- Source #1
- View Source #1
Ni wazi ukipita kwenye mitandao ya jamii hasa X, JF na FB unaweza kudhania Samia hapati hata kura 100. Lakini maisha kwa ground ni tofauti kabisa. Ni wakati sasa Mange Kimambi na Polepole wajitathmini. Watanzania hawadanganyiki, kazi ya Samia wanaiona. Njooni mniue
- Tunachokijua
- Mange Kimambi amejitanabaisha kama mwanaharakati wa masuala mbalimbali hususan ya kisiasa. Amekuwa akizungumzia mambo mengi ya kisiasa yanayoendelea nchini Tanzania.
Madai
Hivi karibuni kumeibuka ujumbe ama chapisho linaloonekana kuchapishwa katika ukurasa wa mtandao wa X wenye utambulisho wa Mange Kimambi, Tazama hapa. Chapisho hilo linaandika;
Kiukweli Watanzanua mnakera, mnajaza comments hapa na bado mnajaza mikutano ya CCM. Hapa ni Mbeya leo (Inafutwa).
Je, ni kweli chapisho hilo limeandikwa na Mange Kimambi?
Ufuatiliaji wa kina uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa chapisho hilo si la kweli.
Utafutaji kwa kutumia maneno muhimu yaani Keyword Search, JamiiCheck imejiridhisha kuwa hakuna ujumbe wowote katika ukurasa wa X wenye utambulisho unaonekana kwenye chapisho hilo ambao umechapishwa, hivyo basi chapisho hilo ni la kughushi.
Chapisho hilo linalosambazwa ni la kughushi kwani linakosa baadhi ya vitu muhimu ambavyo vinaonekana katika ukurasa wa X. Mathalani rejelea sehemu ya chini ambayo inaonesha muda na tarehe, inakosekana sehemu inayoonesha views (waliotazama), rejelea pia mpangilio wa tarehe.
Aidha ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa hadi wakati taarifa hii inaandikwa Septemba 05, 2025 ukurasa huo ulichapisha taarifa kwa mara mwisho Juni 16, 2025 na ku repost kwa mara ya mwisho Agosti 10, 2025 ambayo ndiyo taarifa ya mwisho inayoonekana ukiondoa 'Pinned post'. Lakini pia taarifa hiyo haipo katika ukurasa wake wa X ambao ndiyo amekuwa akiutumia mara kwa mara.