Makonda na Januari wana nyota kali sana

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Kwema Wakuu!

Bila kujadili ubora na udhaifu wao yaani Makonda na Januari. Kitu pekee ambacho nimekiona ni kuwa Wananyota Kali Sana.

Moja ya dalili ambayo itakuonyesha wewe au mtu fulani ananyota kali basi ni mambo mawili tuu, Moja kusemwa Sana iwe kwa Mazuri au kwa Mabaya.

Kusemwa sana inamaanisha kuonekana sana. Huwezi kusemwa kama hauonekani. Kuonekana maana yake unang'aa sana.

Ukitaka kujua wewe nyota yako haing'ai sana basi fanya jambo lolote liwe zuri au baya. Ukiona umefanya lakini Watu wapo kama hawajaliona basi jua nyota yako ipo chini sana.

Lakini ukiona wanashangilia sana au wanapiga mayowe sana jua nyota yako iko juu mno.

Ndicho ambacho kinatokea kwa Makonda na Januari. Hayo mengine ni siasa na mambo yake.

Nyota inapong'aa Watu huweza kukupenda bila sababu. Halikadhalika kukuchukia bila sababu.

Kwa sababu kama ni makosa sio ajabu viongozi au Watu wengi wanafanya makosa tena wengine wamekuzidi lakini kwa nini wewe ndio uchukiwe au upigiwe makelele zaidi?

Au kama ni mazuri umefanya wapo wanaofanya mazuri kukushinda lakini kwa nini kwenye kupongezwa wewe ndio unaoongozwa zaidi? Hiyo ndio maana ya nyota kali.

Ni ngumu sana kumpuuza mtu mwenye nyota Kali. Yaani kumkaushia na kujifanya hujamuona hiyo wengi wanashindwa.

Lazima mdomo uwe na kiherehere kwa aidha kumsifia au kumlinda. Lazima moyo uwe na kiherehere cha aidha kumpenda au kumchukia.

Sisi Watibeli pekee ndio Watu wenye uwezo wa kudhibiti midomo na mioyo yetu. Kwa sababu tunaongozwa na HAKI, UPENDO, KWELI NA AKILI.

Nawatakia Jumatatu njema
 
Back
Top Bottom