Tulishawahi kumkanyaga nyoka wa namna hii kwa gari, nakumbuka uncle ndo alikuwa anendesha tulimpitia tukiwa kama kwenye spidi 80 hivi, gari liliyumba kidogo wakati tunamkanyaga ila tulipogeuka nyuma hatukumuona kumbe alikuwa amenasia chini ya gari GHAFLA kwa spidi ya ajabu ambayo sijawahi kuiona alikigonga kioo cha gari cha dirishani nilipokuwa nimekaa mimi, kioo kilipasuka na yeye kichwa chake kilipasuka palepale...Nashukuru tulikuwa tumefunga vioo maana kama vingekuwa wazi nadhani angenikata kichwa changu kwa ile spidi...usithubutu kumkanyaga na gari umkutapo nyoka wa namna hii.