Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 8,706
- 11,970
Ni kijana alieibuka na kung'ara mno katika medani za siasa za Tanzania. alichomoza katika awamu ya4 chini ya Rais wa wakati huo JK.
Kwa hakika binafsi niliwahi kuchunguza na mpaka wa leo, sijabaini, sijaona wala sijafahamu, ni nini hasa kiliwavutia sana wananchi ikiwa ni pamoja na mimi mwenyewe kumzungumizia na kumuamini sana kijana huyu machachari na hata kumfikiria kwa nafasi za juu za uongozi nchini, katika siku za usoni.
Kwakweli, nilichokiona kwake dhahiri bila uchunguzi ni Natural Love.
Aina hii ya kupendwa huwatokea watu mbalimbali, mtu anajikuta tu from no where anapendwa na wengi. kijana huyu mwenye bahati ya pekee, alipendwa na wananchi bure bila sababu ya msingi na tukashuhudia na kushangilia kijana akipewa nafasi muhimu za juu za uongozi serikalini, kama Naibu waziri na baadae Waziri Kamili.
Kijana aliwahi kuzifanyia kazi wizara kadhaa ikiwa ni pamoja na Mawasilino, Mazingira, Nishati, Mambo ya Nje n.k.
Lakini waungwana, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Hivi ni nini au ni kipi leo hii unaweza kusema kijana huyu alibuni au alitekeleza kikasaidia nchi na wananchi, hata aaminiwe na kukumbatiwa kiasi hiki, na kupewa nafasi za juu Serikalini?
Au anachokipata ni malipo ya fadhila kwa wema aliwahi kuutenda huko nyuma dhidi ya wanaompa nafasi na kumwamini licha ya kutokua na maajabu?
Najaribu kubaini ni kipi au ni nini kinaweza kumtambulisha kijana huyu kwa haraka kwasasa?
Bado sioni ila naona natural love pekee na mgao wa umeme pekee.
kujiamini kwake kupindukia, huku akiwa hana ubunifu wala uthubutu wa kusema na kutenda umenivutia kumfuatilia zaidi kujua ni nini siri ya kubakizwa serikali licha ya empty records kwenye wizara nyingine, lakini record mbovu zaidi ya utendaji katika wizara ya nishati. a otally failed ministry on his tenure.
Labda kuhusu mazingira, alijitahidi kupiga marufu matumizi ya mifuko ya rambo/naylon, ambayo kwasasa imerejea kwa sura nyingine na inaathiri mazingira zaidi hata ya mifuko ya Rambo. Au ni usafi siku za weekend nao sijui uliishia wapi?
Nadhani concentration yake inasukumwa na uchu, tamaa ya mali na madaraka. alijikita na kujisahau zaidi, kuvuna pesa na kutafuta uungwaji mkono nia yake ya kutamani uongozi wa juu, huku akisahau jukumu lake muhimu la utatuzi wa changamoto za wizara ili kusudi wananchi wapate huduma bora na za uhakika za nishati.
Huenda umuhimu wake, uko zaidi kwenye chama chake. Serikalini ni mahala tu, pa kupumzikia, kujikusanya na kujiimarisha kisiasa.
Nionavyo mie, nyota ya kisiasa ya muungwana huyu imefifia karibu kuzimika kwenye medani za siasa za Tanzania.
Si Unajua namzungumzia nani...