Nyumba ndogo, we acha tu!

Nyumba ndogo, we acha tu!

Heee jamani niulize mm kidumu kimebeba mume wangu amezaa nae mtoto nimekuja kugundua wakati mtoto ameshazaliwa ana miezi sita sikuamini macho yangu kuna usemi unasema:mwanamke kujiamini dhubutu yako lazma ukae kama yule mnyama anaitwa Swala vinginevyo yatakukuta yaliyonikuta mm inauma sana,ila nashukuru Mungu nilikaza roho nikatengana nae ila cha kushangaza bado ananifuatafuata sijui kidumu kimepunguza speed.

dah, I feel sorry 4 u.lkn ww noma ukaamua kuondoka???? mi ctaki kulea mtt wa mtu akizaa alee tu hukohuko ctaki hata kuckia
 
Leo nimeamua kupasua jibu. Nalishika pembeni na kulipasua PHWAAA! Mi mke wangu alikua na vituko vya kila aina. Nililalamika sana na hatimae nikaamua kujitwisha mzigo wangu na kuukubali. Ila wakati wote wa vituko hivyo, niliamua kuwa na nyumba ndogo 2, moja kati yao alikua kwenye ndoa (Mrembo mzuri aliolewa na lijamaa kazi yake kulewa tu na kuacha mtoto wa watu kulala tu, mi nikasikiliza kulio cha huyo mrembo nikaamua kumsaidia).

Kusema kweli, ndoa nyingi zina matatizo kweli. Usione watu watatembea barabarani! Wanawake waliowengi hawajui kujali waume zao. Kazi kujiremba kucha tu na nywele. Kupika hawajui, kufua ndo usiseme, hata kukagua nguo za waume zao tu lahasha! Halafu majibu kama mwanamke ameweka kidaftari mdomoni na kufungua ukurasa baada ya ukurasa. Wapo wanaume wasiojali wake zao, esp wale walevi kupindukia. Wengine wanamajivuno kwa wake zao utafikiri wanashindana na nao. Mke sio wakushindana nae coz yuko chini ya mme wake. Dini zote na tamaduni zinasisitiza hivyo!

Anyway, niliamua kuwa mpole na kuachana na nyumba ndogo zote. Niliona kama nimepata ulemavu fulani wa kutoweza kuishi bila nyumba ndogo. Pia nimeacha kabisa kusikiliza malalamiko ya wanawake walio kwenye ndoa, wengine waongo kabisa! "Utaskia oooh baba Manyusi hanijali, mara ngweeee, Baba Nyumbafu hajui kuninanii" Kumbe washezi wakubwa nyie.... Wanaume tunawajali sana, lakini wapi, hamtulii. Mfano pamoja na kuwa na kiherehere chote, mke wangu hana kitu anachokosa kuanzia mbunye hadi gari...Kumbe nilistuka makundi yalikua yanamharibu sana....na wazazi wake wanamatusi kwenda mbele. Wao matusi ni kama mate tu. Hata mke wangu wanamtukana nikiwepo! Utaskie we Jane, pumbafu lete kibakuli hapa! Mara we Hamisi, shenzi kuja hapa usalimie mkwe wako!

They say charity begins at home. Sikujua mke wangu aliishi mazingira hayo na kumbadilisha mtu lazima uwe mpole sana na uwe nae karibu. Ndivyo nilivyoachana na nyumba ndogo na kuwa karibu sana na mke wangu. Leo amebadilika na tunaendana! Nyumba ndogo zilinifanya nisitulie home! Kila weekend niko balabalani kuwafuata Kimara, mara Segerea, mara Kinondoni mweee wanawake mwee! Nilikua kama mwendawazimu kukimbizana na nyumba ndogo. Wanaume wenye nyumba ndogo wanateseka sana ila hawajui hilo. Wanaona bora wateseke kuliko kumaliza matatizo ya kwenye ndoa zao, sawa na wanawake wenye shida kwenye ndoa. Vidumu haviwezi kumaliza matatizo hayo. Jitambue, jishushe na zungumza ndo suluhu ya kila kitu.

Bila shaka mkeo ni mchagga!

Anyway,Hongera kwa kubadilika brother........!
 
Ni kweli, pengine nami nilikuwa na makosa. Kutokuwa karibu mara nyingi kunaleta matatizo. Nilivyoamua kuchukua hatua kuachana na vidumu, nilijikuta nikawa karibu na mke wangu, nikampa muda wakumsikiliza zaidi na kutulia home. Nae akabadilika. Unajua sio rahisi kuachana na vidumu maana vinakoleza vibaya mno!

Waoh, l am so happy for you. Naimani wengine watajifunza kutoka kwako. Hakuna mtu aliyeumbwa monster, siku zote kuna sababu (evil) na upendo, care, understanding and communications ni soln.
 
Hapo sasa! Usikute kesha ukwaa ndio kaamua kutulizana ili amuambikize mkewe

Hahaha, we acha tu! Mi niko fit na majuzi tu tumekwenda kupima afya zetu. Kwani nyie mnasubiri muumwe ndo mkapime? I do it so often!
 
Kwani kwenye hayo mabucha nyama ilikuwa ile ile au tofauti?

Hayo tuyaache kwanza..... Wataelezea wengine ambao kazi yao ni kutafuta umaarufu, na sio wale tunliokuwa tunakimbia shida nyumbani
 
Jamani u have made my morning, nimechekaaaaaaaaaa! Eti ulikuwa unaenda leo segerea, kesho cjui wapi, wenzio wanafuata nyumba ndogo mpaka kiluvya, hahahahha wengine kibaha! Chezeiya mbunyeeeee weye! Ila umenichekeshajeeeeeeeeeee???
 
Jamani u have made my morning, nimechekaaaaaaaaaa! Eti ulikuwa unaenda leo segerea, kesho cjui wapi, wenzio wanafuata nyumba ndogo mpaka kiluvya, hahahahha wengine kibaha! Chezeiya mbunyeeeee weye! Ila umenichekeshajeeeeeeeeeee???

Imagine mimi kimbizana kimbizana ya Segerea, kinondoni, mara Kimara nusura iniletee uendawazimu, Je hao wa Kiluvya na Kibaha au bagamoyo, wengine hadi huko Kisarawe si ndo wamekuwa walemavu wa akili kabisa? Mi nimekoma na wanaume wenzangu nataka sana waisome thread hii. Lengo wazungumze matatizo yao wayamalize. Watu wawili tu wanaweza kumaliza matatizo ya ndani ya ndoa nao ni Mme na Mke basiiii!
 
yani umenifanya tu nicheke..au ulikokimbilia ulikuta yaleyale cha zaidi uliongeza bajeti?
 
Back
Top Bottom