SI KWELI Nyomi mikutano ya Samia Mbeya

SI KWELI Nyomi mikutano ya Samia Mbeya

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Ni wazi ukipita kwenye mitandao ya jamii hasa X, JF na FB unaweza kudhania Samia hapati hata kura 100. Lakini maisha kwa ground ni tofauti kabisa. Ni wakati sasa Mange Kimambi na Polepole wajitathmini. Watanzania hawadanganyiki, kazi ya Samia wanaiona. Njooni mniue
Mange Mikutano.jpg
 
Tunachokijua
Mange Kimambi amejitanabaisha kama mwanaharakati wa masuala mbalimbali hususan ya kisiasa. Amekuwa akizungumzia mambo mengi ya kisiasa yanayoendelea nchini Tanzania.

Madai

Hivi karibuni kumeibuka ujumbe ama chapisho linaloonekana kuchapishwa katika ukurasa wa mtandao wa X wenye utambulisho wa Mange Kimambi, Tazama hapa. Chapisho hilo linaandika;

Kiukweli Watanzanua mnakera, mnajaza comments hapa na bado mnajaza mikutano ya CCM. Hapa ni Mbeya leo (Inafutwa).

Je, ni kweli chapisho hilo limeandikwa na Mange Kimambi?

Ufuatiliaji wa kina uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa chapisho hilo si la kweli.

Utafutaji kwa kutumia maneno muhimu yaani Keyword Search, JamiiCheck imejiridhisha kuwa hakuna ujumbe wowote katika ukurasa wa X wenye utambulisho unaonekana kwenye chapisho hilo ambao umechapishwa, hivyo basi chapisho hilo ni la kughushi.

Chapisho hilo linalosambazwa ni la kughushi kwani linakosa baadhi ya vitu muhimu ambavyo vinaonekana katika ukurasa wa X. Mathalani rejelea sehemu ya chini ambayo inaonesha muda na tarehe, inakosekana sehemu inayoonesha views (waliotazama), rejelea pia mpangilio wa tarehe.

Aidha ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa hadi wakati taarifa hii inaandikwa Septemba 05, 2025 ukurasa huo ulichapisha taarifa kwa mara mwisho Juni 16, 2025 na ku repost kwa mara ya mwisho Agosti 10, 2025 ambayo ndiyo taarifa ya mwisho inayoonekana ukiondoa 'Pinned post'. Lakini pia taarifa hiyo haipo katika ukurasa wake wa X ambao ndiyo amekuwa akiutumia mara kwa mara.
Katiba mbaya ya CCM inafahamika tangu enzi za Nyerere. JK alitumia Tsh 400 Billion na Katiba hatukuiona. Magufuli alisema Katiba haikuwa ahadi yake ya Kampeni.

Samia kasema ataleta Katiba Mpya akichaguliwa. Ubaya uko wapi hapo?

Ubaya uko hapa:

"Tangia 2021 kavuta miguu kuhusu mabadiliko kwa hila ili kwa namna yoyote awe kitini hadi angalau 2030."

Yaangalie maneno yaliyopigiwa mstari kama mwenye akili timamu.

Tatizo huoni wewe?
 
View attachment 3465307
Ni wazi ukipita kwenye mitandao ya jamii hasa X, JF na FB unaweza kudhania Samia hapati hata kura 100. Lakini maisha kwa ground ni tofauti kabisa. Ni wakati sasa Mange Kimambi na Polepole wajitathmini. Watanzania hawadanganyiki, kazi ya Samia wanaiona. Njooni mniue
Watanzania wanamsoma yeye na Pole Pole halafu wanapima wenyewe pumba zipi na ngano safi ni ipi.
 
Hizo ndiyo strategy. Hata wakati wa Mkapa kulikuwa na TOT Band chini ya Capt John Komba. Nothing new
Kwa miaka ya sasa ingekuwa ni TOT band pekee inatumika watu wasingeenda kwa wingi mikutanoni kuwashangaa tofauti na wasanii miziki yao inasikika redioni, youtube, video nk
TOT imechuja ndio maana hamuitumii!!.
 
Kwa hiyo ulitaka Rais awafuate Igawilo na Tukuyu, Chimala na Tunduma? You idiot jelousy will kill you
Dog ! Sasa yeye c ndio mhitaji anataka kula na kura kwanini asiwafwate? After all wananchi ndio mabosi wake you Dog!
 
View attachment 3465307
Ni wazi ukipita kwenye mitandao ya jamii hasa X, JF na FB unaweza kudhania Samia hapati hata kura 100. Lakini maisha kwa ground ni tofauti kabisa. Ni wakati sasa Mange Kimambi na Polepole wajitathmini. Watanzania hawadanganyiki, kazi ya Samia wanaiona. Njooni mniue
Hao hapo ni wanafunzi pamoja na watumishi wote wa uma na wanajeshi. Sisi pia ni CCM tunajua. Tujiki
 
Mama Samia anajaza Sana mikutano kiukweli
Mshauri athubutu kufanya mkutano popote bila kusomba watu wala kutumia wasanii...uone tofauti!.
Sa100 mwenyew hata kuhutubia ni tatizo hana mvuto...pale Kawe wasanii walivyomaliza kuimba alivyoanza tu kuhutubia kuna baadhi ya watu walianza kusepa wakawa wanazuiwa na walinzi wa ccm wasubiri mkutano hadi uishe!!!.

Mapenzi ya ccm kwa wananchi kwa miaka ya karibuni ni ya kulazimisha, hebu imagine chadema wangetumia hata nusu tuu ya nguvu ccm wanazotumia ktk mikutano yao hali ingekuwaje?? Nadhani watu wangekuwa wanakufa kwa kukanyagana kwa wingi wa watu mikutanoni!!!!.
 
Mange anachotaka mkutano uwe hata na watu 100, lakini kiuhalisia hao ni watu wachache sana tofauti na kampeni za nyuma za ccm...
Hata camera man anajitahidi kupiga picha katika angle ionekane wamejaza.. lakini hamna kitu..
 
View attachment 3465307
Ni wazi ukipita kwenye mitandao ya jamii hasa X, JF na FB unaweza kudhania Samia hapati hata kura 100. Lakini maisha kwa ground ni tofauti kabisa. Ni wakati sasa Mange Kimambi na Polepole wajitathmini. Watanzania hawadanganyiki, kazi ya Samia wanaiona. Njooni mniue

Tusubiri mpaka siku ya uchaguzi tuone kama siyo njaa nfiyo inayowapeleka watu kwenye hiyo mikutano
 
Mkuu ni ukweli kabisa hauna uelewa wa mambo... kabla ya DP World - Bandari hiyo hiyi ilikuwa inaendeshwa na TICTS ya wazungu... kwani ni Samia ndio aliuza kipindi hicho???

Elewa ile kelele kipindi cha DP ilikuwa ni vita kubwa sana ya kibiashara - na TICTS walifanya vizuri sana kuamsha hisia kupitia fedha walizohonga kila mtu na kuna madeal kibao yalikatwa... walitumia ujinga wa wabongo.. maeneo alokuwa anaendesha TICTS leo ndio anaendesha DP... kipi kigeni hapooo????
Mkuu Smart wajinga wengi Tanzania hii, watu wanakubali kulishwa matango pori.

Pale Bandarini alikuwepo TICTS Kwa miaka 20 inamaana Mkapa aliiuza nchi kwa wakristo?.

Mbona ulipofika muda wao kuondoka walivunjiwa mkataba wakatimua zao?.

Alipokuwa anaendesha TICTS kwa sasa anasimamia Adani na ndio yenye faida kubwa kuliko yale anayosimamia DP World.
 
View attachment 3465307
Ni wazi ukipita kwenye mitandao ya jamii hasa X, JF na FB unaweza kudhania Samia hapati hata kura 100. Lakini maisha kwa ground ni tofauti kabisa. Ni wakati sasa Mange Kimambi na Polepole wajitathmini. Watanzania hawadanganyiki, kazi ya Samia wanaiona. Njooni mniue
Kama watu wanabebwa hadi kutoka makambako unafikiri watu hawata jaa
 
Mshauri athubutu kufanya mkutano popote bila kusomba watu wala kutumia wasanii...uone tofauti!.
Sa100 mwenyew hata kuhutubia ni tatizo hana mvuto...pale Kawe wasanii walivyomaliza kuimba alivyoanza tu kuhutubia kuna baadhi ya watu walianza kusepa wakawa wanazuiwa na walinzi wa ccm wasubiri mkutano hadi uishe!!!.

Mapenzi ya ccm kwa wananchi kwa miaka ya karibuni ni ya kulazimisha, hebu imagine chadema wangetumia hata nusu tuu ya nguvu ccm wanazotumia ktk mikutano yao hali ingekuwaje?? Nadhani watu wangekuwa wanakufa kwa kukanyagana kwa wingi wa watu mikutanoni!!!!.
Hao watu wanaosombwa wanalazimishwa?
 
Mkuu Smart wajinga wengi Tanzania hii, watu wanakubali kulishwa matango pori.

Pale Bandarini alikuwepo TICTS Kwa miaka 20 inamaana Mkapa aliiuza nchi kwa wakristo?.

Mbona ulipofika muda wao kuondoka walivunjiwa mkataba wakatimua zao?.
Mkuu Steven,

Watu wengi Tanzania hawaelewi mambo, hawafuatilii na ni wepesi kurukia kila hoja..

Issue ya Bandari - Mkapa aliwapa TICTS kamouni tanzu ya Hutchson ya western kwa miaka 20. Mkataba uliposiha walitaka wapewe tena Serikali ikapiga chini...

Hapo ndio changamoto ilikuja - walitaka hata kama asipopewa basi apewe Maersk (western mwingine) - Serikali ikaipa DP world (Mwarabu) - vita kubwa ikaibuka....

Bishara nyingi za watu zilipigwa mkasi - walihonga sana wale jamaa kuchafua ile move - lakini Serikali ishaamua (kulikuwa na madudu kibao) siyo kwamba yataisha soon lakini serikali iliona ni muhimu sana kubadili mwekezaji... sasa wananchi ni fuata upepo - mara kabisa limetoa waraka nk nk (kwani Tanzania ndio nchi ya kwanza kuweka mwekezaji kwenye bandari??) nchi karibia zote duniani zenye bandari zinafanya hivyo - zinaacha private sector ifanye.
 
View attachment 3465307
Ni wazi ukipita kwenye mitandao ya jamii hasa X, JF na FB unaweza kudhania Samia hapati hata kura 100. Lakini maisha kwa ground ni tofauti kabisa. Ni wakati sasa Mange Kimambi na Polepole wajitathmini. Watanzania hawadanganyiki, kazi ya Samia wanaiona. Njooni mniue
 
Attachments

  • 20250512_172008.jpg
    20250512_172008.jpg
    45.1 KB · Views: 16
Back
Top Bottom