Nyote mnaosema kuwa Simba SC jana ilionewa sana na Refa ( Mwamuzi ) tafadhali nijibuni upesi haya Maswali yangu yafuatayo

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Je,

1. Refa ndiyo alikipanga Kikosi kile cha wasiwasi cha Simba SC Jana?

2. Refa ndiyo alimwambia Mshambuliaji wetu Mpuuzi Chris Mugalu acheze Faulo za Kipumbavu ambazo zilitugharimu Kiufundi hasa pale alipotolewa kwa Kadi Nyekundu?

3. Refa ndiyo alimwambia Kocha wa Simba SC Pablo Franco Martin ampange na aendelee kumuacha Uwanjani Kiungo aliyechemsha muda Wote Jana Saido Kanoute?

4. Refa ndiyo alimfanya Mshambuliaji wetu Simba SC Pape Ousmane Sakho muda Wote awe anarukaruka tu Uwanjani na Kupiga Chenga zake zisizo na Faida na akinyang'anywa Mpira hakabi na muda Wote tu anatutafunia Bubble Gum ( Bigjii ) yake?

5. Refa ndiyo alikuwa akiwaambia Kipa Aishi Manula na Beki Mpenda Sifa za Kijinga hadi anakera Henock Inonga Baka wawe wanapoteza muda mara kwa mara kwa Kujiangusha mpaka kuna wakati Beki Mwenzake Shomary Kapombe alienda Kumfokea kwa huo Upuuzi wake na akatulizwa na Beki Pascal Serge Wawa?

6. Refa ndiyo aliwaambia Wachezaji wa Simba SC ( hasa Mabeki ) kuendelea na Kosa lile lile ( Udhaifu ule ule ) wa kutokucheza Mipira ya Krosi ambalo limeshakuwa Sugu Kwetu hadi Mshambuliaji wa Orlando Pirates FC akaruka Freely Hewani na Kupiga Kichwa Kizuri na Goli Kuingia?

7. Refa ndiyo alimwambia Kocha wa Simba SC aanze Kumpanga Mchezaji wa Kiungo wa Simba SC Jonas Mkude ( ambaye hana Rekodi ya Upigaji Penati Simba SC ) aanze Kupiga badala ya kuanza na wale Wazoefu na wenye uhakika Siku zote? au kuna Goli lolote lile labda Simba SC tulilifunga na Refa akalikataa?

Nawasubiri majibu yenu huku nikiwa kama Mwanamichezo na mwana Simba SC lia lia nikimalizia kwa kusema kuwa tumejitahidi ila tumetolewa Kimchezo, tujipange zaidi kwa Mashindano yajayo, tusikate Tamaa Mpira ndivyo ulivyo ila nitakuwa ni mwenye Furaha muda wowote kuanzia sasa nikisikia Kocha Mkuu wa Simba SC Pablo Franco Martin na Msaidizi wake Suleiman Abdallah Matola na Meneja wa Timu ( Simba SC ) Patrick Rweymamu wakifutwa Kazi na Simba SC iajiri Wapya wa Kuwazidi uwezo na Kuziba hizo Nafasi zao.

Binafsi kama MINOCYCLINE kwa nilivyoutizama Mpira ule kwa Umakini wangu wote na mkubwa nimeona kuwa Refa ( Mwamuzi ) alitubeba Simba SC kuliko Maelezo hasa katika Matukio kama Manne hivi yakiwemo ya Penati Mbili baada ya Mabeki Wetu Kuunawa na Nidhamu mbovu ya mara kwa mara aliyokuwa akiionyesha Kiungo Wetu Jonas Mkude ambapo kama angeamua Kutanguliza Sheria 17 za Soka na kutotumia Ubinadamu jana hali ingekuwa mbaya na HATARI zaidi Kwetu.

Imeisha hiyo........!!!!
 
8) Refa ndiye aliyewaambia mkachome ile karatasi ya juju pale uwanjani kabla ya mchezo kuanza?

9) Refa ndiye aliyemkataza kocha wetu Pablo kutomchezesha mchezaji wetu mahiri na mwenye uwezo mkubwa wa kukimbia kama digidigi, na pia kuruka viunzi uwanjani kama Usein Bolt #Kibu Dennis aka Kibunenga?

10) Refa ndiye aliyesababisha tuanzishe timu ya mabeki tu uwanjani, na kumgeuza mshambuliaji wetu mahiri Chris Mugalu kuwa kiungo mkabaji?
 
Simba wasitafute mchawi. Mwaka huu fowadi imewagharimu sana Simba kwenye CL na hata kwenye NBC ligi. Hata takwimu za mabao kwa washambuliaji zinaonyesha wazi kabisa kuwa eneo la usahambuliaji lilikuwa ni tatizo. Na kwenye NBC ligi pia imeisha hiyo. Waongeze tu nguvu kwenye kombe la Azam basi. Kwa fowadi waliyokuwa nayo hata kufika robo fainali Afrika ni jambo la kujivunia sana.

Wasirudie makosa waliyofanya wakati wa usajili mwaka jana. Kuanzia Sasa waache mihemuko wajikite kutafuta mafowadi wawili wa nje na mmoja wa ndani wa kuwapa matokeo kabla hawajafikiria kusajili wachezaji wa nafasi nyingine.
 
Back
Top Bottom