI ZAIDI
Alisema baada ya kuongea nao aliwaagiza kusitisha malipo kwa mkandarasi na kisha mthamini wa ujenzi wa halmashauri awasilishe taarifa yake ya kukubali jengo hilo la walimu kuwa na thamani ya sh. milioni 89
ANECHELEWA MKUU WA WILAYA ANGELIPWA MKANDARASI THENI BAADHI YA PESA ZINGERUDI KWA WATAALAM WA HALMASHAURI AKIWEMO DED
Huyu aliyepitisha BOQ ya fedha hizo tunamtaka ajieleze kwa kuwa jengo halilingani na thamani ya fedha iliyotajwa," alisema Kingu
MTU WA KWANZA KUJIELEZA NI DED NA MHANDISI WA WILAYA
Ndani kuna AC 12, Thamani za ndani zote zimenakishiwa kwa madini ya Alumas na Dhahabu,chezea wajanja weweee.....
Kwanini isiwezekane kama mifuko ya saruji quotation ilionesha serekali itauziwa tsh 30000 na tender ikapita anashangaa nini?Hebu aache siasa fungua nyumba kafanye mengine.
halafu unaweza kuta mjenzi wa hiyo nyumba ni mwanachama wa chadema halafu anasema serikali ya ccm iache ufujaji
View attachment 195418
Nyumba ya mil. 89/-MIRADI ya ujenzi katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, imeghubikwa na tuhuma za ufisadi, ambapo hivi karibuni imekabidhiwa nyumba ya mwalimu yenye vyumba viwili vya kulala na sebule, ikitajwa kugharimu sh. milioni 89, jamba ambalo limeibua utata na kumlazimu Mkuu wa wilaya hiyo, Elibariki Kingu kuingilia kati.
Gharama ya ujenzi wa nyumba hiyo katika shule ya sekondari Ichama kata ya Chabutwa ni sehemu ya matumizi ya kiasi cha sh. milioni 219 zilizotolewa na Serikali kuu kupitia mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.
Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumatano, umebaini kuwa mbali na kiasi hicho pia katika muendelezo wa matumizi ya fedha hizo, sh. milioni 8.6, zimetumiwa kwa ajili ya kujenga tanki la kuvunia maji ya mvua katika nyumba hiyo, hali inaibua maswali kwa wakazi wa Chabutwa kutokana na ubora wa nyumba yenyewe na gharama zinazotajwa kutumika.
Kutokana na utata huo, tayari mkuu wa wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu, ameingilia kati na kutaka malipo ya mradi huo yasitishwe huku akiagiza wataalam wa halmashauri kufanya tathmini upya kuthibitisha kama thamani ya fedha inalingana na ubora wa nyumba.
Oktoba 8 mwaka huu, wakati kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Rache Kasanda akiikagua nyumba hiyo ya mwalimu baada ya kuifunga, alisikika akisifia kuwa ni bora kwa kile alichoeleza kuwa haina dalili yoyote ya nyufa.
Gazeti hili lilipomhoji juu ya gharama zilizotajwa katika taarifa ya halmashauri kama zinarandana na ubora wa nyumba, Kasanda alisema wahusika walimueleza kuwa gharama zilizoandikwa katika taarifa zilikuwa zimekosewa na kwamba nyumba imegharimu sh. milioni 38 na si 89 iliyosoma kwake.
Wasaidizi wangu ulioongea nao awali waliniambia juu ya hilo na nikafuatilia na mkurugenzi ameniambia walikosea katika kuandika na kwamba gharama zake ni sh. milioni 38, alisema Kasanda akiwa katika kata ya Simbo.
Nyumba hiyo ina vyumba viwili vya kulala visivyokuwa na vyoo vya ndani, sebule moja pamoja na madirisha manne yaliyowekwa nondo na nyavu, huku sakafu yake ikiwa ya kawaida ya saruji na kuezekwa kwa bati.
Kwa mujibu wa taarifa fupi ya ujenzi iliyosomwa kwa kiongozi wa mbio za mwenge, mbali na sh milioni 89 gharama za nyumba hiyo, pia zimetumika sh .milioni 58.5 kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha maabara, sh. milioni 38.8 kwa ajili ya vyumba viwili vya madarasa na sh. milioni 23.9 kwa ununuzi wa samani.
Mmoja wa maofisa wa Kampuni ya ukandarasi ya Elisha & Son Ltd ya mjini Igunga, iliyopewa kazi ya ujenzi wa majengo hayo, alipoulizwa gharama za nyumba ya mwalimu alisema hazizidi sh. milioni 50 na si chini ya milioni 40.
Kama wanasema ni sh. milioni 89 sasa unanifumbua macho labda kuna mkataba unaotuhusu sisi na ule unaohusu taarifa zao mbele ya umma lakini hizo gharama za nyumba hazifiki huko, alisema.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Igunga, Rustruka Turuka alipoulizwa gharama halisi ya jengo hilo, alielekeza swali hilo kwa Afisa Elimu Sekondari, Aloyce Kaziyareli ambaye alisema gharama zilizosomwa siku ya uzinduzi ndizo zinapaswa kufuatwa.
Gharama ni hizo hata hiyo nyumba ndiyo gharama yake, sasa ukitaka kujua zimefikaje hayo ni maswali ya Mkandarasi, alisema Kaziyareli.
Jana, mkuu wa wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu, alizungumza na gazeti hili na kukiri kuwaita badhi ya maofisa wa halmashauri katika ofisi yake kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa ubora wa mradi huo na fedha zilizotumika.
Alisema baada ya kuongea nao aliwaagiza kusitisha malipo kwa mkandarasi na kisha mthamini wa ujenzi wa halmashauri awasilishe taarifa yake ya kukubali jengo hilo la walimu kuwa na thamani ya sh. milioni 89.
Kwa mujibu wa Kingu, baada ya hatua hiyo wataalam mbali mbali wataenda kufanya tathmini upya kuthibitisha kama nyumba iliyojengwa ina thamani ya fedha iliyotajwa.
Huyu aliyepitisha BOQ ya fedha hizo tunamtaka ajieleze kwa kuwa jengo halilingani na thamani ya fedha iliyotajwa, alisema Kingu.
Chanzo: Tanzania Daima
Hivi wewe engineer kweli??; Na kama una uzoefu wa ujenzi hata kama materials yanatoka mbali hiyo nyumba inaweza kufika thamani hiyo kweli?? Na katika hali ya kawaida vipimo vya nyumba ya vyumba viwili vya kulala na sebule utashindwa ku estimate?? Chumba meter 3 kwa 4 na sebule ya meter 5 kwa 5 nk unashindwa ku estimate??
Wewe siyo engineer wewe na kama ni engineer basi rudi darasani! Hata kama vifaa vimetoka mbali, within the same district kwa nyumba kama hiyo kitu cha kutoka mbali sana ni mchanga tu hapo, kulingana na mazingira hayo, lakini bati, rangi, mbao, nyavu za madirisha na nondo zinapatikana kwa urahisi tu! Cement pia!.
Mafundi wa mikoani hawana bei ya kutisha! Usitusumbue hapa wewe!
DC naye kaleta mpya, huo mradi umeingia kwenye taarifa ya wilaya-mkoa-taifa. Na kwa hiyo katika kilele cha mbio za mwenge mgeni rasmi alipokea taarifa ya miradi iliyozinduliwa ikiwa na mapungufu kiasi hiki!? Sasa swali dogo hiyo miradi wakati inapendekezwa DC alikuwa wapi? Lingine dogo je, taarifa kama hizi ni ngapi zilizopotoshwa?!
Ndani ya serikali ya CCM yote hayo yanawezekana...