Nyota yake ya kisiasa iliyong'ara sana mwanzoni, imefifia mno kwa sasa kwenye medani

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,170
11,572
Ni kijana alieibuka na kung'ara mno katika medani za siasa za Tanzania. alichomoza katika awamu ya4 chini ya Rais wa wakati huo JK.

Kwa hakika binafsi niliwahi kuchunguza na mpaka wa leo, sijabaini, sijaona wala sijafahamu, ni nini hasa kiliwavutia sana wananchi ikiwa ni pamoja na mimi mwenyewe kumzungumizia na kumuamini sana kijana huyu machachari na hata kumfikiria kwa nafasi za juu za uongozi nchini, katika siku za usoni.

Kwakweli, nilichokiona kwake dhahiri bila uchunguzi ni Natural Love.

Aina hii ya kupendwa huwatokea watu mbalimbali, mtu anajikuta tu from no where anapendwa na wengi. kijana huyu mwenye bahati ya pekee, alipendwa na wananchi bure bila sababu ya msingi na tukashuhudia na kushangilia kijana akipewa nafasi muhimu za juu za uongozi serikalini, kama Naibu waziri na baadae Waziri Kamili.

Kijana aliwahi kuzifanyia kazi wizara kadhaa ikiwa ni pamoja na Mawasilino, Mazingira, Nishati, Mambo ya Nje n.k.

Lakini waungwana, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Hivi ni nini au ni kipi leo hii unaweza kusema kijana huyu alibuni au alitekeleza kikasaidia nchi na wananchi, hata aaminiwe na kukumbatiwa kiasi hiki, na kupewa nafasi za juu Serikalini?

Au anachokipata ni malipo ya fadhila kwa wema aliwahi kuutenda huko nyuma dhidi ya wanaompa nafasi na kumwamini licha ya kutokua na maajabu?

Najaribu kubaini ni kipi au ni nini kinaweza kumtambulisha kijana huyu kwa haraka kwasasa?

Bado sioni ila naona natural love pekee na mgao wa umeme pekee.

kujiamini kwake kupindukia, huku akiwa hana ubunifu wala uthubutu wa kusema na kutenda umenivutia kumfuatilia zaidi kujua ni nini siri ya kubakizwa serikali licha ya empty records kwenye wizara nyingine, lakini record mbovu zaidi ya utendaji katika wizara ya nishati. a otally failed ministry on his tenure.

Labda kuhusu mazingira, alijitahidi kupiga marufu matumizi ya mifuko ya rambo/naylon, ambayo kwasasa imerejea kwa sura nyingine na inaathiri mazingira zaidi hata ya mifuko ya Rambo. Au ni usafi siku za weekend nao sijui uliishia wapi?

Nadhani concentration yake inasukumwa na uchu, tamaa ya mali na madaraka. alijikita na kujisahau zaidi, kuvuna pesa na kutafuta uungwaji mkono nia yake ya kutamani uongozi wa juu, huku akisahau jukumu lake muhimu la utatuzi wa changamoto za wizara ili kusudi wananchi wapate huduma bora na za uhakika za nishati.

Huenda umuhimu wake, uko zaidi kwenye chama chake. Serikalini ni mahala tu, pa kupumzikia, kujikusanya na kujiimarisha kisiasa.

Nionavyo mie, nyota ya kisiasa ya muungwana huyu imefifia karibu kuzimika kwenye medani za siasa za Tanzania.

Si Unajua namzungumzia nani...
 
ni kijana alieibuka na kung'ara mno katika medani za siasa za Tanzania. alichomoza katika awamu ya4 chini ya Rais wa wakati huo JK.

huyu imefifia karibu kuzimika kwenye medani za siasa za Tanzania.

si unajua namzungumzia nani.......
Hizi siasa za vigogo na watoto wao sio nzuri. Kila kiongozi anataka mtoto wake naye awe kiongozi, hapana!
 
Hizi siasa za vigogo na watoto wao sio nzuri. Kila kiongozi anataka mtoto wake naye awe kiongozi, hapana!
Huyu hapa
20230926_162643.jpg
 
Mwanzoni ulianza vizuri kabisa, ukaweka code za kutosha.
Hapo katikati umekuja kuvuruga na maana yote imepotea!

‘Kijana’ kamalizwa na wizara ile ya lawama. Ila bado sana kusema kamalizika kisiasa, wana mbinu nyingi hao watu.
Kama Lowassa alirudi na kashfa yote ile na akatikisa itakuwa yeye?
 
ni kijana alieibuka na kung'ara mno katika medani za siasa za Tanzania. alichomoza katika awamu ya4 chini ya Rais wa wakati huo JK.

kwa hakika binafsi niliwahi kuchunguza na mpaka wa leo, sijabaini, sijaona wala sijafahamu, ni nini hasa kiliwavutia sana wananchi ikiwa ni pamoja na mimi mwenyewe kumzungumizia na kumuamini sana kijana huyu machachari na hata kumfikiria kwa nafasi za juu za uongozi nchini, katika siku za usoni.

kwakweli, nilichokiona kwake dhahiri bila uchunguzi ni Natural Love.
aina hii ya kupendwa huwatokea watu mbalimbali, mtu anajikuta tu from no where anapendwa na wengi. kijana huyu mwenye bahati ya pekee, alipendwa na wananchi bure bila sababu ya msingi na tukashuhudia na kushangilia kijana akipewa nafasi muhimu za juu za uongozi serikalini, kama Naibu waziri na baadae waziri Kamili.

Kijana aliwahi kuzifanyia kazi wizara kadhaa ikiwa ni pamoja na Mawasilino, Mazingira, Nishati, Mambo ya Nje n.k

Lakini waungwana, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Hivi ni nini au ni kipi leo hii unaweza kusema kijana huyu alibuni au alitekeleza kikasaidia nchi na wananchi, hata aaminiwe na kukumbatiwa kiasi hiki, na kupewa nafasi za juu Serikalini?

Au anachokipata ni malipo ya fadhila kwa wema aliwahi kuutenda huko nyuma dhidi ya wanaompa nafasi na kumwamini licha ya kutokua na maajabu?.

Najaribu kubaini ni kipi au ni nini kinaweza kumtambulisha kijana huyu kwa haraka kwasasa?
Bado sioni ila naona natural love pekee na mgao wa umeme pekee.

kujiamini kwake kupindukia, huku akiwa hana ubunifu wala uthubutu wa kusema na kutenda. umenivutia kumfuatilia zaidi kujua ni nini siri ya kubakizwa serikali licha ya empty records kwenye wizara nyingine, lakini record mbovu zaidi ya utendaji katika wizara ya nishati. a otally failed ministry on his tenure.

Labda kuhusu mazingira, alijitahidi kupiga marufu matumizi ya mifuko ya rambo/naylon, ambayo kwasasa imerejea kwa sura nyingine na inaathiri mazingira zaidi hata ya mifuko ya Rambo. Au ni usafi siku za weekend nao sijui uliishia wap?

nadhani concentration yake inasukumwa na uchu, tamaa ya mali na madaraka. alijikita na kujisahau zaidi, kuvuna pesa na kutafuta uungwaji mkono nia yake ya kutamani uongozi wa juu, huku akisahau jukumu lake muhimu la utatuzi wa changamoto za wizara ili kusudi wananchi wapate huduma bora na za uhakika za nishati.

Huenda umuhimu wake, uko zaidi kwenye chama chake.
Serikalini ni mahala tu, pa kupumzikia, kujikusanya na kujiimarisha kisiasa.

nionavyo mie, nyota ya kisiasa ya muungwana huyu imefifia karibu kuzimika kwenye medani za siasa za Tanzania.

si unajua namzungumzia nani.......
Kijana Hana nyota yoyote inayong'aa!!

Kilichofanyika ni Hila, mtu Hana karma ya uongozi, anakwenda Kwa walozi mnaowaita wataalamu, anakwiba nyota za watu wenye kaliba na karma za uongozi,

Akishakwiba anahamishia kwake, aliyeibiwa uiitayo nyota anabaki kifungoni, ni sawa tu ukimwita msukule au kichaa.

Ghafula utaanza kumwona milango ijimfungukia mwiba Karma za wengine nk nk.

Kilichotokea nw, wapo najemedari, raia wa Mbinguni, wamekwenda kuibomoa magereza na vibuyu walimofungwa waibiwa nyota/karma,KIBALI, na baada ya kubomoka magereza hayo, wamewaweka huru waibiwa KIBALI!!

Matokeo yake, waiba hatma wanafifia na KURUDIA Hali Yao ya asili.

Na SOON utaanza ona wenye karma na KIBALI halisi Toka Kuzaliwa wakiinuka kurudi mahala Pao na Nchi itastawi saana.

Rejea thread; Macho ya kinabii yatumike kuboresha vetting zetu nchini -Rabbon.

Amen
 
nakubali nabii,sina cha kuongeza
 
Mwanzoni ulianza vizuri kabisa, ukaweka code za kutosha.
Hapo katikati umekuja kuvuruga na maana yote imepotea!

‘Kijana’ kamalizwa na wizara ile ya lawama. Ila bado sana kusema kamalizika kisiasa, wana mbinu nyingi hao watu.
Kama Lowassa alirudi na kashfa yote ile na akatikisa itakuwa yeye?
sure!!
 
Back
Top Bottom