Nyumba ndogo, we acha tu!

Wiyelelee

JF-Expert Member
Nov 9, 2012
1,071
347
Leo nimeamua kupasua jibu. Nalishika pembeni na kulipasua PHWAAA! Mi mke wangu alikua na vituko vya kila aina. Nililalamika sana na hatimae nikaamua kujitwisha mzigo wangu na kuukubali. Ila wakati wote wa vituko hivyo, niliamua kuwa na nyumba ndogo 2, moja kati yao alikua kwenye ndoa (Mrembo mzuri aliolewa na lijamaa kazi yake kulewa tu na kuacha mtoto wa watu kulala tu, mi nikasikiliza kulio cha huyo mrembo nikaamua kumsaidia).

Kusema kweli, ndoa nyingi zina matatizo kweli. Usione watu watatembea barabarani! Wanawake waliowengi hawajui kujali waume zao. Kazi kujiremba kucha tu na nywele. Kupika hawajui, kufua ndo usiseme, hata kukagua nguo za waume zao tu lahasha! Halafu majibu kama mwanamke ameweka kidaftari mdomoni na kufungua ukurasa baada ya ukurasa. Wapo wanaume wasiojali wake zao, esp wale walevi kupindukia. Wengine wanamajivuno kwa wake zao utafikiri wanashindana na nao. Mke sio wakushindana nae coz yuko chini ya mme wake. Dini zote na tamaduni zinasisitiza hivyo!

Anyway, niliamua kuwa mpole na kuachana na nyumba ndogo zote. Niliona kama nimepata ulemavu fulani wa kutoweza kuishi bila nyumba ndogo. Pia nimeacha kabisa kusikiliza malalamiko ya wanawake walio kwenye ndoa, wengine waongo kabisa! "Utaskia oooh baba Manyusi hanijali, mara ngweeee, Baba Nyumbafu hajui kuninanii" Kumbe washezi wakubwa nyie.... Wanaume tunawajali sana, lakini wapi, hamtulii. Mfano pamoja na kuwa na kiherehere chote, mke wangu hana kitu anachokosa kuanzia mbunye hadi gari...Kumbe nilistuka makundi yalikua yanamharibu sana....na wazazi wake wanamatusi kwenda mbele. Wao matusi ni kama mate tu. Hata mke wangu wanamtukana nikiwepo! Utaskie we Jane, pumbafu lete kibakuli hapa! Mara we Hamisi, shenzi kuja hapa usalimie mkwe wako!

They say charity begins at home. Sikujua mke wangu aliishi mazingira hayo na kumbadilisha mtu lazima uwe mpole sana na uwe nae karibu. Ndivyo nilivyoachana na nyumba ndogo na kuwa karibu sana na mke wangu. Leo amebadilika na tunaendana! Nyumba ndogo zilinifanya nisitulie home! Kila weekend niko balabalani kuwafuata Kimara, mara Segerea, mara Kinondoni mweee wanawake mwee! Nilikua kama mwendawazimu kukimbizana na nyumba ndogo. Wanaume wenye nyumba ndogo wanateseka sana ila hawajui hilo. Wanaona bora wateseke kuliko kumaliza matatizo ya kwenye ndoa zao, sawa na wanawake wenye shida kwenye ndoa. Vidumu haviwezi kumaliza matatizo hayo. Jitambue, jishushe na zungumza ndo suluhu ya kila kitu.
 
.............safiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!! hongera sana kaka yangu kwani hapo ulitumia akili na hekima. Hili liwe pia funzo kwa wanandoa wote....!!
 
siyo kwamba maisha yamepanda umeshindwa kuhudumia nyumba zote?.... hongera kwa kutoka huko

Wala, nilichokuwa natafuta ni amani. Kwa taarifa yako tu maisha ndo nayala ile mbaya na hela ipo ya kumwaga! Kwanza elimu ninayo ya kutosha, then kazi yangu nzuri na nalipwa vzr
 
Wiyelele said:
Kusema kweli, ndoa nyingi zina matatizo kweli.
Usione watu watatembea barabarani! Wanawake waliowengi hawajui kujali waume zao.
Kazi kujiremba kucha tu na nywele. Kupika hawajui, kufua ndo usiseme, hata kukagua nguo za waume zao tu lahasha! Halafu majibu kama mwanamke ameweka kidaftari mdomoni na kufungua ukurasa baada ya ukurasa.
Wapo wanaume wasiojali wake zao, esp wale walevi kupindukia. Wengine wanamajivuno kwa wake zao utafikiri wanashindana na nao. Mke sio wakushindana nae coz yuko chini ya mme wake. Dini zote na tamaduni zinasisitiza hivyo!

Mkuu nimeyasoma haya malalamiko hapa lakini nikajiwa na swali moja tu.

Je kabla ya kuoana (kuoa au kuolewa), hizo tabia hazikuonekana???

NB:
Mwanzo hutabiri mwisho
 
Inaelekea wewe una upendo sana na mkeo. Ni wachache sana wanaweza kujirudi baada ya kunogea na nyumba ndogo. ila basi punguza masimango kwa wanawake, mbona wanawake wanaojali waume zao ni wengi tu
 
Mkuu nimeyasoma haya malalamiko hapa lakini nikajiwa na swali moja tu.

Je kabla ya kuoana (kuoa au kuolewa), hizo tabia hazikuonekana???

NB:
Mwanzo hutabiri mwisho


Ukitaka kujua tabia ya mwanamke, mweke ndani....Kila mmoja kabla hajaoa au kuolewa huficha kucha zake. Hata mvuta sigara anasafisha meno yake na colgate! Akioa au kuolewa mswaki ndo basi!
 
Uzi wako japo unatia matumaini umeniacha na maswali....

Ni nini kimemfanya mkeo abadilike?

Wewe kuachana na nyumba ndogo au?

Isije ikawa hakuwa na shida yeyote ila ulikuwa unalazimisha ili ku justfy cheating...

Yani mtu anabadili tabia tu ghafla?
 
safi sana,wanawake wako wengi mno inabidi tuwasaidie kwa kuwahifadhi.
Nalog off
 
mmmh,,nyumba ndogo siachi,,uyu mwanamke angu nikijishusha tuu na kuwa mdogo,,mnyakyusa nitapigwa adi ki.,d,o,l,e
CHEZEA MPALESTINA...ACHA KABISAAA
 
Ratio kulingana na tafiti ni kuwa kila watu binadamu kumi sita ni wanawake na wanne ni wanaume. Sasa tusaidiane jee hawa wanawake wawili watapata mambo toka wapi? Ni swali tu jamani.
 
hahaha Tafuta pesa mkuu itakuwa umeishiwa ndio maana umeona bora kupunguza majukumu
 
Nimefurahi kusoma habari yako, na wewe kama mfano mzuri uliejaribu na kuona bora uweke nyumba na ndoa yako sana nakupa hongera.
Natumaini wanaume wengine watafuata mfano wako, as watasoma na kufikiria na kujiona wanakosea na wao ni wakusaidia maisha ya home kubadilika.

Ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom